TEGEMEA MUNGU KUZUNGUMZA NAWE KATIKA MAMBO MADOGO

TEGEMEA MUNGU KUZUNGUMZA NAWE KATIKA MAMBO MADOGO

Shalom, karibu tujifunze maandiko.

Kama kuna njia tunaiendea ambayo itakuja kuleta majuto mbele yetu, basi Mungu wetu huwa anatangulia kututahadharisha kabla ya hatari yenyewe kutufikia!..Lengo ni tuiache hiyo njia ili madhara yasitukute!

Lakini jambo la kuogopesha ni kwamba mara nyingi Mungu hatumii tu mambo makubwa kututahadharisha,  au kuzungumza na sisi, bali pia  anatumia vitu vidogo, na vilivyo dharaulika, na visivyo na heshima kuzungumza na sisi au kututahadharisha..

Wakati Fulani Mungu alitumia Punda kumtahadharisha Balaamu, hatari iliyopo mbele yake.. Ghafla akiwa njiani kuelekea kufanya jambo ambalo ni kinyume na mapenzi ya Mungu, punda wake aliyempanda alifunga breki ghafla wakiwa katikati ya safari!.. Na kwasababu alimdharau mnyama Yule pasipo kujua kuwa kusimama kule kwa punda wake kusikokuwa kwa kawaida,  inawezekana kuna jambo, lakini yeye hakulitafakari hilo..badala yake aliona ni punda tu!, na kuanza kumpiga!.. Kumbe Mungu alimtumia punda kuyanusuru maisha yake asiende kufa!! (habari hiyo kwa urefu unaweza kuisoma katika kitabu cha Hesabu 22).

Sio huyo tu!, tunaweza kujifunza kwa mtu mwingine ambaye alitahadharishwa na mnyama lakini hakusikia.. Na huyo si mwingine zaidi ya Petro.

Wakati Fulani Petro alifikia hatua ya kufanya jambo la hatari la kumkana Bwana, na wakati anaanza tu! Kumkana kwa mara ya kwanza.. Maandiko yanasema Jogoo aliwika!, sasa sauti ile ya jogoo!, haikuwa ya kawaida.. Petro aliona ni sauti ya kawaida tu!, kumbe ni Roho Mtakatifu aliingia ndani ya jogoo na kumfanya awike muda ule, ili kumtahadharisha Petro kuwa anakoelekea sio kuzuri, lakini  Petro hakuelewa chochote, akaendelea kumkana Bwana kwa mara nyingine ya pili na ya tatu!, lakini Mungu jinsi alivyo wa huruma akazungumza naye tena kupitia Yule Yule jogoo ili kwamba aache hiyo njia, atubu lakini tunaona  jogoo alipowika tena mara ya pili bado Petro hakuelewa wala kukumbuka.. Mpaka Bwana alipomgeukia na kumtazama, ndipo Petro akafahamu na kukumbuka, na kwenda kutubu…Kama tu Balaamu baada ya kufumbuliwa macho na kumwona Yule malaika, ndio akatambua!.

Marko 14: 66 “Na Petro alikuwa chini behewani; akaja mmoja wa vijakazi wa Kuhani Mkuu,

67  akamwona Petro akikota moto; akamkazia macho, akasema, Wewe nawe ulikuwapo pamoja na yule Mnazareti, Yesu.

68  Akakana, akasema, Sijui wala sisikii unayoyasema wewe. Akatoka nje hata ukumbini; JOGOO AKAWIKA.

69  Na yule kijakazi akamwona tena, akaanza tena kuwaambia waliosimama pale, Huyu ni mmoja wao.

70  Akakana tena. Kitambo kidogo tena wale waliosimama pale wakamwambia Petro, Hakika u mmoja wao, kwa sababu u Mgalilaya wewe.

71  Akaanza kulaani na kuapiza, Simjui mtu huyu mnayemnena.

72  NA MARA  JOGOO AKAWIKA MARA YA PILI. Petro akalikumbuka lile neno aliloambiwa na Yesu, Kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu. Na alipolifikiri, akalia”

Sasa ili tuzidi kuelewa vizuri baada ya jogoo kuwika mara ya pili ni nini kilitokea… hebu tusome tena habari hiyo katika kitabu cha Luka..

Luka 22:59  “Halafu, yapata saa moja, mtu mwingine alikaza kusema, Hakika na huyu alikuwa pamoja naye, kwa kuwa yeye pia ni Mgalilaya.

60  Petro akasema, Ee mtu, sijui usemalo. Na papo hapo alipokuwa katika kusema, jogoo aliwika.

61  BWANA AKAGEUKA AKAMTAZAMA PETRO. Petro akalikumbuka lile neno la Bwana jinsi alivyomwambia, Leo kabla hajawika jogoo utanikana mara tatu.

62  Akatoka nje akalia kwa majonzi”

Umeona hapo?.. Bwana alipomtazama Petro, ndipo Petro akakumbuka kuwa Bwana alimwambia na vile vile akafahamu  kuwa sauti ile ya jogoo ilikuwa ni ya kumtahadharisha aache kumkana Bwana, Njia aliyokuwa anaieleka sio salama, maneno aliyokuwa anayatamka ni hatari, mwisho wake ni uharibifu!…

Laiti kama Bwana asingemgeukia Petro, au asingemwambia unabii ule, pengine Petro angeendelea kumkana Bwana hata kwa mara ya nne na tano.. na usalama wa Petro ungeendelea kuwa chini, kwasababu wale watu tayari walikuwa wameshamjua na labda wangemkamata!..na kumdhuru katika hali yake ile ile ya kumkana Bwana, lakini baada ya Bwana kumtazama, akajua kosa lake na akatoka kule behewani..Akatoka nje!, kutubu, hakuendelea kukaa kule ndani!

Ndugu, jambo hilo hilo linaendelea sasa, Ipo sauti ya Mungu inayotuonya katika mambo mengi tunayoyafanya!..Yule mhubiri unayemdharau na kumwona si kitu, ni huyo huyo Mungu anamtumia kuzungumza na wewe, hata mara tatu au nne, tofauti na Yule unayemdhania sana.. Wakati wewe unategemea kwenda kusikia sauti ya Mungu kwa mtu Fulani ambaye umemkuza sana katika kichwa chako, kumbe Mungu hatumii hiyo njia sana.

Mungu alimtumia Punda kumtahadharisha Balaamu, kadhalika alimtumia  jogoo kumtahadharisha Petro, ambaye alikuwa ni mtume wake aliyemchagua yeye, ambaye leo hii ni nguzo katika Imani.. Atashindwaje kututahadharisha wewe na mimi kupitia mjusi au bata?.  Anaweza kufanya hivyo!. Ni kuzidi kuwa wanyenyekevu tu na kuongoza umakini tu!. Na sio tu kututahadharisha, bali pia kuzungumza na sisi.

Unapopita mahali na kusikia mahubiri yanayomtaja Yesu Kristo wa kwenye biblia, usidharau chochote kile!, hata kama wewe una maarifa mengi kuzidi hapo unaposikia,  tega sikio lako kwa makini sana, kwasababu kuna uwezekano Mungu anasema na wewe hapo!, haijalishi Yule anayehubiri ni mdhaifu na wewe ni Mchungaji au mtumishi!.. na wajibu wako kujinyenyekeza kwasababu, Mungu anatumia chochote kuzungumza na  sisi, hivyo hatujui ni kwa njia gani atatumia kusema na sisi, ni kuwa tayari tu muda wote na kwa chochote.

Bwana atusaidie na kutubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Akawaambia Enendeni ulimwenguni mwote,MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE.(Marko16:15.) Yesu Anamaanisha nini kusema MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE?

NI VIZURI SISI KUWAPO HAPA.

TUSIRUHUSU MAMBO YA KUSUBIRISHA, YAVURUGE MUDA WETU NA MUNGU.

kwanini Yakobo amefananishwa na mdudu?(Isa 42:14)

IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Getrude Charles
Getrude Charles
2 years ago

Amen, Mungu awabariki sana jamani, hakika mnatutoa sehem moja na kutupeleka sehem nyingine kiroho.