Ni wayahudi wa aina gani wanaotajwa kuwa sinagogi la shetani? (Ufunuo 2:9, Ufunuo 3:9)

Ni wayahudi wa aina gani wanaotajwa kuwa sinagogi la shetani? (Ufunuo 2:9, Ufunuo 3:9)

Ni wale wa wayahudi wa kimwili au kiroho?, yaani ni wale wazaliwa wa Uyahudi au wale walimomwamini Kristo Yesu na kufanyika kuwa wayahudi kwa namna ya rohoni. (Ufunuo 2:9, ufunuo 3:9)?.


Tusome,

Ufunuo 2:9 “Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.

10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima”.

Wayahudi wanaozungumziwa hapo ni wayahudi kwa kuzaliwa kabisa, ambao walikuwa wanajiona kama wao ndio Wayahudi kweli kweli, yaani uzao wa Mungu mteule, lakini Mungu alikuwa anawaona tofauti, kwasababu walikuwa wanaipinga injili ya Masihi, yaani Yesu Kristo, ambaye alitabiriwa katika torati yao hiyo hiyo (Matendo 3:20-24 na Yohana 5:39).. Mfano wa hao ni Mafarisayo na Masadukayo, ambao walikuwa ni wayahudi kwa kuzaliwa lakini walikuwa wanaenda kinyume na maneno ya uzima ya Bwana YESU.

Katika nyakati za kanisa la kwanza, waliokuwa maadui wa kwanza wa Injili ya Bwana Yesu, walikuwa ni wayahudi, ambao walikuwa wanaona wivu wanapowaona watu wengine hususani wa Mataifa wanamgeukia Mungu wa Israeli.

Sasa Kundi hilo la wayahudi wasioamini Injili ya Bwana Yesu na kuipiga vita, ndio Bwana anawaita “sinagogi la shetani”..Na wayahudi hawa walikuwa wamezagaa sehemu nyingi duniani kote, kila walipowaona watu wa mataifa wanamwamini Yesu, walikuwa wanaitumia torati yao kuwavunja moyo na kuwaaminisha mambo yaliyo kinyume na injili ya Kristo.

Matendo 14:1 “Ikawa huko Ikonio wakaingia pamoja katika sinagogi la Wayahudi; na kwa vile walivyonena, kundi kubwa la Wayahudi na la Wayunani wakaamini.

2 Walakini Wayahudi wasioamini wakawataharakisha watu wa Mataifa na kuwatia nia mbaya juu ya ndugu”.

Ni heri kama wangekuwa hawaiamini tu!, lakini walikuwa wanaipiga vita injili ya Bwana Yesu..mfano wa hao ni Mafarisayo na Masadukayo. Mitume waliwatahadharisha sana watu wa mataifa wajihadhari na wayahudi hao, (Kitabu cha Wagalatia chote ni waraka wa Mtume Paulo kwa wakristo wa Galatia, akionesha kuhuzushwa kwake kwa jinsi walivyogeuzwa nia kirahisi na kundi hilo la wayahudi wa uongo, na hata kuiacha injili ya kweli).

Myahudi kweli kweli ni yule anayemwamini Bwana Yesu Kristo na maneno yake kama torati ilivyotabiri.

Kumbukumbu 18:15 “Bwana, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye.”

Sasa hao ndio waliokuwa maadui wa Injili katika kanisa la kwanza, lakini katika siku za hizi za Mwisho vita ni vikali Zaidi, kwasababu shetani hawatumii tena hawa wayahudi kufanya vita na Ukristo. Bali anawatumia wanaojiita wakristo, (ambao kiuhalisia ni wakristo wa uongo) kuuangamiza ukristo wa kweli.

Leo hii ukihubiri injili kamili ya kimaandiko au ukiuishi utakatifu, vita vya kwanza vitatoka kwa “wanaojiita wakristo”.. shetani anawatumia Zaidi wanaojiita wakristo kuliko watu wa mataifa.

Ni kipindi cha kuwa macho sana na kuyasoma maandiko, ili tuweze kuushinda upotofu wa shetani.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?

NI NANI ALIYEKUPA MAMLAKA HII UYATENDE HAYA?

Kwanini Paulo aungane na wale watu wanne wenye nadhiri?

NI KWA NAMNA GANI SHETANI ANAIZUIA INJILI?

MAWE YALIYOKWISHA KUCHONGWA MACHIMBONI.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments