Je ni lazima kushiriki Meza ya Bwana?

Je ni lazima kushiriki Meza ya Bwana?

Je kama mtu hataki au hajisikii kushiriki meza ya Bwana, na akaamua maisha yake yote kutokufanya hivyo, lakini amri nyingine anashika, je ataokolewa siku ya mwisho?.

Jibu: Shalom.

Yapo maandiko ambayo ni hiari kwetu kuyafanya na yapo ambayo ni maagizo, ambayo ni lazima kila anayejiita mkristo ayafanye.

Mfano wa maandiko ambayo ni hiari sisi kuyafanya au kutoyafanya ni “Ndoa”. Biblia imetoa maagizo ya ndoa lakini haijaweka ulazima wa jambo hilo, maana yake si lazima kuoa au kuolewa, mtu akiamua kukaa bila kuoa au kuolewa hajavunja sheria. (1Wakorintho 7:1-2).

Lakini yapo maandiko ambayo ni maagizo ya lazima kwa kila mkristo, na mojawapo ya hayo ni KUSHIRIKI MEZA YA BWANA.

Mengine ni ubatizo, na kuoshana miguu. Agizo la ubatizo si la hiari bali ni la lazima.

Ni lazima kila mtu baada tu ya kuamini akabatizwe, na si kubatizwa tu!..bali kubatizwa katika ubatizo sahihi.

Na pia ni lazima kila mtu baada ya kuokoka awe mshirika wa meza ya Bwana, maana yake ni lazima ashiriki mwili na damu ya Yesu. Hii ni lazima kama vile agizo la ubatizo lilivyo, haijalishi wewe si mpenzi wa Mkate au divai. Ni lazima ushiriki, kwasababu ni kiwango kidogo tu kinachohitajika kwako sio sufuria nzima ya mikate wala chupa nzima ya divai.

Sasa kwanini ni agizo la lazima?.

Ni kwasababu tusiposhiriki meza ya Bwana Yesu alisema hatuna UZIMA NDANI YETU!.

Yohana 6:53 “Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.

54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho”.

Sasa tukirudi kwenye swali, je! Tusiposhiriki Meza ya Bwana, baada ya kuokoka tutaokolewa?
Jibu ni hilo hapo juu kwamba hatutaokolewa, kwasababu hatutakuwa na uzima, maana yake hatutakwenda kwenye unyakuo na hata tukifa hatutafufuliwa! Kulingana na maandiko hayo!.

Hiyo ikifunua kuwa Neno la Mungu hatulitimizi kama tutakavyo sisi, bali kama atakavyo yeye.

Bwana akisema tushiriki hiyo ni amri kwetu, sio suala la kusema nasikia kichefuchefu, (au sipendagi ngano)..Huna budi kula hivyo hivyo hata kama hupendi.
Kadhalika Bwana akisema tukabatizwe, sio suala la kutoa mapendekezo yetu au hisia zetu, kwamba tunaogopa maji, au tunaogopa kuzamishwa, au hatupendi kuzamishwa..ni lazima kufanya kama Bwana alivyosema, kama tunataka kuokoka.

Lakini kama hutaki siku ile kufufuliwa na kuurithi uzima wa milele, au kama hutaki kunyakuliwa usibatizwe wala usishiriki meza ya Bwana na huku tayari umeshajua umuhimu wa kufanya hayo.

Watakaopata neema ya kuokoka ni wale ambao hawakuwahi kujua wala kusikia juu ya haya, tunayoyasikia sisi..lakini kwa wewe na mimi ambao tayari tumeshayasikia na kujua hivi..tusiposhiriki meza ya Bwana kwa makusudi hatuna udhuru.

Lakini pia hatushiriki tu kama tutakavyo sisi, bali biblia inatuonya tujitakase kwanza, na tujipambanue nafsi zetu kama kweli tunastahili kushiriki, maana yake kama maisha yetu ni ya dhambi, hatuna budi kwanza kumpokea Yesu ndipo tushiriki..

1 Wakorintho 11:27 “Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.

28 Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.

29 Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili.

30 Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala.

31 Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa”.

Bwana atubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Je tunapaswa tushiriki Meza ya Bwana mara ngapi?

NI NINI BWANA ANATAZAMIA KILA TUNAPOSHIRIKI MEZA YAKE.

NI NINI BWANA ANATAZAMIA KILA TUNAPOSHIRIKI MEZA YAKE.

Ni wayahudi wa aina gani wanaotajwa kuwa sinagogi la shetani? (Ufunuo 2:9, Ufunuo 3:9)

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Bishop Johnson Mulewa Karema
Bishop Johnson Mulewa Karema
5 months ago

These teachings are good. Be blessed.