Mungu alikuwa anaongea na nani aliposema na “Tumfanye mtu kwa mfano wetu”,(Mwanzo 1:26)?

Mungu alikuwa anaongea na nani aliposema na “Tumfanye mtu kwa mfano wetu”,(Mwanzo 1:26)?

Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi

JIBU: Mara nyingi Mungu alikuwa anatumia neno “sisi” kama wingi kuashiria kuwa hakufanya mambo yote peke yake, bali alikuwa na wengine aliowashirikisha mawazo yake, Kumbuka kuumba aliumba yeye peke yake lakini mawazo yake ya kufanya baadhi ya mambo aliwashirikisha wengine, hivyo hapo aliposema na tumfanye mtu kwa mfano wetu alikuwa anaongea na malaika zake, na hakuwa anazungumza na nafsi ya tatu katika uungu wake,kama wengi tunavyodhani Mungu ni mmoja tu na hana nafsi tatu, neno “TUMFANYE” halimaanishi ni watatu tu! bali linaweza likamaanisha wawili, au watano, au mia au milioni n.k.

Hivyo tukisema Mungu ana nafsi tatu kwa kuusimamia mstari huu sio kweli, pale Bwana alikuwa anazungumza na malaika zake ambao walikuwa wameshaumbwa kabla yetu sisi, Tunaona pia jambo hili linajirudia sehemu nyingine nyingi katika biblia Bwana akizungumza na malaika zake, Ukisoma

Mwanzo 3:22″Bwana Mungu akasema basi huyu mtu amekuwa kama MMOJA WETU, kwa kujua mema na mabaya”…,

pia,

Mwanzo 11:6 “Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. 7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. 8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.”

Unaona hapo sehemu zote hizi mbili Bwana alionekana akijadiliana na malaika zake. Mungu huwa anatenda kazi na malaika zake. Tukisoma pia

Isaya 6:8 Kisha nikasikia sauti ya Bwana ikisema, nimtume nani? naye ni nani atakayekwenda KWA AJILI YETU? Ndipo niliposema mimi hapa nitume mimi. Naye akaniambia enenda ukawaambie watu hawa fulizeni kusikia lakini msifahamu; fulizeni kutazama lakini msione…”

Unaona tena hapo Bwana alimuuliza nabii Isaya ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu (yaani Mungu na jeshi lake la mbinguni)?. Kwahiyo Mungu kujadiliana na malaika zake sio jambo jipya tunaweza tukaliona pia kwenye ile habari ya mfalme Ahabu na nabii Mikaya ukisoma

2 nyakati 18:15-22” utaona jinsi Bwana alivyokuwa anashauriana na malaika zake juu ya hatma ya mfalme Ahabu.

Kwahiyo pale katika mwanzo 1:26 aliposema Na tumfanye mtu kwa mfano wetu Mungu alikuwa hazungumzi na YESU wala Roho Mtakatifu bali na malaika zake waliokuwepo kabla yetu sisi. (Lakini kumbuka sio kwamba malaika ndio waliokuwa wanaumba, hapana Mungu peke yake ndiye aliyekuwa muumbaji.)

Ubarikiwe sana.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.

UZAO WA NYOKA.

JINSI EDENI ILIVYOKUWA.

 


Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Yohan muss
Yohan muss
1 year ago

Kama Mungu alikuwa akifanya kazi kwa kuwashilikisha malaika je! Walimwona vp Mungu na wakati hakuna aliye mwona Mungu isipokuwa Mwana?

Abdallah
Abdallah
2 months ago
Reply to  Yohan muss

1) Muombe mungu akusaidie
2) Tenga muda kwa ajili ya Kusoma ili uimarishe uwezo wako wa kufikiri
3) Jifunze lugha lugha ya Kiswahili

Anonymous
Anonymous
3 years ago

Wakati wa uumbaji malaika hawakuhusika, Baba, mwana na roho

Abdallah
Abdallah
2 months ago
Reply to  Anonymous

Shida nyingine hii Pia..
Kwa imani yetu ya Kiislamu, Mungu pekee ndie aliekuwepo, aliepo na atakaekuwepo. Na hatuna Mungu aliegawika vipande, ametakasika na Kila Sifa ya Udhaifu, nae ni Mwenye Nguvu na hekima..

John johnson
John johnson
3 years ago

Hapana ndugu unahitaji mafundisho zaidi ili kuujua uwepo halisi wa Mungu na utendaji kazi wake.na yakupasa ufunuliwe pia na roho mtakatifu.

Abdallah
Abdallah
2 months ago
Reply to  John johnson

Ni Shida ya Kutokuwa Tayari kuupokea ukweli.. Mimi ni Muislamu, maelezo ya muandishi yamenyooka vizuri ..
Kama tumekwenda Shule japo kidogo tutajua kuwa, Mfano katika Lugha ya Kiingereza kuna PLURAL OF NUMBER & PLURAL OF RESPECT.. (Kuna aina 2 za wingi) .. Wingi wa Idadi na Wingi wa Heshima .. Aweza mtu kuzungumza kwa Plural Form na akajikusudia mwenyewe.. .. Na hivi ndivyo Mayahudi, Waarabu pia wanavyozungumza..