SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!

SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!

Lengo la Mungu kuwapa watu amri ya kuitunza sabato lilikuwa ni tofauti na lilivyochukuliwa au kutafsiriwa.Tuchukue mfano wa kawaida wa kimaisha…

Kikawaida, kila mtu ni lazima katika siku moja anao muda wa kulala (kupumzika), ili mwili wake uwe katika ustawi bora, hakuna mtu asiyelala kabisa.Hivyo ni sawa na kusema usingizi umeumbwa kwa ajili yetu sisi, ili tupate kuwa na afya bora na sio sisi tumeumbwa tuutumikie usingizi.
Kwa mantiki hiyo basi, ingawa tuna sheria ya kulala kila siku, lakini hatuna sheria ya muda wa kulala au wakati wa kulala.

Wengine watalala kuanzia saa 3 usiku na kuamka saa 11 alfajiri ili kuwahi shughuli zao..hivyo wakawa wamelala masaa 8.

Wengine wataanza kulala kuanzia saa 6 usiku na kuamka saa 2 asubuhi na wakawa wamelala masaa yaleyale 8..wengine hawatalala kabisa usiku bali watalala mchana..

Hao wote wametimiza sheria ya kulala,ilitowekwa na Mungu, hakuna hata mmoja aliyeivunja..isipokuwa kila mtu kaitimiza kwa wakati wake aliouona unafaa.

Hivyo muda wa kulala haujalishi kinachojalisha ni masaa na matokeo baada ya kulala..kwamba wote mtalala na miili itakuwa imepumzika..Na usipolala mwili wenyewe utakutumia taarifa ya deni la usingizi, hivyo hilo deni utalilipa tu, na taarifa hiyo sio Mungu anayekutumia bali ni mwili ndio unaokutumia.

Lakini sasa inapotokea kwamba ni amri kwamba kila saa 3 usiku mpaka saa 11 asubuhi watu wote wawe vitandani wamelala, hapo tutakuwa tunauabudu usingizi, tutakuwa ni watumwa wa usingizi, na tutakuwa wajinga na maana ya kulala itakuwa imepotea kabisa.

Kwasababu kuna wakati itakubidi uwahi kulala ili uwahi kuamka, kuna kipindi utachelewa kulala kutokana na dharura za kimaisha na hivyo utajikuta unachelewa kuamka pia, kuna wakati utaugua utakuwa kitandani muda wote, au usiwe unapata usingizi kabisa..Hivyo usingizi upo lakini ni sisi ndio tunaouendesha na sio wenyewe unatuendesha sisi..Hatuwi watumwa wa usingizi!

Na Sabato ni hivyo hivyo..

Maandiko yanasema Sabato ilifanyika kwaajili yetu na sio sisi kwaajili ya sabato.

Marko 2:27 “Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato”

Mungu aliiweka sabato ili tupumzike tupate muda wa kumtafakari yeye, na kutengeneza mambo yetu ya kiroho katika wiki inatofuata mbele yetu, kama vile usingizi ulivyowekwa kwamba tupumzike ili miili yetu istawi, ipate nafasi ya kujitengeneza upya kwaajili ya kuiendea siku inayofuata.
Hivyo ni kweli tumepewa amri ya kuishika sabato, lakini hiyo hatuishiki kwa kanuni fulani maalumu, kwamba ni lazima iwe ni kila jumamosi, kiasi kwamba mtu ukiabudu siku tofauti na hiyo ni kosa!…au kwamba ni lazima iwe kila jumapili kiasi kwamba mtu akiabudi jumamosi ni kosa, hapo tutakuwa hatujaelewa maana ya Sabato!.

Hivyo siku ya Bwana ni chaguzi wetu, kwamba siku ipi ni bora kwetu, kama ni jumamosi, au jumapili, au jumatatu, au jumanne au siku nyingine yeyote maadamu, katika hiyo tutaifanya siku nzima iwe takatifu kwa Bwana.

Kulingana na mfumo wa kalenda ya nchi yetu, siku ambazo hazina masumbufu ni jumamosi na jumapili, hizo ni siku ambazo ni nzuri kuzifanya kuwa za Bwana, lakini pia sio amri, hata jumanne ni siku iliyokubalika, hata jumatano, lakini shida ya siku hizo ni kwamba zina masimbufu mengi ya kimaisha, hivyo ni ngumu kuzitakasa.

Mataifa ya kiarabu, siku ya ijumaa ndio siku isiyo na masumbufu kwao, kama vile ilivyo jumapili na jumamosi kwetu, kwao ni ijumaa…hivyo siku kama hiyo kulingana na kalenda za mataifa hayo ni vizuri kuifanya siku ya Bwana iwe Ijumaa kuliko jumapili au jumamosi kwasababu, siku ya jumapili ni sheria watu wao kwenda makazini kama kawaida tofauti na huku kwetu.

Ni jambo la aibu mkristo kushindania siku ya kuabudu.
Utakuta mtu hafahamu kitu kingine chochote zaidi ya kushabikia jumamosi au jumapili. Mtu kama huyo anakuwa hana tofauti na mtu anayeshabikia muda wa kulala.

Bwana atupe macho ya kuyaona haya, na tutokane na upofu huo, ambao unaufanya ukristo usieleweke kwa watu waliopo nje.

1 Wakorintho 14:40 “Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu”

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Neno Saumu lina maana gani katika biblia?

IMESALIA RAHA YA SABATO KWA WATU WA MUNGU.

TUSIRUHUSU MAMBO YA KUSUBIRISHA, YAVURUGE MUDA WETU NA MUNGU.

Neno Saumu lina maana gani katika biblia?

Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments