Biblia inamfananisha Bwana wetu Yesu Kristo na Melkizedeki kuhani wa Mungu aliye hai.. Na hiyo yote ni Kutokana na jinsi alivyofanana na Kristo kwa kila tabia aliyokuwa nayo.
Waebrania 7:1-3 [1]Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; [2]ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani; [3]hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.
Waebrania 7:1-3 [1]Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;
[2]ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;
[3]hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.
Sasa kama wewe ni msomaji wa biblia utajiuliza ni kwanini siku ile Ibrahimu alipotoka kumwokoa ndugu yake Lutu ambaye alikuwa tayari ameshatekwa na maadui, Melkizedeki hakumpa zawadi nyingine zaidi ya MKATE NA DIVAI..
Jiulize ni kwanini iwe mkate na Divai, na ni kwanini uwe ni wakati ule? Na si mwingine..kwanini Melkizedeki asingempa Dhahabu na Lulu kama pongezi, au kwanini asingempa kondoo na mbuzi kama zawadi kwake..badala yake anampa divai na makate, kitu kidogo tu.. kuna nini?
Mwanzo 14:17-20 [17]Abramu aliporudi kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme. [18]Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. [19]Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. [20]Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.
Kama tulivyotangulia kuona kuwa Melkizedeki anafananishwa na Yesu Kristo kwa kila kitu..Habari hiyo inajirudia kwa Kristo alipokuwa anaondoka duniani..
Hakuwaacha hivi hivi tu mitume wake, bali aliwapa uzima wake kwa mfano wa mkate na divai akasema huu ndio mwili wangu na damu yangu imwagikayo kwa ajili ya ondoleo la dhambi, kuleni huu, na nyweni hii kwa ukumbusho wangu na kutangaza mauti yake inayowaokoa watu (Mathayo 26:28)
Sasa tarajio lake kubwa ni kutuona sisi tunashiriki ipasavyo..anatarajia kutuona tupo katika mazingira kama ya Ibrahimu..ambaye yeye hakuona vema kukaa tu hivi hivi angali ndugu yake Lutu amechukuliwa mateka..aliamua kutoka aende kumkomboa, kutoka mikononi mwa wale wafalme wa mbali.
Na ndipo Mungu alipouona moyo huo wa Ibrahimu akaona anastahili kushiriki mwili na damu ya Yesu Kristo.
Lakini je! Tujiulize na sisi tangu tulipoanza kwenda makanisani, na kushiriki meza ya Bwana mara zote hizo..Je! Ni ushuhuda gani Kristo anauona ndani yetu aone kwamba tumestahili kuishiriki meza yake.
Kila tendo la rohoni lina kanuni yake.. Ili ule uzima ambao Bwana Yesu alisema utaingia ndani yetu pale tu tunaposhiriki meza yake, uingie, ni lazima tujue kanuni zake vinginevyo tutakuwa tunafanya kazi bure tu.
Yohana 6:53-54 [53]Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. [54]Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
Hivyo, tukumbuke hilo pia tukaribiapo nyumbani kwa Bwana anatazamia tuwaangazie na wengine nuru yetu ya wokovu tuliyoipokea..Ndipo tustahili vema kushiriki meza yake. Lakini kama tutakuwa ni watu wa kuingia kanisani na kutoka, baada ya hapo hatuna habari tena na Mungu. Ni heri tuache tu.
Bwana atasaidie katika hilo.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU.
Je tunapaswa tushiriki Meza ya Bwana mara ngapi?
Je Lutu alikwenda kuwahukumu watu wa Sodoma na Gomora? Kulingana na Mwanzo 19:9?
NI WAPI MAHALI SAHIHI PA KULIPA ZAKA?
BWANA alimaanisha nini kwenye mstari huu Marko 2:21″ Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kukuu?
Rudi nyumbani
Print this post
Thanks 🙏🙏🙏
Amen