Mitume wote waliopita walikuwa ni watu weupe hata manabii wote waliopita hadi Ma-papa ni ngozi nyeupe. ni kweli ngozi nyeusi ililaaniwa ?

Mitume wote waliopita walikuwa ni watu weupe hata manabii wote waliopita hadi Ma-papa ni ngozi nyeupe. ni kweli ngozi nyeusi ililaaniwa ?

JIBU: Hakuna ngozi yoyote iliyolaaniwa, watu wote kwa Mungu ni sawa, Mungu hana upendeleo kwa jamii fulani ya watu, Pia ni muhimu kufahamu utendaji kazi wa Mungu katikati ya wanadamu tangu kuumbwa kwao, Mungu alimchagua Ibrahimu na kumbariki yeye na uzao wake, kuanzia hapo Bwana Mungu aliliteua taifa moja pekee ambalo atashughulika nalo katika mpango wake wa wokovu kwa wanadamu (yaani taifa la Israeli), hilo pekee ndilo liliokuwa taifa la Mungu katikati ya mataifa yote ulimwenguni katika agano la kale.

Hivyo Wayahudi(au Waisraeli) kwa asili hawakuwa wazungu au watu wazuri nikiwa na maana kuwa “weupe sana” kuliko watu wa mataifa mengine duniani, walikuwa ni watu wa kawaida sana, na hata ngozi zao hazikuwa nyeupe kama za watu wa mataifa mengine mfano wa Ugiriki, Rumi, ambayo yalikuwa kando kando ya Israeli n.k  ni jamii iliyokuwa inakaribia kufanana na Waarabu, na kama unavyojua Waarabu sio weupe kama wazungu au Wachina, hivyo Hao (waisraeli) ndio Mungu aliowateua sio kwa mwonekano wao bali kwa kusudi lake Mungu, ili baadaye aje kutimiza mpango wake wa wokovu alioukusudia kuja kuuleta kwa kupitia Bwana wetu Yesu Kristo kwa watu wa ulimwengu mzima na ndio maana utaona kuanzia mwanzo wa biblia hata mwisho huwezi kuona ngozi nyeusi au nyeupe ikitajwa, na sio tu ngozi nyeusi hutaweza pia kuona mzungu, au mchina yoyote, au mhindi yoyote akitajwa kama nabii halisi wa Bwana, kwasababu kwa wakati huo Mungu alikuwa anatenda kazi na wayahudi (waisraeli) tu. na sio na watu wa ulimwengu mzima,  

Lakini ulipofika wakati wa neema ya Bwana wetu Yesu Kristo kudhihirishwa ulimwenguni kote, watu wote mbele za Mungu tumekuwa sawa hakuna tena cha myahudi, au mtu wa mataifa au mweusi, au mwarabu, au mchina n.k Bwana Yesu Mungu wetu alikiondoa kile kiambaza cha kati kilichotutenga sisi na jamii ya waisraeli, na kutufanya mbele za Mungu kuwa wamoja, na ndio maana leo utaona kuna manabii, waalimu, wakizungu, wa ki-wakiafrika, wa-kichina, wa-kihindi, jambo ambalo hapo kwanza halikuwepo. Ilikuwa ni kwa wayahudi tu, na sio kwasababu eti wao ni weupe, hapana wakati huo wazungu walikuwepo wengi sana, wachina walikuwepo nao pia lakini hawakuruhusiwa hata mmoja kumkaribia Mungu wa Israeli katika shughuli zozote zinazohusiana na ibada..  

Waefeso 2:11 “Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono;

12 kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.

13 Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo.

14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga.

15 Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani.

16 Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba”.  

Na Pia papa hatuwezi kumweka katika kundi la Mitume au Manabii, kwasababu mfumo wa anachokiamini ni kinyume na mfumo wa maandiko unavyoagiza..  

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

UZAO WA NYOKA.

JIRANI YAKO NI NANI?

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

UNYAKUO.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

1 comment so far

Elizabeth kasichiPosted on7:33 pm - Mar 16, 2022

Je kwa nini watu wanaozaliwa sehemu za baridi ambao wazazi wao ni waafrica bado wanaendelea kuwa na ngozi nyeusi?

Leave a Reply