Gumegume ni nini? (Isaya 50:7)

Gumegume ni nini? (Isaya 50:7)

Gumegume ni jamii ya miamba ambayo ni migumu sana, inapatikana huko maeneo ya mashariki ya kati sana sana  nchi ya Palestina. Zamani ilitumika katika kutengeneza vifaa, kama nyundo, mashoka, visu, majembe, ncha za mikuki na michale n.k. hiyo yote ni kwasababu ya sifa ya ugumu wake.

Neno hili limetumika sehemu kadha wa kadha katika biblia kama tunavyoweza kulisoma katika vifungu hivi;

Yoshua 5:2 “Wakati huo Bwana akamwambia Yoshua, Haya, jifanyie visu vya mawe ya gumegume, watahiri tena wana wa Israeli mara ya pili.

Ayubu 28:9 “Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake; Huipindua milima hata misingi yake”.

Isaya 5:28 “Mishale yao ni mikali, na pindi zao zote zimepindika; Kwato za farasi zao zitahesabika kama gumegume; Na gurudumu zao kama kisulisuli”;

Ezekieli 3:9 “Kama almasi ilivyo ngumu kuliko gumegume, ndivyo nilivyokifanya kipaji chako; usiwaogope, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba ya kuasi”.

Kumbukumbu 32:13 “Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka, Naye akala mazao ya mashamba; Akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini, Na mafuta yaliyotoka katika mwamba wa gumegume;”

Lakini je Neno hili/ Mwamba huu unafunua nini rohoni?

Mungu anataka na sisi tuwe na mioyo ya gumegume kwake,(yaani mioyo migumu isiyokengeuka haraka), Kama ilivyokuwa kwa mwanawe mpendwa Yesu Kristo, ambaye tunamsoma unabii wake katika Isaya 50:7, akielezewa jinsi  moyo wake ulivyokuwa mgumu kwa Bwana kama gumegume, licha ya kuwa alipitia mateso makali namna ile.

Isaya 50:5 “Bwana MUNGU amenizibua sikio langu, wala sikuwa mkaidi, wala sikurudi nyuma.

6 Naliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang’oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate

7 Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, KWA SABABU HIYO NIMEKAZA USO WANGU KAMA GUMEGUME, nami najua ya kuwa sitaona haya.

Umeona, Bwana Yesu, japokuwa alipitia mateso makali, lakini bado moyo wake haukugeuka nyuma. Nasi pia ndivyo Mungu anavyotaka atuone.

Mtume Paulo pia alikuwa ni mtu wa namna hii, mpaka akadhubutu kusema hakuna jambo lolote linaloweza kumtenga yeye na upendo wa Kristo.

Warumi 8:38 “Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,

39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Swali la kujiuliza, je! Na sisi, mioyo yetu ni ya gumegume kwa Bwana? Au ya Udongo?

Je! Dhiki na mateso vitakapotujia, bado tutaweza kung’ang’ana na Bwana?

Bwana atusaidie, tuwe watu na namna hii.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Group la whatsapp Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Shinikizo ni nini?

Donda-Ndugu ni nini?

MAOMBOLEZO YA HADADRIMONI.

Tofauti kati ya kukana na kusaliti ni ipi?

Matulizo ya mapenzi ni nini? (Wafilipi 2:1).

Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “Saa yangu haijawadia?”

Kwanini Bwana Yesu alivikwa taji ya miiba?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Getrude Charles
Getrude Charles
2 years ago

Amen, Bwana yesu atutie nguvu sana.