Jibu: Tusome,
Marko 4:35 “Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo. 36 Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye 37 Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. 38 Naye mwenyewe alikuwapo katika SHETRI, amelala JUU YA MTO; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?”.
Marko 4:35 “Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo.
36 Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye
37 Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji.
38 Naye mwenyewe alikuwapo katika SHETRI, amelala JUU YA MTO; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?”.
Katika kisa hicho tunaona Wanafunzi walimchukua Bwana Yesu kama alivyo (yaani bila ya kitu chochote cha njiani kama vile chakula, au mavazi). Walimchukua kama alivyo..Na kumchukua kunakozungumziwa hapo ni kumchukua, kama vile mtu anavyomchukua mwenzake na kumpa lifti ya gari, ndivyo wanafunzi walivyomchukua Bwana Yesu..
Lakini tunaona walipokuwa njiani ndani ya ile Merikebu, Bwana Yesu alienda kulala katika Shetri ya Merikebu.
Sasa “SHETRI” au kwa lugha nyingine “TEZI”, ni sehemu ya Nyuma ya Meli au Merikebu, ambayo ni pana, na ndiyo iliyotumika katika kuwekea mizigo, na pia ndipo palipotengenezewa vyumba vya kulala watu. Sehemu ya mbele ya Meli au Merikebu inaitwa “OMO”, ambayo ni nyembamba ili kuisiaidia meli kukata mawimbi.
Sasa Bwana Yesu alienda kulala kwenye Shetri, mahali ambapo kulikuwa na nafasi ya kulala, na akawa amelala juu ya mto! (Mto unaozungumziwa hapa sio mto wa kutiririsha maji, bali ni ule mto wa kulalia kitandani, kuupatia shingo egemeo bora). Na akiwa Dhoruba ikaanza, na chombo kikakaribia kuzama..na Baadaye wanafunzi wakamwamsha Bwana na Bwana Yesu akaikemea ile Dhoruba ikatulia.
Sasa kikubwa tunachoweza kujifunza katika tukio hilo ni kuwa, Bwana Yesu anaweza kuwa yupo ndani yetu lakini amelala!. Tusipopaza sauti zetu kwa nguvu kwa maombi, basi tutahangaika na Dhoruba zilizopo nje, na wala yeye hatasema chochote.
Hii inatukumbusha kuwa waombaji, na si waombaji tu, bali waombaji wenye bidii, wenye kupaza sauti mpaka majibu ya maombi yatokee.
Bwana atusaidie katika hayo.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Ahera ni wapi? Kama tunavyosoma katika biblia.
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
Bustani ya Edeni ipo nchi gani?
MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.
NI NINI TUNAJIFUNZA KWA DEMA NA MARKO?
Rudi nyumbani
Print this post