NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE

Tangu kipindi cha Bwana Wetu Yesu Kristo kuondoka duniani mpaka sasa imepita miaka takribani elfu mbili na katika hichi kipindi cha miaka hii elfu mbili kanisa limekuwa likipitia katika vipindi tofauti tofauti saba vinavyoitwa NYAKATI SABA ZA KANISA, kulingana na kitabu cha..

Ufunuo 1:12-20″ Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu;

13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.

14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto;

15 na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.

16 Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking’aa kwa nguvu zake.

17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,

18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.

19 Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo.

20 Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba.

Amen.

Ufunuo huu alipewa Yohana na Bwana Yesu alipokuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, akionyeshwa jinsi kanisa litakavyokuja kupitia katika siku za mwisho. Leo hii si rahisi sana kuona kitabu cha ufunuo kikiguswa au kuelezewa katika kanisa, na shetani hataki watu wafahamu siri zilizoandikwa katika hiki kitabu maana ndio kinaelezea hatma ya mambo yote ikiwemo na shetani mwenyewe. Kwahiyo ndugu fungua moyo wako ujifunze na Mungu akusaidie unapoenda kusoma ujue ni wakati gani tunaishi na jinsi Bwana Yesu alivyo mlangoni  kurudi kuliko hata unavyoweza kufikiri.

Tafadhali pitia taratibu mpaka mwisho ili uelewe.

  • vile vinara saba vinavyozungumziwa ni makanisa saba tofauti tofauti ambayo yamepita tangu wakati wa Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani hadi wakati tunaoishi sasa.
  •  Na zile nyota saba ni malaika saba/wajumbe wa duniani(wanadamu 7 ambao Mungu aliwatia mafuta ) kupeleka ujumbe kwa hayo makanisa saba. Kila mjumbe kwa kanisa lake.

NYAKATI YA KWANZA:

Kanisa: Efeso

Malaika/Mjumbe: MTUME PAULO

kipindi cha kanisa: 53AD -170AD

Tabia ya kanisa: limeacha upendo wake wa kwanza,tangu wakati wa mauaji ya wakristo yaliyoongozwa na Nero mtawala wa Rumi hadi kifo cha mtume Yohana. Na kipindi hiki ndipo matendo ya wanikolai yalianza kuingia katika kanisa (mafundisho ya kipagani). kuanza kujichanga na ukristo. ufunuo 2:1-7

onyo kwa kanisa- litubu lirudi katika upendo wake wa kwanza, lililopoteza.

Thawabu: Yeye ashindaye atapewa kula matunda ya mti wa uzima ulio katika bustani ya Mungu.

NYAKATI YA PILI;

Kanisa; Smirna

Malaika/Mjumbe;IRENIUS

kipindi cha kanisa: 170AD -312 AD

Tabia ya kanisa; Ni kanisa lilopitia dhiki nyingi kutoka katika utawala mkali wa Diocletian wa Rumi , watakatifu wengi waliuawa katika hichi kipindi kuliko kipindi chochote katika historia ya kanisa.walichinjwa wengi, na wengine kutupwa kwenye matundu ya simba na wanawake kukatwa matiti na kuachwa mbwa walambe damu zao, na ukatili mwingi sana wakristo walitendewa katika hichi kipindi lakini walistahimili dhiki zote hizi soma kitabu cha (Foxe’s book of Martyr- kwenye archives zetu kinaelezea vizuri mauaji ya wakristo).

Japo wakristo walikuwa maskini sana  Lakini Kristo aliwafariji kuwa wao ni  Matajiri. ufunuo 2:8-11

Thawabu; Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.

NYAKATI YA TATU;

Kanisa ; Pergamo

Malaika/Mjumbe; MARTIN

Kipindi; 312AD -606AD

Tabia ya kanisa; Kanisa laingiliwa na mafundisho ya uongo zaidi, ambayo ndio yale matendo ya wanikolai sasa wakati huu yamegeuka kuwa mafundisho ya kidini. Ukristo ukaoana na upagani ukazaa Kanisa mama mfu Katoliki, katika baraza la Nikea AD 325 siasa na mafundisho ya miungu mitatu,ibada za sanamu na za wafu,sherehe na sikukuu za kipagani, ubatizo wa Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, vyeo vya upapa n.k ndipo vilipochipukia. kwa mambo haya basi ikasababisha kanisa kuingia katika kipindi kirefu cha giza (Dark age). Ufunuo 2:12-17

Onyo kwa kanisa: litubu lirudi katika imani iliyoanzishwa na mitume wa Kristo

Thawabu; Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, ila yeye anayelipokea.

NYAKATI YA NNE:

Kanisa; Thiatira

Malaika/Mjumbe;COLUMBA

Kipindi; 606AD -1520AD

Tabia ya kanisa; Japo kanisa lilikuwa na juhudi na bidii katika kumtafuta Mungu, lakini bado lilikuwa na mafundisho ya yule mwanamke kahaba Yezebeli yaani mafundisho ya Kanisa Katoliki.

Onyo; Litubu litoke katika mafundisho ya wanikolai. Ufunuo 2:18-29

Thawabu: Yeye ashindaye na kuyatunza matendo yangu hata mwisho nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.

NYAKATI YA TANO:

Kanisa; Sardi

Malaika/Mjumbe; MARTIN LUTHER

kipindi; 1520AD -1750AD

Tabia; Ni kanisa lililokuwa linarudi katika matengenezo kutoka katika mafundisho ya yule kahaba mkuu kanisa katoliki. lakini lilikuwa bado na Jina lililokufa, wakishikilia baadhi ya mafundisho ya kanisa mama katoliki, huku ndiko chimbuko la walutheri lilipoanzia.Ufunuo 3:1-6

Onyo: litubu, lirejee kwenye mafundisho ya mitume.

Thawabu; Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri Jina lake mbele za baba yangu na mbele ya malaika zake.

NYAKATI YA SITA;

Kanisa;Filadelfia

Malaika/Mjumbe; JOHN WESLEY

Kipindi; 1750AD -1906AD

Tabia; Ni kanisa lililosifiwa kwa matendo yake mema, lilifanikiwa kujua na kuyarekebisha mafundisho ya uongo Kristo alisema ”tazama nakupa walio wa sinagogi la shetani wasemao kwamba ni wayahudi nao sio, bali wasema uongo, tazama nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda”.ufunuo 3:7-13

Thawabu;Yeye ashindaye nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu, huo Yesalemu mpya ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe lile jipya.

NYAKATI YA SABA;

Kanisa; Laodikia

Mjumbe;WILLIAM BRANHAM

Kipindi;1906- Unyakuo

Tabia; Ni kanisa ambalo sio baridi wala moto, bali ni vuguvugu, Kristo anasema ni heri lingekuwa moto au baridi, hii ndiyo hali ya kanisa tunaloishi sasa mimi na wewe, uvuguvugu mbaya umeingia katika kanisa, watu wanajiona kuwa wanamwabudu Mungu katika uzuri wao wa majengo ya kanisa, kwaya.na injili ya mafanikio, wakidhani kuwa hivyo yatosha tu kumjua Mungu kumbe hawajui wameshaingia katika udanganyifu wa shetani pasipo wao kujua,

Watu wanasema kuwa wanampenda Mungu na bado wanapenda mambo ya ulimwengu huu kama fashion za mitindo ya kisasa wanawake kuvalia mavazi ya nusu uchi, michezo, miziki, muvi, ponography, ulevi. anasa,uasherati,na shughuli za ulimwengu huu ambazo zinawasonga wengi hususani kwa kizazi hichi cha ubize, watu wanapata muda wa kufanya kazi sana, lakini muda wa kumtolea Mungu hawana na bado ni wakristo., huu ndio uvuguvugu Kristo anaouzungumzia kwa kanisa letu la Laodikia.Hapa Kristo anasema unajiona kuwa tajiri kumbe ni maskini na mnyonge na uchi na unamashaka na kipofu, jiulize ni hali gani ya kanisa tulilopo sasa. 

Na hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hili, na ndio linakaribia kuisha. jiulize umejiwekaje tayari kumpokea Bwana Yesu akirudi mara ya pili?. Mungu alimtuma mjumbe wake ndugu William Branham kulionya kanisa letu lirudi katika NENO na imani iliyohubiriwa na mitume pamoja na utakatifu.

Onyo; Kristo anasema kanisa liwe na bidii likatubu na kumgeukia Mungu.

Thawabu;Yeye ashindaye nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na baba yangu katika kiti chake cha enzi. ufunuo 3:14-22

Watu wa Mungu hili ndilo kanisa la mwisho tunaloishi hakutakuwa na kanisa lingine baada ya hapa, tunaishi katika wakati ambao Kristo yupo mlangoni kulichukua kanisa lake teule, JIULIZE! UMEKWISHA KUJIWEKA TAYARI KUMLAKI BWANA, TAA YAKO INAWAKA??UMEMPOKEA ROHO MTAKATIFU??YEYE ALIYE NA SIKIO, NA ALISIKIE NENO HILI AMBALO ROHO AYAAMBIA MAKANISA.

Mungu akubariki

MARAN ATHA!


Mada Nyinginezo:

MIHURI SABA

UBATIZO SAHIHI NI UPI?

ROHO SABA ZA MUNGU NI ZIPI? NA JE ZINATOFAUTIANA NA ROHO MTAKATIFU?

HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)?


Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Clever Shukrani
Clever Shukrani
2 years ago

Shalom

Mohamed kassim
Mohamed kassim
2 years ago

Amin amin.
Be blessed bro
Lakini ninaswali linanitatiza.
Ni kwamba umepataje kujua kuhusu Hawa malaika saba??? Yaani nyakati zao na majina yao???
Ubarikiwe sana ndugu

sir benjamin assaph king
sir benjamin assaph king
3 years ago

shalom mtumishi wamungu; nafurahia sana masomo haya , na pia nasoma kwa hali ya juu zaidi kujua na kupata ufahamu vizuri zaidi. ningeomba kupata mfululizo wake, yaani mfululizo wa masomo haya ikiwezekana; ahsante sana nipo dar es salaam hapa; eneo ni kinyerezi tabata; nina huduma yangu hapa ya maombi na maombezi;- mbarikiwe sana sana:-