Ahera ni wapi? Kama tunavyosoma katika biblia.

Ahera ni wapi? Kama tunavyosoma katika biblia.

Neno Ahera limeonekana mara tatu tu katika biblia, limeonekana katika kitabu cha 1Wafalme 2:6 na 9  na katika kitabu cha Wimbo ulio bora 8:6, mara zote hizi Neno hilo limetumika likimaanisha “kaburi”. Hivyo Ahera maana yake ni kaburi.

1Wafalme 2:5 “Na zaidi ya hayo, umejua alivyonitenda Yoabu, mwana wa Seruya, yaani, alivyowatenda majemadari wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri, mwana wa Neri, na Amasa, mwana wa Yetheri, ambao aliwaua, na kuimwaga damu ya vita wakati wa amani, akautia damu ya vita mshipi uliokuwa viunoni mwake, na viatu vilivyokuwa miguuni mwake.

 6 Kwa hiyo ufanye kama ilivyo hekima yako, wala usimwachie mvi zake kushukia AHERA KWA AMANI”.

Ahera inatukumbusha kuwa kuna mwisho wa maisha haya… hivyo hatuna budi kutengeneza maisha yetu, kabla hatujaingia kaburini… Kwasababu baada ya kifo kitakachokuwa kimebakia kwetu ni hukumu..

Waebrania 9:27  “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu”.

Bwana atujalie tuishi maisha yanayompendeza yeye, angali bado tunaishi.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Maana Ya Maneno Katika Biblia.

Mahali pa juu palikuwa ni wapi kama tunavyosoma katika biblia?

Tofauti kati ya uchafu wa mwilini na rohoni ni  ipi?

NYAKATI HIZI NI ZA MWISHO, HII DUNIA INAKWENDA KUISHA.

MUNGU ATAKUUA UKIWA MBAYA MACHONI PAKE.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments