TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?

TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?

HEKALU.

Kulingana na historia ya Taifa la Israeli, tangu zamani wakiwa jangwani walikuwa wanamwabudu Mungu kwa kumtolea Dhabihu za aina mbalimbali mbele ya ile hema ya kukutania kama Musa alivyoagaizwa na Mungu kufanya, Na hema hii ilikuwa ni ya kuhama hama sio rasmi. Lakini mara baada ya kuingia katika nchi yao ya ahadi, Mfalme Daudi baada ya kuona kuwa Mungu hana eneo rasmi la kuliweka jina lake, eneo ambalo watu wa makabila yote ya Israeli yatakusanyika kumtolea Mungu kafara, akaazimia ndani ya moyo wake kumjengea Mungu nyumba.. Hivyo Mungu akasikia matamanio yake, na kuyaridhia lakini kwa masharti kuwa mwanawe ndiye atakayemjengea Nyumba hiyo.

Hivyo mwanawe Sulemani akaja kumjengea Mungu Nyumba kwa mafanikio yote, ambayo Mungu aliitukuza na kuliweka jina lake huko  katika mji wa Yerusalemu..Na Nyumba hiyo  ndiyo iliyoitwa HEKALU. Hivyo Hekalu hili lilikuwa ni moja tu, watu wote walipanda kwenda kumtolea Mungu kafara zao mbele ya hekalu hili lililokuwepo Yerusalemu.

2 Nyakati 7:1 “Basi Sulemani alipokwisha maombi hayo, moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; utukufu wa Bwana ukaijaza nyumba. 

2 Wala makuhani hawakuweza kuingia nyumbani mwa Bwana, kwa kuwa utukufu wa Bwana umeijaza nyumba ya Bwana. 

3 Wakatazama wana wa Israeli wote, uliposhuka ule moto, utukufu wa Bwana ulipokuwapo juu ya nyumba; wakasujudu kifulifuli hata nchi sakafuni, wakaabudu, wakamshukuru Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele”

SINAGOGI.

Lakini mara baada ya wana wa Israeli kuchukuliwa tena utumwani Babeli, na nyumba ya Mungu kubomolewa, kukawa hakuna tena sehemu ya kwenda kumfanyia Mungu ibada na kutoa sadaka za kuteketezwa, Hivyo waliporudi tena Yerusalemu kutoka Babeli, iliwalazimu kuwa na makusanyiko madogo madogo kwa ajili ya kujifunzia torati, na kusoma Zaburi pamoja na Kufanya dua. Hayo ndio yaliyoitwa masinagogi, Na Huko ndipo madhehebu ya mafarisayo na Masadukayo yalipozaliwa. Na  yaliendelea kusambaa karibu sehemu kubwa ya dunia.

Muda rasmi haujulikana yalianza hasaa wakati gani..Lakini ni kipindi cha kati ya kuchukuliwa babeli hadi kipindi cha karibu na kuja kwa Bwana Yesu Kristo.

Na ndio maana Biblia inarekodi Bwana Yesu alikuwa pia akizunguka katika masinagogi yao akihubiri.

Marko 1:38 “ Akawaambia, Twendeni mahali pengine, mpaka vijiji vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko nako; maana kwa hiyo nalitokea.

39  Akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya, na kutoa pepo”

Unaona soma pia (Luka 4:16-21)

KANISA.

Kulingana na tafsiri ya kibiblia kanisa maana yake ni “walioitwa”..Wale walio mwamini Yesu Kristo, wakiwa wamekusanyika wawili au watatu kwa jina lake, tayari hilo ni kanisa. Japokuwa Neno hilo limezoeleka  na wengi kama jengo linalotumiwa na wakristo kuabudia..

Hivyo kwa kuhitimisha hekalu lilikuwa ni moja, ambalo lilijengwa na Mfalme Sulemani, lakaja kubomolewa na Mfalme Nebukadneza wa Babeli, likaja kujengwa tena na Zerubabeli na kubomolewa na Warumi mwaka 70 W.K, Na litakuja kujengwa tena pale Jerusalemu katika siku za mwisho.. Lakini masinagogi yalikuwa mengi, ambayo tunaweza kuyaita makanisa ya wayahudi yakifundisha dini za kiyahudi.. Na makanisa ambayo leo hii tunayaona ni Makanisa ya kikristo yakifundisha imani ya YESU KRISTO..Hiyo ndio tofauti yao.

Shalom.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=4AC-rH1ndvo[/embedyt]

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

Mada Nyinginezo:

Sanduku la Agano lilikuwa linawakilisha nini katika Agano jipya?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 7 (Yeremia na Maombolezo)

Nifanye nini ili niondokane na Hofu maishani mwangu?

Tofuati kati ya Myahudi, Mwisraeli na Muebrania ni ipi?

Nini Tofauti kati ya uzinzi na uasherati ?

Tofauti kati ya ndoto na Maono ni ipi?

TOFAUTI KATI YA SHERIA YA ROHO WA UZIMA NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI!

Tofauti katika ya zaka na sadaka ni ipi?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
10 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

Luka alikuwa mwanafunzi wa Yesu na walikuwa pamoja kila wakati. Je, kwa nini aliandika habari za Yesu kwa kubahatisha bahatisha, na anaanza kwa kusema “naandika hadithi” ! Kwa nini aseme hadithi badala ya kusema “naandika uhalisia”? Maana alikuwa pamoja naye!!

Kingine kwa nini hakuandika miaka ya matukio na tarehe zake?? Maana alikuwa msomi yule na alikuwa shahada ya uuguzi!! Alishindwaje kunakili tarehe za matukio????

AMOS PAUL
AMOS PAUL
1 year ago

Asante sana kwa ufafanuzi mzuri. Nimebarikiwa.

Anonymous
Anonymous
1 year ago
Reply to  AMOS PAUL

Nahitaji mafundisho Zaidi

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Be blessed.

Victor Mwandunga
Victor Mwandunga
2 years ago

Amina. Barikiwa sana mtumishi wa MUNGU

Imani
Imani
2 years ago

I’m on line

Anonymous
Anonymous
2 years ago

uongo huu sinagogi sio kanisa weka andio liseme kanisa sio wewe

Anonymous
Anonymous
3 years ago

Leave your message0703262003