Donda-Ndugu ni nini?

Donda-Ndugu ni nini?

Tusome,

2Timotheo 2:16 “Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu,

17 na neno lao litaenea kama DONDA-NDUGU. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,

18 walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha”.

Donda-ndugu ni kidonda kinachotokana na damu kuacha kupita katika kiungo kimojawapo cha mwili, husuani katika vidole au katika viungo vya ndani ya mwili kama Maini, na hivyo kusababisha kusababisha kiungo hicho kitengeneza kidonda kisichopona..

Na kiungo hicho kisipoondolewa basi kidonda hicho kinasambaa mwili mzima, na kusababisha matatizo mengine makubwa zaidi.  Ugonjwa wa donda-ndugu hauna tofauti na ugonjwa wa Kansa. Na suluhisho la kutibu ugonjwa huo ni kukikata hicho kiungo.

Mtume Paulo alifananisha mafundisho ya uongo ya Himenayo na Fileto na ugonjwa huo wa Donda-Ndugu.

FILETO na HIMENAYO walianza kuwafundisha watu kuwa Kiyama kimeshapita. Hakuna tena kiyama kinachokuja mbeleni, unyakuo umeshapita zamani, na hautakuja tena..

Na kwasababu mafundisho hayo ni mafundisho hatari, maana yake yasipokataliwa na kuzuiliwa vikali ni rahisi kusambaa kwa watu wengi na kusababisha imani za watu wengi kuvurugika na watu wengi kufa kiroho.

Watu wakishaamini kuwa hakuna tena unyakuo unaokuja, kitakachofuata ni kupoa na kuendelea na dhambi na anasa, hata kama watajiita bado ni wakristo, lakini ndani yao hakuna tena tumaini lolote la maisha yanayokuja. Utaona tena Mtume Paulo, analionya kanisa la Thesalonike juu ya mambo hayo hayo..

2Thesalonike 2:1 “Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake,

2 kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.

3 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;

4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.

5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?

6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake”.

Hata sasa Unyakuo bado haujatokea, lakini siku yoyote kuanzia sasa, kanisa litaondolewa, na watakatifu wakweli walioukataa ulimwengu na kujitakasa kwa Neno, watanyakuliwa juu katika utukufu, na duniani kitakachokuwa kimesalia ni dhiki kuu ya Mpinga-Kristo.

Sasa hivi kuna mafundisho mengi yamezalika ndani ya Imani ya Kikristo, wapo wanaosema kwamba hakuna unyakuo wa kanisa, wapo wanaosema kuwa unyakuo umeshapita, na sasa tupo katika utawala wa miaka elfu moja, Wengine wanaamini kuwa mamlaka ya Bwana Yesu imeshapita, sasa tupo mamlaka nyingine,  ya Mungu Baba na mafundisho mengine mengi sana…

Na mafundisho haya katika siku hizi za mwisho yameenea kama donda-ndugu kiasi kwamba hata kuwabadilisha tena watu wayarudie maandiko inakuwa ni ngumu.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Group la whatsapp Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada Nyinginezo:

Je! Siku ya unyakuo watoto wachanga watanyakuliwa?

TOFAUTISHA KATI YA MAFUNDISHO YA YESU, NA YA WAANDISHI.

Je ni lazima kupitia mafundisho ya muda mrefu kabla ya kubatizwa?

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.

Sadaka ya Amani ilikuwaje?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Kaijage
Kaijage
2 years ago

Amen 🙏MUNGU awabarik sana kwa hayo mafundisho mazuri ya kuujenga mwili wa KRISTO.

Getrude Charles
Getrude Charles
2 years ago

Amina mtumishi wa Mungu, kiukweli saivi kuna mafundisho ya kila aina hapa chini ya jua. Lakini kwa neema ya kristo yesu inatupasa tuendelee kuyatafuta mafundisho ya kweli na kutafakari neno kwani ndio njia pekee itakayo tufikisha katika uzima wa milele. Amen