kwanini Yakobo amefananishwa na mdudu?(Isa 42:14)

kwanini Yakobo amefananishwa na mdudu?(Isa 42:14)

SWALI: Mtumishi wa Bwana napenda kufahamu Neno hili kwenye Isaya 41:14 kwanini Yakobo amefananishwa na mdudu?


JIBU: Tuanzie kusoma juu kidogo mstari wa 8 na kuendelea ili tupate picha nzuri Zaidi..

Isaya 41:8 “Nawe, Israeli, mtumishi wangu; Yakobo, niliyekuchagua; mzao wa Ibrahimu, rafiki yangu;

9 wewe niliyekushika toka miisho ya dunia, na kukuita toka pembe zake, nikikuambia, Wewe u mtumishi wangu; nimekuchagua wala sikukutupa;

10 usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

11 Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia.

12 Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako.

13 Kwa maana mimi, Bwana, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.

14 USIOGOPE, YAKOBO ULIYE MDUDU, NANYI WATU WA ISRAELI; mimi nitakusaidia, asema Bwana, na mkombozi wako ni Mtakatifu wa Israeli.

15 Tazama, nitakufanya kuwa chombo kikali kipya cha kupuria, chenye meno; utaifikicha milima, na kuisaga; nawe utafanya vilima kuwa kama makapi.

16 Utawapepeta, na upepo utawapeperusha; upepo wa kisulisuli utawatawanya; nawe utamfurahia Bwana, utajitukuza katika Mtakatifu wa Israeli”.

Kama tunavyoweza kuona hapo Mungu anawafananisha Israeli watu wake na  wadudu, viumbe wanyonge wasio na uwezo wala nguvu yoyote ya kushindana, au kujitetea, tena mdudu anayezungumziwa hapo ni yule mnyoo, ambaye hawezi kutembea umbali mrefu, ni rahisi kukanyagwa, na kupotea,..

Hiyo ni kuonyesha kuwa watu waliochaguliwa na Mungu ni kama wadudu tu, masalia ya dunia, mabaki, watu wasiokuwa na kitu chochote cha kujivunia, , wasioweza kufanya lolote,

Kumbuka wakati  Mungu anayazungumza hayo maneno  taifa la Israeli wakati huo halikuwa taifa hodari sana kama mataifa mengine duniani, ulinganisha na   Babeli au Misri, au Ashuru, au Tiro, au Sidoni, bali lilikuwa ni taifa la kawaida tu linyonge.

Lakini kwasababu lilimfanya Mungu kuwa tegemeo lao, ndio maana likaonekana kuwa ni tishio ulimwenguni kote,.Na mataifa yakawa yanaliogopa taifa hilo kwa jambo hilo tu moja la Mungu wao Yehova.

Sasa kulingana na vifungu hivyo tunaona Mungu akilifariji dhidi ya maadui zao ambao watakuja kukusanyika  kupigana nao, na ndio hapo utaona akiwaambia japo wao ni kama wadudu tu, lakini atawafanya kuwa kama chombo kikali cha kupuria, chenye meno, ya kuisambaratisha milima mikubwa na kuisagasaga..(Mstari wa 15-16). Na sote tunajua jinsi Mungu alivyokuwa akilipigania taifa hili katika vita vigumu vilivyoshindakana

Na sisi pia, tukimfanya Mungu kuwa tegemeo letu, haijalishi tutakuwa ni dhaifu kiasi gani mbele za watu, tutakuwa ni wadudu wadogo kiasi gani, lakini tutaiangusha milima mikubwa, na mambo mengine yote ambayo hayawezekaniki. Lakini hiyo yote. Ni mpaka tumfanye Mungu kuwa kila kitu kwetu. Kama ilivyokuwa kwa Israeli.

Isaya 41:8 “Nawe, Israeli, mtumishi wangu; Yakobo, niliyekuchagua; mzao wa Ibrahimu, rafiki yangu;”

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Ni kwanini mifugo ya Yakobo iliongezeka kwa wingi kiasi kile?

Mataifa ni nini katika Biblia?

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 7 (Yeremia na Maombolezo)

Nini maana ya msiwe waalimu wengi (Yakobo 1:3)?

SIKU YA TAABU YA YAKOBO.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments