Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?

Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?

JIBU:Neno la Mungu linasema Mungu ni Roho nao wamwabuduo imewapasa wamwabudu katika roho na kweli. Wakristo hawahesabiwi haki mbele za Mungu katika siku, miezi au miaka ya kuabudia, aidha uabudu jumapili, jumatatu, jumamosi au jumatano huo ni utaratibu wa mtu tu! haimuongezei mtu chochote katika uhusiano wake na Mungu. Biblia inasema..  

Wagalatia 4:9 “Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? Mnashika SIKU, NA MIEZI, NA NYAKATI NA MIAKA.”

 Na Pia inasema tena katika

Wakolosai 2:16 “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.”  

Hivyo Maana ya NENO sabato ni “Pumziko”, na pumziko kwa wakristo lipo rohoni, na mwokozi wetu Yesu yeye alituambia kuwa ndiye BWANA wa sabato (soma Mathayo 12:8), hivyo tukimpata YESU tumeipata SABATO au “pumziko letu la rohoni” na ndio maana anasema..  

Mathayo 11:28 “ Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami NITAWAPUMZISHA. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; 30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

Kwahiyo wanaoabudu jumamosi, au jumapili au jumatano hawafanyi makosa, ni utaratibu wao tu, mbele za Mungu wote wapo sawa, kwa mfano tunasoma katika biblia wakristo wakwanza waliiteua siku ya kwanza ya juma ( yaani JUMAPILI) kwa ajili ya kukusanyika na kufanya changizo pamoja na kumega mkate,ukisoma Matendo 20:7 na 1Wakoritho 16:1-2 utaona jambo hilo, hivyo kuteua siku fulani na kusema hiyo ndio Mungu anairidhia kuabudia zaidi ya siku nyingine, ni kutokuyaelewa maandiko.   kwasababu ibada halisi ipo rohoni na Mungu anaabudiwa katika roho na kweli, na sio katika siku maalumu au miezi maalumu au miaka maalumu bali ni kila saa na kila wakati mahali popote.  

Ubarikiwe sana.

Group la whatsapp

jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada zinazoendana:

BABA YANGU ANATENDA KAZI HATA SASA!.

MAMBO (2) YATAKAYOKUTENGA NA IMANI SIKU HIZI ZA MWISHO.

EPUKA MUHURI WA SHETANI


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

17 comments so far

braitonyPosted on7:45 um - Januari 3, 2023

Leave your message swal lingine je wanyama wote wametakaswa?

braitonyPosted on7:37 um - Januari 3, 2023

Leave your message mbarikiwe nimejifunza makumbwa sana

Zacharia kiprutoPosted on9:17 mu - Novemba 17, 2022

Watu wa mungu wamepotoshwa na mafundisho potovu.,hosea 4:6 na watu wanaojifanya at wanaojifisha mgozi ya kondoo kumbe ni mbwa mwitu.

UnknownPosted on12:02 um - Julai 8, 2022

Barikiwa kwa somo mtumishi ila soma mafungu haya halafu tafakari kwa Maombi na uruhusu Mungu akuongoze. Mwanzo 2:1-3, Kutoka31:15-17, Kutoka 20:8-11, Mathayo5:17, Luka 4:16, Luka 23:44-56, Matendo 17:2-3, Waebr 4:4-11 Isaya 66:22-23 Hivyo ipo siku ya ibada maalumu kwa Mwenyezi Mungu Mwanzo 2:1-3 inathibutishwa na Luka 23:50-56. Barikiwa sana

Frank NtimiaPosted on5:27 um - Juni 30, 2022

Naitaji masomo zaidi ya kujifunza natafuta kujua ukweli

Joshua georgePosted on2:39 um - Mei 17, 2022

Mungu awatangulie

AsiyejulikanaPosted on2:30 mu - Aprili 15, 2022

Shukran mtumishi kwa somo hili nimejifunza..Ubarikiwe

Paul jackobPosted on10:48 um - Aprili 4, 2022

Barikiwa mpendwa kwa SoMo hilo

Edson RukaigaPosted on5:30 um - Mechi 20, 2022

Asante, nimejifunza!! Ila nilitaka kujiunga na kundi lenu la WhatsApp nikaambiwa limeshajaa.

Jackline jonasPosted on11:45 um - Desemba 6, 2020

Umenfungua pakubwaaa mungu awabarki abariki kazi ya mikono yenu

Leave a Reply