Ili kulielewa hili vizuri tunaweza kujifunza katika mambo yanayotuzunguka ya kila siku. Siku hizi kuna kilimo kijulikanacho kama “ kilimo cha Banda-kitalu” kwa lugha ya kigheni iliyozoeleka na wengi kinaitwa GREEN HOUSE farming. Kilimo hichi hakina tofuati na kile kingine isipokuwa tu, hichi mmea au mboga, au matunda, au maua huwa yanawekwa katika banda maalamu lililozibwa pande zote katika uzalishaji wake. Na wanafanya hivyo sio kwasababu wamependa tu iwe hivyo hapana, lakini kama wewe ni mkulima mzuri utajua kuwa kulima mazao yako katika green-house, kuna faida kubwa kuliko kulima huria, sababu kubwa kwanza ni kinazuia wadudu waharibifu wa mazao kuvamia shamba, pili kinazuia mionzi mikali ya jua kuharibu mimea, hivyo inasaidia kuhifadhi unyevunyevu na kutokutumia gharama nyingi za kupiga madawa, kwa ajili ya wadudu. Na matokeo yake ile mimea huwa inakuwa vizuri, yenye afya, na mwisho wa siku kuleta mazao mengi kuliko hata Yule ambaye yalilimwa mabondeni tu. Huyu anaweza akajiona analoshamba kubwa, lakini mimea ikiaanza kumea tu wadudu waharibifu wanakuja, na hivyo atajikuta anahangaika kupiga madawa, mimea inaliwa na kukosa mvuto na hata akifanikiwa kupeleka sokoni bidhaa yake hainunuliwi kwasababu inakuwa haina ubora unaostahili. Maua mengi ya thamani kama Maua Rose, yanalimwa ndani ya Green house, nje na hapo matokeo yatakuwa hafifu, na ndio maana unaona ubora wake na thamani yake ni kubwa.![]()
Sasa chukua mfano huo huo urudishe pale Edeni, Mungu alimweka Adamu katika GREEN-HOUSE yake, ambayo ndio ile bustani, akamwekea wigo mkubwa wa utukufu wake, na ndio maana chakula na kila kitu kilikuwa kinajiotea tu chenyewe katika ubora wote ndani ya bustani ile, hiyo yote ni kwasababu hakukuwa na viumbe viharibifu vilivyoingia na kugeuza mambo. Lakini sasa baada ya wao kumpa nafasi NYOKA, nyoka akawadanganya walitoboe HEMA lao, na walipofanya vile tu, basi lile hema lote likapasuka, kukawa hakuna ulinzi tena wowote wa bustanini, wanyama hawaribifu wakaanza kuingia. Ndio tunaona pale Mungu anaanza sasa kuwaeleza matokeo yatakayofuatana nao kwa kosa walilolitenda..Adamu atakula kwa jasho, nchi itamzalia michongoma, na mwisho wa siku atakufa tu.