Nakusalimu katika jina la Mkuu ya uzima, Mfalme wa wafalme, Bwana wetu Yesu Kristo. Sifa heshima na utukufu vina yeye milele na milele Amina.
Karibu tujifunze biblia. Leo tutatazama viashiria vikuu vitakavyomtambulisha huyo mpinga—kristo ambaye anatarajiwa kuja duniani. Kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na mikanganyiko mwingi, kuhusiana na ujio wake, na chapa yake ya 666, na hiyo imepelekea wengine kudhania kuwa mpinga-Kristo ni mkuu wa freemason atatokea kuzimu au ni ugonjwa wa Corona, kwamba mtu akichanjwa tayari ameshaipokea hiyo chapa ya 666. Lakini je! Biblia inatufundisha hivyo?
Ni kweli Bwana Yesu alisema wapinga-kristo wengi watatokea duniani, ambao kimsingi hadi sasa wapo wengi, lakini yupo mmoja ambaye atakuja. Ili kuleta uharibifu huku ulimwenguni (Soma 1Yohana 2:18). Ambaye ndio huyo tutakayekwenda kusoma tabia zake, na kwamba tukiona hizo zote zipo ndani yake, basi tujue ule mwisho umefika, tayari ameshafunuliwa, dunia imebadikiwa na kipindi kifupi sana zisichozidi miaka 7 (2Wathesalonike 2:1-6).
Zifuatazo ni tabia zitakazomtambulisha.
1) ATATOKEA KATIKA DINI KONGWE.
Mpinga-kristo tofauti na watu wanavyodhani kwamba atazuka tu ghafla kama mwanaharakati Fulani, pasipokuwa na chanzo, hapana, biblia inatuonyesha atatokea katika utawala utakaokuwa unaongoza ulimwengu wakati huo, ambao ulishawahi kuongoza pia hapo kabla, Na utawala wenyewe ni Rumi-ya-rohoni, na utakuja kupata nguvu tena kipindi cha kukaribia mwisho wa dunia, na utafanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu tu, yaani kwa maelezo mafupi ni kuwa mpinga-Kristo hatotokea mahali pengine isipokuwa katika ofisi ya UPAPA.
Ufunuo 17:11 “Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu”
2) DUNIA NZIMA ITAMSTAAJABIA:
Tabia nyingine ni kuwa dunia nzima itamstaajabia, kustaajabia maana yake ni kushangazwa na matendo yake, na ukuu wake, ikiwa na maana atakubalika sana na makundi yote, biblia inasema mataifa yatakubaliana naye, na watu wa itikadi zote, na kabila zote, na jamii zote za watu ulimwenguni. Hakuna hata mmoja atakayemwona kuwa ni mtu mwovu, isipokuwa tu wale masalia machache yatakayokuwa yamebaki duniani wakati huo.
Ufunuo 13:3 “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule…. 8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia”.
Ufunuo 13:3 “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule….
8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia”.
Lakini sio Corona, au mtu Fulani mbaya, mwenye mapembe ambaye, leo hii anaogopeka, hapana mpinga-Kristo ataonekana ni mkombozi wa ulimwengu wakati huo.
3) ATAITWA MTU WA AMANI:
Sio mtu wa vurugu, au mchinjaji, kwani mikakati atakayokuwa ameipanga na ulmwengu, italenga katika kuleta amani ya dunia, na hivyo jambo lolote atakalolianzisha, au mfumo wowote atakaouleta duniani utapokewa na mataifa yote kwa moyo mmoja, na huko huko atapatia nguvu ya kuileta chapa yake yenye 666 ndani yake, na kwamba hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kuuza au kununua asipokuwa nayo.
Danieli 11: 21 “Kisha badala yake atasimama mmoja, mtu astahiliye kudharauliwa, ambaye hawakumpa heshima ya ufalme; naye atakuja wakati wa amani, naye ataupata ufalme kwa kujipendekeza. 22 Na wale wenye silaha mfano wa gharika watagharikishwa mbele yake, na kuvunjika, naam, mkuu wa maagano pia”.
Danieli 11: 21 “Kisha badala yake atasimama mmoja, mtu astahiliye kudharauliwa, ambaye hawakumpa heshima ya ufalme; naye atakuja wakati wa amani, naye ataupata ufalme kwa kujipendekeza.
22 Na wale wenye silaha mfano wa gharika watagharikishwa mbele yake, na kuvunjika, naam, mkuu wa maagano pia”.
4) ATAKUJA NA ISHARA NA MIUJIZA YA UONGO:
Mpinga-Kristo atakuwa na uwezo pia wa kufanya miujiza, Kwasababu roho ya shetani itakuwa nyuma yake, mfano wa Yane na Yambre kipindi kile walipokuwa wakishindana na Musa, ambao tunaona nao pia shetani aliwapa uwezo wa kufanya miujiza,. Ili tu kushindana na kuwapinga watakatifu wa Mungu. Hivyo mpinga-Kristo naye atakuwa na uwezo huo wa shetani,lengo likiwa ni kuwachukua wale ambao watadhani ni yeye ni mpinga Kristo.
2Wathesalonike 2:8 “ Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake; 9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; 10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. 11 Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; 12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu”
2Wathesalonike 2:8 “ Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
9 yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
10 na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa.
11 Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo;
12 ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu”
5) ATATAKA KUABUDIWA KAMA MUNGU.
Kwasababu atakuwa ni mtu wa rohoni, na vilevile mtu wa mwilini, lengo lake litakuwa ni kufikia kilele cha kiti cha enzi cha Mungu duniani. Atataka watu wamwone yeye kama Mungu,.Hivyo atajiinua juu ya dini zote, na madhehebu na imani zote duniani, ili apewe sifa na utukufu kana kwamba ni yeye ni Kristo.
2Wathesalonike 2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; 4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu”.
2Wathesalonike 2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;
4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu”.
6) ATATOA MANENO YA MAKUFURU.
Kutaka kuwa kama Mungu tu peke yake haitoshi, bado atakuwa anaitukana njia ya wokovu, Ataukandamiza ukristo wa kweli pia, atadiriki kumtakana Mungu anayeabudiwa na watakatifu. Ili tu aonekane yeye ndio kila kitu.
Ufunuo 13:5 “Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. 6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. 7 Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa”
Ufunuo 13:5 “Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.
6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.
7 Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa”
7) HESABU YA JINA LAKE ITAKUWA NI 666.
Vilevile jina lake litakuwa ni hesabu ya 666. Yaani ukizihesabu tarakimu za jina lake, ni lazima ziishie na jumla ya 666
Ufunuo 13:16 “Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; 17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. 18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
Ufunuo 13:16 “Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;
17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
Sasa haya yote kwa jumla ukiyaona kwa wakati mmoja ndani ya huyo mtu mmoja, basi ujue huyo ndiye mpinga-Kristo mwenyewe, ambaye ataipelekea duniani ifikie kiama chake. Wakati huo ukifika dunia haitakuwa na zaidi ya miaka 7 tu mpaka itakapoisha, Na kulingana na maandiko watakaokumbana na kazi zake ni wale wote ambao hawatakwenda katika unyakuo, ambao hivi karibuni unakwenda kutokea.
Huyu mpinga-Kristo ataleta dhiki kubwa sana kwa wale watakaoachwa katika unyakuo. Kwasababu hutaruhusiwa kuuza wala kununua kama huna chapa yake. Ni dhiki ambayo watu watatamani vifo lakini vifo vitawakimbia.
Dalili zote zimeshatimia, Na huyu mtu wakati huu pengine anaishi duniani, ndio, anaishi duniani, kwasababu atatokea katika dini kongwe duniani, ya kirumi, katika kiti cha UPAPA,.kinachongojewa tu ni unyakuo wa kanisa, na baada ya hapo, aanze kutenda kazi yake ya kuuharibu ulimwengu. Huyu ndio lile Chukizo lenyewe la uharibifu linalozungumziwa katika maandiko.
Ndugu Je! Hadi sasa upo upande gani, Yesu akirudi leo utakuwa mgeni wa nani huko uendako?. Jibu unalo.
Maran Atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
UNYAKUO.
UFUNUO: Mlango wa 18
YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.
Je ni sahihi kusikiliza miziki ya kidunia?.
UFUNUO: Mlango wa 14
Rudi nyumbani
Print this post
Mafundisho haya nimazuri Sana kwamaana yanasaidiya watukwa kujitambua,na kujuwakujitayarisha kwamaishayakiroho,nilikuwanahitajikujifunzazaidi.
Amina, Mungu awabariki kwa mafundisho mazuri, lakini samahani nina swali kwa somo hili umesema kwamba mpinga kristo atatokea katika ofisi ya upapa, na andiko la uthibitisho ni la (ufu17:11) sasa hapo biblia inasema uyo atakaenda kwenye uharibifu ni wa nane, mbona kwa sasa papa aliyeko ni wa 266 ambaye ni Fransisco? maanake uyo wa nane si alishapita zamani sana…?
Amen nawe pia ubarikiwe.
Anapotaja wanane hamaanishi kuwa ni papa wa 8, hapana.. bali ni namba inayofuatia baada ya vile vichwa 7.. Ukisoma kwa makini ufunuo wa vile vichwa saba.. Kuelewa kwa urefu vile vichwa saba ni nini, unaweza kufungua hapa VICHWA SABA
Unaweza kufungua hapa utapata jibu> VICHWA SABA