Marago ni nini? ( Waamuzi 10:18)

Marago ni nini? ( Waamuzi 10:18)

Marago ni mahali ambapo watu wanaweka makao ya muda kwa makusudi maalumu.

Kwamfano watu zamani walipokuwa wanakwenda vitani, waliweka makempu au makambi au mahema mahali mahali…hayo ndio yaliitwa marago..

Kwamfano ukisoma..

Waamuzi 10:17-18 inasema..

[17]Wakati huo wana wa Amoni walikutana pamoja, wakapanga marago huko Gileadi. Wana wa Israeli nao wakajikusanya wakapanga marago Mispa.

[18]Na hao watu, wakuu wa Gileadi, wakaambiana wao kwa wao, Je! Ni mtu yupi atakayeanza kupigana na wana wa Amoni? Yeye atakuwa ni kichwa juu ya wenyeji wote wa Gileadi.

Ikiwa na maana wote waliweka kambi zao za kijeshi huko Mispa.

Hali kadhalika Wana wa Israeli walipokuwa katika safari yao ya kuelekea nchi  ya ahadi waliweka makazi ya muda sehemu kadha wa kadha..

Kwamfano ukisoma..

Kutoka 29:13-14

[13]Kisha twaa mafuta yote yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo juu yake, uyateketeze yote juu ya madhabahu.

[14]Lakini nyama yake huyo ng’ombe, na ngozi yake, na mavi yake, utayachoma kwa moto nje ya marago; ni sadaka kwa ajili ya dhambi.

Akiwa na maana hivyo viungo vya ndani watavichoma mbali na pale wana wa Israeli walipoweka makambi..

Neno hilo italisoma pia katika vifungu hivi;

Kutoka 36:6, Walawi 4:21, 10:5, Waamuzi 21:12.

Ni nini twajifunza kwa habari za marago.

Hata sisi hapa duniani ni kama tupo maragoni..Hatuna makazi ya kudumu..tumewekwa kwa makusudi maalumu..kusudi hilo likiisha..hakuna kukutanika tena..

Ibrahimu alilijua hilo..Kiasi kwamba japokuwa alikuwa na tajiri na mwenye mali nyingi..Moyo wake hakuuweka hapa duniani, hata kidogo..Bali kule kwenye mbingu mpya na nchi mpya(YERUSALEMU MPYA)..Na hiyo ndio ilikuwa sababu ya kuitwa Baba wa imani..Aliishi kama mpitaji hapa duniani..

Waebrania 11:9-10

[9]Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.

[10]Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu….

[14]Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe.
[15]Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea.
[16]Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.

Je na sisi twaweza fanana na Ibrahimu?

Je tunaweza kuwa kama Ayubu ambaye japo alipoteza kila kila hakutetereka katika imani yake..kinyume chake ndio analibariki jina la Bwana.?

Hivyo nasi tuishi kama wapitaji. Kwasababu tukiwa ni watu wa namna hii, tunapata faida zote mbili kwanza ulimwengu hauwezi kutuzomba tukamsahau Mungu. Na pili Bwana atatubariki hata kwa hivyo tusivyovitazama..Kwasababu mioyo yetu haipo huko.

Bwana atusaidie.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Shetri ni nini kama tunavyosoma katika Marko 3:38?

Neno Buruji lina maana gani katika biblia?

Pomboo ni nini katika biblia?(Kutoka 25:5, Ezekieli 16:10)

Gumegume ni nini? (Isaya 50:7)

HERI WAPATANISHI, MAANA HAO WATAITWA WANA WA MUNGU

Easter ni nini?..Na je tunaruhusiwa kuisheherekea?

JIHUDHURISHE, ILI AANZISHE MAZUNGUMZO NA WEWE

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments