Vichwa saba vya mnyama wa kwenye Ufunuo 13 na 17, Ni nini?

Vichwa saba vya mnyama wa kwenye Ufunuo 13 na 17, Ni nini?

Je! Vichwa saba vya mnyama wa kwenye Ufunuo 13 na 17, Ni nini?


JIBU: Tukisoma kitabu cha Ufunuo ni kweli tunamwona mnyama aliyetajwa mwenye vichwa saba na pembe kumi..Tofauti na idhaniwavyo na wengi kwamba zile pembe kumi zimejigawanya kwenye vichwa vyote 7..na kwamba kuna vichwa vingine labda vitakuwa vimepata pembe mbili mbili au zaidi…Lakini ukweli ni kwamba ni kichwa kimoja tu ndicho kilichokuwa na pembe zote 10..Hivyo vingine havikuwa na pembe yoyote.

Na kama ukitafakari kwa makini kwa msaada wa Roho utagundua kuwa vile vichwa saba ni Wanyama saba katika mwili mmoja na sio tu vichwa kama vichwa vilivyojiotea kwenye mwili mmoja…bali ni Wanyama saba tofauti wanaoshiriki mwili mmoja (yaani wana-share mwili mmoja)..

Ufunuo 17: 11 “Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu”.

Sasa hiyo imekaaje kaaje?..Inawezekana Wanyama Zaidi ya mmoja kushiriki mwili mmoja?..

Hiyo inawezekana asilimia 100..wapo ng’ombe mapacha wanaozaliwa wakiwa na mwili mmoja lakini vichwa viwili tofauti, kadhalika wapo nyoka wanaozaliwa hata watatu au wanne wakiwa na wanashea mwili mmoja…Na Zaidi ya yote wapo pia wanadamu ambao wanaozaliwa wakiwa wameungana…Kuna mapacha wanaoishi leo duniani ambao wameungana kila kitu isipokuwa kichwa tu…yaani ukikutana nao unaweza kusema umekutana na mtu mmoja mwenye vichwa viwili lakini kumbe ni watu wawili waliozaliwa wameungana wanaoshea mwili mmoja..Na watu hao walioungana kila mmoja anatafakari kivyake na ana malengo yake na mipango yake, na matamanio yake.

Na katika tukio hilo la Ufunuo ni vivyo hivyo..Biblia imemtaja mnyama huyo kuwa mwenye vichwa saba..Lakini kiuhalisia ni Wanyama saba tofauti wenye mwili mmoja…Na kila mnyama (yaani kichwa kina mambo yake)…Na pia ni mnyama mmoja tu kati ya hao wote mwenye pembe kumi (yaani ni kichwa kimoja tu chenye pembe hizo kumi).

Sasa hao Wanyama saba au vichwa saba ni nini?

Biblia inasema ni wafalme saba..

Ufunuo 17:9 “Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo

10 Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache. ”.

Falme hizo kama zinavyojidhihirisha katika taifa la Mungu kwenye biblia ni MISRI, ASHURU, BABELI, UMEDI & UAJEMI, UYUNANI, RUMI YA KIPAGANI na RUMI YA KIDINI..Hizi ndizo falme hizo saba au Wanyama hao 7..Falme hizi ni Mataifa aliyotumia shetani kuutesa uzao wa Mungu kwa ujumla wake…

Mataifa Matano ya kwanza yaliwatesa wana wa Israeli peke yao, wakiwa Misri, na mengine baada ya kuchukuliwa tena mateka babeli..lakini haya mawili ya mwisho yaliwatesa wana wa Israeli pamoja na Kanisa la Kristo…Na hicho kichwa ndicho cha mwisho na ndiye mnyama wa 7 ambaye ni RUMI YA KIDINI,.. nacho ndicho chenye pembe zote saba.. mnyama huyu ndiye ambaye yupo sasa na anazidi kuongezeka nguvu siku baada ya siku,.atakapofikia kilele chake atazitumia pembe zake 10 ambayo ni mataifa yanayounda umoja wa ulaya (EU) kuhimiza ile chapa ya mnyama. Kwasasaba umoja huo una wanachama Zaidi ya 10..

Lakini unabii unaonyesha yatakuja kubakia 10 tu yenye nguvu kwenye umoja huo. Na Kwa pamoja yatashirikiana na mnyama huyo, (Rumi ya kidini Iliyopo chini ya kiongozi wa kanisa katoliki ,Papa) kuishawishi dunia kuendesha zoezi la kuwatia watu chapa. Kwa kipindi kifupi sana kisichozidi miaka mitatu na nusu, Chapa itakuwa imeshawafikia watu wote duniani…Watakaoikataa watakamatwa na kupelekwa kwenye kambi maalumu za mateso…

Wakati huo unyakuo utakuwa umeshapita…Watakatifu wameondolewa duniani,.kuepushwa na ghadhabu ya Mungu na majaribu ya mpinga-kristo.

Ukali wa dhiki kuu.

Na huko katika magereza hayo ya mateso, watu watakitafuta kifo hawatakiona kama unabii unavyosema.. “kwasababu mtu anayekutesa siku zote hataki ufe haraka..lengo lake uteseke kwa muda mrefu”..Ndicho kitakachotokea siku hiyo..watu watateswa lakini hawatauawa kwa haraka (Yatakuwa ni mara 100 zaidi ya yale ya Hitler, ambayo alikuwa anawapiga watu kwa nyundo yenye uzani mdogo kichwani mara nyingi aangalie ni kwa kiwango gani watu wanasikia maumivu, na kiwango cha watu kustahimili vifo wanapouliwa taratibu..mtu huyo anapigwa nyundo hata saa 4 mpaka anazirai, na mwisho wa siku kufa..

Au wanamfanyia mtu operation bila ganzi huku anatazamwa uwezo wake wa kumudu maumivu, au wanawatia watu kwenye barafu kali wakiwa uchi kwa masaa kadhaa kila siku)…ndivyo atakavyofanya mpinga-kristo na ziadi wakati huo wa dhiki kuu, na mateso hayo yatadumu kwa muda mrefu sana kwenye kambi hizo..kwa miaka sio chini ya mitatu na nusu..baadaye ndipo watawaua..wakati wengine waliosalia huko nje wakiendelea kufurahia Maisha baada ya kuipokea chapa…Hivyo dhiki kuu haitawahusu watu wote, bali tu wale watakaoikataa chapa…

Dhiki ya mataifa.

Baada ya wale waliokataa chapa kufa wote…Itakuwa ni zamu ya wale walioikubali chapa kupitia dhiki na wao…Dhiki hiyo ni ghadhabu ya Mungu mwenyewe atakayoimwaga juu ya wale wote walioipokea chapa…Ghafla tu wakati wanaona dunia ni tamu mambo yataanza kubadilika…Bahari itakuwa damu, mito na chemchemu zote zikuwa damu, majipu na magonjwa ya ajabu yataanza kuwatokea, roho za mapepo wabaya zitaachiwa juu ya wanadamu, kutokuelewana kutaanza kutokea,vita vya wenyewe kwa wenyewe vitazuka, mvua ya mawe makubwa kama talanta zitaanza kushuka juu ya wanadamu,.. jua litashushwa chini kuwaunguza wanadamu kwa kipindi kirefu..na mwisho jua na mwezi na nyota vitatiwa giza, tetemeko kubwa duniani litatokea, kila visiwa kitapotea na kuzama kwenye bahari ya damu, na milima itafumuka..

Wanadamu wote walioipokea chapa watakufa kifo kibaya kuliko hata cha wale walioikataa chapa..na baada ya kifo hicho wote wataelekea jehanamu ya moto..Na kabla hawajamalizika wote kufa, wale wa mwisho mwisho kufa wachache sana ambao ni washirika wa vita vya Harmagedono ndani ya giza hilo kuu watamwona Kristo akija katika mawingu wataomboleza sana , lakini biblia inasema wataangamizwa kwa upanga utokao katika kinywa chake..

Biblia inasema

Mathayo 24:29 “Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;

30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi”

Je! Unatamani kuwepo kwenye dhiki kuu?.. mimi sitamani..Natumai hata na wewe pia hutamani, Lakini unafahamu kuwa huo wakati upo karibu sana yamkini mambo hayo yatatokea katika kizazi chetu? Je! umempa Kristo Maisha yako?..Una uhakika wa kwenda kwenye unyakuo?…au bado upo kwenye ulimwengu?..kama bado ni mwasherati endapo parapanda italia leo utabaki hapa kukutana na hayo yote tuliyoyasoma hapo juu..

Kama hujaokoka na unataka kuokoka, fanya hivyo sasahivi.. Hapo ulipo tubu..na mwambie Bwana unataka kufanyika kuwa kiumbe kipya..baada ya kutubu tafuta kanisa ushiriki na wengine wenye Imani moja na wewe.. Na baada ya hapo pia hakikisha unabatizwa katika ubatizo sahihi kama hujabatizwa…Ubatizo sahihi ni wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo..Na Roho Mtakatifu atakusaidia kufanya yaliyosalia katika Maisha yako, na kukuweka katika mstari wa wale watakaonyakuliwa na kuepushwa na hukumu ya Mungu ya milele.

Bwana akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

UFUNUO: Mlango wa 13

UFUNUO: Mlango wa 17

UFUNUO: Mlango wa 16.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Kati ya Unyakuo,dhiki kuu, utawala wa miaka 1000 kipi kinaanza

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Ezekiel Lumwecha Tabanya

Nashukuru Mungu kujiunga na chaneli pendwa ya kufahamu namna maandiko yatupasayo kupewa wokovu na si kuamini tu.Amina ahsanteni Mungu atubariki..
By Ezekiel sevant of God

Pierre Mugisha
Pierre Mugisha
2 years ago

Asante kwa ujumbe kwa maafunuo