Maandiko yanasema siku zetu za kuishi ni miaka70 tukiwa sana na nguvu ni miaka 80, sasa swali mbona kuna wengine wanaizidi hiyo miaka na kufikisha hata miaka 90?
Tusome,
Zaburi 90:10 “Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara”.
Tunapaswa pia tujiulize kwanini kuna watu hawaifikii hiyo miaka 70 au 80, ambayo Mungu amesema mwanadamu ataiishi, badala yake wanakufa katika umri mdogo na hata wengine katika uchanga kabisa?..Je Mungu ni mwongo?.
Jibu ni la! Mungu si mwongo, alipotaja umri huo wa miaka 70-80 kama ndio umri wa mwanadamu hakumaanisha kuwa ndio amri/sheria kwamba kila mtu ni lazima aufikie huo, na asizidi hapo, hapana! bali alitaja huo umri kama Wastani wa maisha ya mtu.
Maana yake wastani wa umri wa mwanadamu ni kati ya miaka 70 hadi 80. Ikiwa na maana kuwa wanadamu wengi watakufa katikati ya huo umri. Lakini hiyo haimaanishi kuwa ni wote!.. bali wengi wao.
Wapo watakaofika miaka 90 au hata 100, lakini ni wachache sana, ukilinganisha na wanakaokufa kati ya umri wa miaka 70-80. Na wapo watakaokufa chini ya umri huo.
Na kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda ni kama wastani huo wa umri wa wanadamu unazidi kushushwa kutokana na kuongezeka kwa maasi.
Wanadamu wa kwanza walikuwa wanaishi hata miaka elfu, lakini wastani wa miaka hiyo ilikuja kushushwa hadi miaka 120, baada ya gharika..Na ikaja kushushwa zaidi hadi miaka 80 wakati wa Daudi, na sasa pengine wastani huo umeshushwa zaidi, kulingana na uhalisia wa takwimu za watu wanaokufa sasa, ni wachache sana wanaofika hata hiyo miaka 70.
Lakini yote katika yote iwe tunaishi miaka 50 au 80 au 100, maisha yetu duniani bado ni mafupi tu! ukilinganisha na umilele ambao unakuja mbele yetu baada ya kifo.
Itatufaidia nini tuishi miaka 120 ya dhambi hapa duniani halafu tukatumikie mamilioni ya miaka katika ziwa la moto?.
Ni heri tuishi miaka 80 au 100 katika kumtumikia Mungu, na mwisho tukaishi mamilioni ya miaka ya raha katika mbingu mpya na nchi mpya.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
KUJIPAMBA NI DHAMBI?
Binadamu wa kwanza aliishi miaka mingapi?
Nuhu alipataje ujuzi wa kuwatambua wanyama wale wote na kuwaweka ndani ya Safina?
SHUSHANI NGOMENI NI WAPI KWA SASA?
Rudi nyumbani
Print this post
Mwenyezi MUNGU atujalie kutimiza amri Mwenyezi MUNGU atujalie kutimiza amri zake.
Amen