WAMNGOJEAO BWANA WATAPATA NGUVU MPYA.

WAMNGOJEAO BWANA WATAPATA NGUVU MPYA.

Wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya.


Ipo ahadi kubwa sana ambayo Mungu kaitoa kwa wale walioamua kuiacha dunia na kumfuata yeye kwa gharama zote. Na ahadi yenyewe ni “kupokea nguvu mpya kipindi baada ya kipindi”. Mungu anafahamu kabisa safari ya wokovu ni ngumu kama ilivyosafari nyingine yeyote ya haya maisha…kuna milima na mabonde, kuna kuchukiwa na kudharauliwa, kuna kuonekana umerukwa na akili na kutokuthaminiwa, kuna kutengwa na kuudhiwa, kuna kupungukiwa na kuvunjwa moyo, kuna msiba na dhiki n.k. vyote hivyo mtu yeyote aliyeamua kumfuata Kristo, kwa namna moja au nyingine atakumbana navyo…

Lakini utajiuliza pamoja na hali kama hizo ni kwanini bado watu waliookoka wengi ki-kweli kweli wanaweza kustahimili?..Ni rahisi mtu kwa kidunia kuvunjika moyo au kukatishwa tamaa na mambo kama hayo lakini kwa mkristo aliyedhamiria kumfuata Yesu, ndio kwanza anazidi kuwa karibu na Mungu wake..Hiyo yote ni kwasababu ipo nguvu inayoachiliwa ndani yake kipindi baada ya kipindi..

Biblia inasema..

Isaya 40:28 “Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.

29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.

30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka;

31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia”.

Kama sio neema hiyo, hakuna hata mmoja wetu angeweza kumwamini na kumtuamini Mungu asiyemwona sikuzote za maisha yake..Lakini kwasababu ipo nguvu anayoiachia ndani ya wale wanaomngojea wanajikuta tu wanazidi kumtafuta Mungu, safari yao ya wokovu wanaiona kama vile imeanza jana..

Hiyo ndio tofauti na mtu aliyeokoka na yule ambaye hajaokoka..Yule ambaye hajaokoka, anaweza akawa anajisumbua katika jambo Fulani, au katika shughuli yake,.. au katika elimu yake, lakini upo wakati atachoka, ataboreka, atazimia na kusema ngoja nipumzike kwanza, nitakuja kuendelea baadaye, lakini kwa mtu aliyejitwika msalaba wake na kumfuata Kristo, pale ambapo ataonekana anakaribia kuzimia hapo ndipo Mungu anapompa nguvu mpya, anapompa uwezo mpya.

Hufanya njia pale pasipo na Njia:

Pale ambapo watu watasema sasa huyu ndio basi, kwa hali hii, anayoipitia hamalizi huu mwaka atakuwa amesharudi tu huku kwenye dunia, lakini wanashangaa mwaka unapita, miaka inapita,.. ndio kwanza anazidi kumpenda na kumtafuta Mungu wake Zaidi ya hapo mwanzo..Kwasababu gani, Ni kwasababu Mungu anahakikisha anawapa nguvu mpya wale wao waliodhamiria kujitwika msalaba wao na kumfuata..kama maandiko yanavyosema:

watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.

Ukristo ni safari ya kuwezeshwa, ukiona mtu anasema nimeishiwa pumzi njiani siwezi kuendelea mbele nimezidiwa na tamaa za ulimwengu, fahamu kuwa mtu huyo tangu mwanzo alikuwa bado hajadhamiria kumfuata Kristo kwa moyo wake wote.. Kwasababu ni kitu ambacho hakiwezekani kuishiwa pumzi katikati angali kila wakati unawezeshwa, unapokea nguvu mpya, sasa huko kuishiwa pumzi kunatoka wapi?.

Leo hii unaweza ukajiuliza hivi kweli nikiokoka, nitaweza kuishi bila uzinzi kwa muda mrefu?, nitaweza kuacha kunywa pombe kwa kipindi kirefu,.. nitaweza kuvumilia kutovuta sigara kwa miaka 2 kweli, nikiamua kumfuata Kristo nitaweza kujizuia kutokuweka make-up maisha yangu yote, na kutokuvaa suruali,.. nitaweza kutokwenda Disko, nitaweza kutokufanya Musturbation…Nataka nikuambie kwa akili zako na nguvu zako chache hutaweza, lakini ukiamua kwa kudhamiria kweli kumfuata Kristo kwa moyo wako wote, ukasema leo hii naanza upya kupiga mwendo na Kristo, hilo jambo ni rahisi sana kulishinda kuliko unavyodhani..

Utapokea nguvu mpya:

Kabla hata hujakaribia kuishiwa pumzi Bwana atakuwa pembeni yako kukutia nguvu mpya..Kila siku itakuwa fresh kwako, wiki itapita, mwezi utapita, mwaka utapita, miaka itapita na bado ile hamu ya kufanya hayo mambo haipo ndani yako, ..Hiyo ni neema kubwa Mungu aliyowahaidia wale wote watakaomngojea…Hapo ndipo tunapouna wepesi wa wokovu, vinginevyo hakuna ambaye angeweza kuushinda huu ulimwengu, si mchungaji, si mwinjilisti..hakuna atakayeweza kuushinda ulimwengu.

Hata kama utapitia hali ambayo unaona kesho au kesho kutwa haifiki, lakini maadamu upo kwa Bwana, na unamtazama yeye, utaona tu jinsi atakavyokufanyia njia mahali ambapo hapana njia na wewe mwenyewe utajikuta unamwimbia, EBENEZA MWAMBA WANGU!..

Hata katika magonjwa, au dhiki, katikati yake atakufungulia mifereji ya faraja na uponyaji, nawe utasema ni heri Mungu nilichagua kukufuata maana ninauona mkono wako ukinizunguka!..Hali hiyo hiyo utaendelea nayo mpaka utakapomaliza mwendo wako hapa duniani kama unyakuo hautakukuta..hata Katika raha atakuwa na wewe pia kukuongezea raha Zaidi..

Je na kwa mwenye dhambi ni hivyo hivyo?

Lakini ikiwa upo mbali naye, na unasema kuishi maisha ya wokovu haiwezekani hapa duniani..Nataka nikuambie utajikuta unaendelea kusema hivyo mpaka unakufa na dhambi zako,..

Bwana Yesu aliwaambia mafarisayo katika Yohana 8:24 ‘Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu’.

Kuna madhara makubwa sana kufa katika dhambi…Ukifika kule mbele ya kiti cha hukumu wataletwa watu wa kizazi chako walioweza kukishinda hicho kinachokushinda wewe leo hii,..Nao wataulizwa ilikuaje kuaje nyie mliweza kuushinda uzinzi katika dunia iliyojaa vishawishi namna ile? na wakati hawa wengine wameshindwa?..Nao watajibu kwa ku-unukuu mstari huo;

Isaya 40:29-31

 ‘29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.

30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka;

31 bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia”.

Hapo utakosa cha kujibu, ukijua kuwa kumbe na wewe ulikuwa na fursa kama hiyo lakini uliikataa.

Hivyo usisibiri upendeleo wa kipekee kama huo ukupite, acha kufikiria fikiria kwa juhudi zako utawezaje. Leo hii dhamiria kutubu dhambi zako zote, hapo ulipo tenga muda mchache ukiwa peke yako piga magoti, anza kumweleza Mungu mambo yako maovu yote uliyomtendea,… kisha mwambie Naomba msamaha,..Fanya hivyo kwa kumaanisha kabisa kutoka moyoni mwako kwasababu yupo hapo kukusikia, na yupo hapo kukusamehe dhambi zako zote..

Na Ile damu yake Yesu Kristo itakusafisha kabisa, na uthibitisho wake ni kuwa, baada ya Toba Amani ya ajabu na utulivu wa kipekee utaingia ndani yako, ukishaona hivyo, dhamiria sasa kuacha kufanya yale yote uliyokuwa unafanya nyuma yasiyompendeza Mungu, kwasababu Mungu kashakukaribia….kama ulikuwa ni mlevi kaa mbali na walevi na pombe, ulikuwa ni mzinzi kaa mbali na wazinzi na acha uzinzi, Na Mungu akishaona mwitikio wako, na kwamba umegeuka kivitendo sawasawa na toba yako, Sasa ile nguvu yake ya kukufanya uzidi kupiga mbio upae juu Zaidi kwa mbawa za tai, itaanza kuachiliwa ndani yako..Na kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo utakavyojiona tamaa ya vile vitu ulivyokuwa unavifanya vinakufa ndani yako, na mwisho wa siku vitapotea kabisa..

Hatua inayofuata baada ya toba:

Hivyo ukishatubu bila kupoteza muda hakikisha unatafuta kanisa, ukabatizwe, katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi (Yohana 3:23) na kwa jina la YESU KRISTO sawasawa na Matendo 2:38 ili kuukamilisha wokovu wako.

Kumbuka ubatizo sahihi ni muhimu sana..Vilevile anza kujumuika na wakristo wenzako, wale unaoona wamesimama kweli kweli na anza kusoma Neno kwa bidii na kusali..Yaliyosalia Roho Mtakatifu atakuongoza kuyatenda..

Shalom.

Mada Nyinginezo:

MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.

MNGOJEE BWANA

INGIENI KWA KUPITIA MLANGO ULIO MWEMBAMBA.

HERI NINYI MLIAO SASA, KWA SABABU MTACHEKA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments