Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tuyatafakari pamoja maneno ya uzima ya Mungu wetu.
Kuna wakati mtume Petro alialikwa kama mgeni, nyumbani kwa mtu mmoja aliyeitwa Simoni, Lakini siku moja alisikia njaa sana, Na njaa ile inaonekana haikuwa ya kawaida, pengine Petro hakula kitu chochote tangu jana yake, hivyo ulipofika muda wa chakula ikambidi akatafute kitu cha kula, lakini biblia inatuambia muda huo ndio walikuwa katika maandalizi kwamaana ilikuwa ni saa sita mchana..
Lakini tunaona Petro hakusubiri mpaka chakula kiive, ale kwanza ndio aendelee na shughuli zake za ibada, bali alitumia muda huo kuingia uweponi mwa Mungu ili aombe katika njaa yake, aliendelea hivyo mpaka alipozimia katika maono, ndipo Mungu akatumia Ono linalofanana na njaa yake kumfunulia Siri kubwa sana ya ukombozi, ambayo haikuwahi kufunuliwa kwa vizazi vyovyote vilivyomtangulia. Na siri yenyewe ilikuwa ni kuhusu “Ukombozi wetu sisi watu wa mataifa”
Matendo 10:9 “Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana; 10 akaumwa na njaa sana, akataka kula; lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia, 11 akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi; 12 ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani. 13 Kisha sauti ikamjia, kusema, Ondoka, Petro, uchinje ule”.
Matendo 10:9 “Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana;
10 akaumwa na njaa sana, akataka kula; lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia,
11 akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi;
12 ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani.
13 Kisha sauti ikamjia, kusema, Ondoka, Petro, uchinje ule”.
Sasa nachotaka tuone ni kuwa, wakati wa kusubiria huduma, Petro hakuona vyema muda huo upite hivi hivi tu, ni heri autimie kwa Bwana, hata kama atakuwa katika njaa.
Hata sasa, sisi kama watumishi wa Mungu, sisi kama wakristo, tunavurugiwa muda wetu kwa Mungu, kwasababu tu ya huduma tunazozisubiria za kimwili,. Na hiyo imetufanya tukose kuzijua siri nyingi za Mungu katika maisha yetu, na kanisa.
Wakati tunasubiri kwenda masomoni, kwanini tusitumie muda huo hapo katikati kuutafuta uso wa Mungu, au kuifanya kazi yake, kwanini tusitumie kuhudhuria mikesha, au kumfanyia Mungu ibada, nani ajuaye atatuonyesha njia iliyo bora zaidi, kuliko hiyo tuliyokuwa tunaiendea?.
Wakati tumemaliza chuo tunasubiria kupata kazi, ni sawa na kusema njaa ya kazi imekushika, kwanini usiende kuhubiri injili na wengine mitaani, kuliko muda wote, kuwaza ufanye hiki au kile ili utoke, hujui kuwa unapoteza muda wako mwingi kusubiria na wakati mwingine inapita hata miezi au miaka, ukisumbukia tu hicho hicho kitu kimoja ambacho bado hujakipata, kwanini usitumie muda huo ukiwa nyumbani, kuhudumu nyumbani kwa Mungu.
Wakati unasubiria kuolewa, njaa ya kuolewa imekukamata, pengine umri umeenda sana, ujana unakukimbia, Embu fanya kama Petro, wakati Mungu anakuandalia mume wako, au mke wako, tumia muda huo kujishughulisha na masuala ya Mungu, usipoteze muda wako mrefu kutanga tanga huku na huko, au kujiweka hivi au vile, vitakupotezea tu muda, wakati muda huo Mungu angekuwa anakufunulia mambo makubwa na ya ajabu.
Wakati njaa ya mafanikio imekushika, unasubiria siku ya kupewa mkopo ifike, au kupandishwa cheo, au kupata promosheni, kwanini usijishughulishe na mambo ya ufalme wa mbinguni?, kuliko kutwa kuchwa, unapambana umpendeze huyu au Yule, ili upate upendeleo, unakosa hata muda na Mungu wako, upo buzy kusubiria kitu ambacho bado kipo kwenye maandalizi.
Hivyo, tujifunze kuutumia muda wetu vizuri kama mitume, kwasababu hapa duniani, mambo ya kusubirisha yapo mengi. Na huwa yanavuruga akili kweli, na kupotezesha muda sana, kwa mfano unapoona wengine wamepata kazi wewe huna, fikra zako zote ni rahisi kuelekea kwenye njia mbalimbali, ili tu na wewe ukipate kwa haraka kama wao walivyopata, na hapo ndipo kumsahau Mungu kunapokuja, au kupunguza muda wako na Mungu kunapokuja. Kwasababu unapigana ili na wewe usipitwe nyuma Hivyo, hali kama hiyo ikikukuta wakumbuke mitume, Kwasababu hata wao walikuwa na sababu zote za kusubiri, lakini walitumia muda wao wa hapo katikati vizuri na ndio maana mpaka leo hii tunafaidi matunda ya kujitoa kwao.
Vivyo hivyo na sisi tusiruhusu hata kidogo mambo ya kusubirisha yatuvurugie muda wetu na Bwana. Tusiruhusu njaa zetu, zimweke Mungu nyuma.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
NJAA ILIYOPO SASA.
KWASABABU MUDA TULIOBAKIWA NAO SI MWINGI.
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3
KU WAPI, EWE MAUTI, KUSHINDA KWAKO?
Rudi nyumbani
Print this post
Leave your message Mpendwa biblia inaposema “yohana1.1-2” hapo mwanzo kulikuwako neno naye neno alikuwa mungu,huyo mwanzo aliwako kwa mungu…swali! Kuna uhusiano gani kati ya “neno” “mwanzo” na “mungu”?
Biblia inasema yeye ndio Mwanzo na Mwisho.. Ufunuo 1:8,Ufunuo 21:6 na Ufunuo 22:13