Midiani ni nchi gani kwasasa?.

Midiani ni nchi gani kwasasa?.

Midiani kwasasa ni eneo la Mashariki mwa nchi ya Saudi-Arabia, Kusini mwa nchi ya Yordani. Asili ya waMidiani ni Ibrahimu.

Maandiko yanaonyesha baada ya Sara kufa, Ibrahimu alimwoa mwanamke mwingine aliyeitwa Ketura, na huyu Ketura, alikuja kuzaa Watoto 6 wa kiume , na mmojawapo wa Watoto hao aliitwa Midiani, ambaye ndiye Baba wa wa-Midiani.

Mwanzo 25:1 “Ibrahimu alioa mke mwingine jina lake akiitwa Ketura.

2 Akamzalia Zimrani, na Yokshani, na Medani, na MIDIANI, na Ishbaki, na Sua”.

Wamidiani walikuwa wanamwabudu Mungu wa Ibrahimu isipokuwa si katika sheria za Musa kama Israeli walivyofanya, kwasababu Torati ilikuja miaka mingi baada ya Midiani kuwa Taifa kubwa.

Wamidiani walimtumikia Mungu katika mfumo wa sadaka za kafara kama alivyofanya Ibrahimu, hawakumjua Mungu kwa mapana ( yaani katika sheria kama Israeli walivyomjua walipokuwa jangwani). Na hiyo ni kwasababu ahadi ya agano Mungu aliyompa Ibrahimu,  ilikuwa ni kwa Ibrahimu na mwanaye  Isaka mwana wa Sara na si kwa wana wa Ketura.

Hivyo wamidiani walimtumikia Mungu wa Ibrahimu lakini si kwa usahihi wote. Ndio maana tunakuja kumwona Mkwewe Musa aliyeitwa Yethro (au Reuli) ambaye alikuwa ni Mmidiani kwa asili, maandiko yanasema alikuwa ni “kuhani” wa nchi hiyo ya Midiani (soma Kutoka 2:16).

Ikiwa na maana kuwa alikuwa anafanya kazi za kikuhani kama Haruni lakini si katika ukamilifu wote kama walivyokuwa wanafanya akina Haruni na wanawe.

Hivyo kwaasili waMidiani walikuwa ni ndugu ya Israeli kupitia Ibrahimu. Lakini baadaye tunakuja kusoma wamidiani waligeuka na kuwa madui wa kubwa wa Israeli, kipindi Israeli wanatoka Misri kuelekea Kaanani hawa wamidiani walijiunga na WaMoabu na kumwajiri mtu aliyeitwa Balaamu ambaye alikuwa ni mchawi kutoka Midiani kuja kuwalaani, jambo ambalo lilimchukiza sana Mungu, na kufanya Mungu awalipize kisasi wamidiani kwa kosa hilo.

Hesabu 31:1 “Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

2 Walipize kisasi wana wa Israeli juu ya Wamidiani; kisha baadaye utakusanywa uwe pamoja na watu wako.

3 Basi Musa akanena na watu, na kuwaambia, Wavikeni silaha watu miongoni mwenu waende vitani, ili waende kupigana na Midiani, wapate kumlipiza kisasi Bwana, juu ya Midiani”.

Lakini Ijapokuwa Mungu aliwapiga waMidiani karibia wote, lakini hawakuisha wote.. Wamidiani walikuja kunyanyuka tena na kuwa Taifa kubwa, na lenye nguvu kuliko hata Israeli.

Na miaka kadhaa baadaye Israeli walipomwacha Mungu, na kwenda kuabudu miungu mingine, Mungu aliwatia waisraeli mikononi mwa hawa Wamidiani wawatese, na Waisraeli wakateswa miaka 7 na waMidiani, mpaka walipomlilia Bwana, na kupelekewa mwokozi awaokoe (ambaye alikuwa ni Gideoni).

Waamuzi 6:1 “Kisha wana wa Israeli walifanya yaliyo maovu mbele za macho ya Bwana; Bwana akawatia mikononi mwa Midiani muda wa miaka saba

2 Mkono wa Midiani ulikuwa na nguvu juu ya Israeli; tena kwa sababu ya Midiani wana wa Israeli walijifanyia hayo mashimo yaliyo milimani, na hayo mapango, na hizo ngome.

3 Basi ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamepanda mashamba, Wamidiani wakakwea, na Waamaleki, na hao wana wa mashariki; wakakwea juu yao;

4 wakapanga marago juu yao, na kuyaharibu hayo maongeo ya nchi, hata ufikapo Gaza, wala hawakuacha katika Israeli riziki ziwazo zote; kondoo, wala ng’ombe, wala punda.

5 Kwa maana walikwea na ng’ombe zao na hema zao, wakaja mfano wa nzige kwa wingi; wao na ngamia zao pia walikuwa hawana hesabu; nao waliingia katika hiyo nchi ili kuiharibu.

6 Israeli walitwezwa sana kwa sababu ya Wamidiani; nao wana wa Israeli wakamlilia Bwana.

7 Kisha ikawa, hapo wana wa Israeli walipomlilia Bwana kwa sababu ya Midiani,

8 Bwana akamtuma nabii aende kwa hao wana wa Israeli; naye akawaambia, Bwana, yeye Mungu wa Israeli, asema hivi, Mimi niliwaleta ninyi mkwee kutoka Misri, nikawatoa katika nyumba ya utumwa;

9 nami niliwaokoa na mikono ya Wamisri, na mikono ya wote waliokuwa wakiwaonea, nami niliwafukuza watoke mbele zenu, nami niliwapa ninyi nchi yao;

10 kisha niliwaambia, Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu; msiiche miungu ya Waamori, ambayo mwaketi katika nchi yao; lakini hamkuitii sauti yangu.

11 Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.

12 Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa”.

Jamii ya Wamidiani kwasasa haipo, bali imemezwa na jamii nyingine za Arabia na Yordani na Misri, kiasi kwamba kwasasa hakuna ajijuaye kama yeye ni mmidiani au la!.

Lakini tunachoweza kujifunza kwa Habari ya Wamidiani ambao walikuwa ni maadui wa Israeli kwa kipindi chote, ni kuwa “maadui wanatabia ya kuchipuka tena”.

Wamidiani waliuawa karibia wote na mali zao kutekwa nyara na wa Israeli, kwaufupi ni kama vile walifutwa juu ya uso wa nchi, lakini tunaona walikuja kuchipuka tena na kuwa Taifa kubwa tena lenye nguvu kuliko Israeli, na tena likawatawala Israeli. Lakini hiyo yote ni matokeo ya Waisraeli kumwacha Mungu.

Vile vile na sisi tukimwacha Mungu, haijalishi yale magonjwa ambayo yalikuwa yameondoka miaka mingi na hatuyaoni tena, yatarudi tena na kuchipuka kwa nguvu na kutuangamiza!.

 Tukimwacha Mungu haijalishi tulikuwa na ushindi mkubwa kiasi gani dhidi ya mapepo na wachawi!, tukimwacha Mungu Watanyanyuka tena na kutudhuru na kututesa!.

Tukimwacha Mungu na kurudia ulevu, uzinzi, wizi, uvaaji mbaya, utukanaji…haijalishi tulikuwa na ushindi mkubwa dhidi ya shetani hapo kabla…atanyanyuka tena na jeshi lake kwa nguvu na kuteka nyara… Israeli hawakutegemea kama Taifa walilopiga na karibia kulitowesha kabisa, leo lingekuja kuwatawala kwa miaka 7 tena kwa utumwa mkali.

Na sisi hatuna budi kujifunza katika haya, ili tusifanya makosa waliyofanya Israeli.

1Wakorintho 10:11 “Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.

12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke”.

Bwana atusaidie nasi pia tusirudi nyuma.. kusudi tusije tukampa nguvu adui yetu shetani.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

Je ni kweli Musa alikuwa mtu mpole kuliko wote duniani?

Ninawi ni nchi gani kwasasa?

Babeli ni nchi gani kwasasa?

Moabu ni nchi gani kwasasa?

Ni lini na wapi Ibrahimu aliioona siku ya Bwana akashangilia?.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Charles Athanas chishsyela
Charles Athanas chishsyela
1 year ago

Asante

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Asante