Je! mwanadamu wa kwanza kuumbwa ni yupi?

Je! mwanadamu wa kwanza kuumbwa ni yupi?

Je! mwanadamu wa kwanza kuumbwa ni yupi Mzungu, mwafrika au Mchina na kama ni mmojawapo kati ya hao je hao wengine wametoka wapi?

JIBU: Ni muhimu kufahamu kuwa Mungu aliiumba jamii moja tu ya watu..Hakuumba jamii nyingi za watu pale Edeni na hii jamii tunaipata kutoka kwa Adamu na Hawa

(Mwanzo 1: 27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba ).

Watu Hawa wawili ndio Mungu aliowaumba kwa ukamilifu wote bila kasoro kubwa wala ndogo,sasa Adamu na mke wake hawakuwa wazungu hapo mwanzo, kama wengi wanavyodhani, au waafrika au wachina au wahindi au jamii nyingine yeyote ya watu tunayoiona leo. la! Adamu na Hawa walikuwa ni watu wenye upekee wao ambao leo hii hatuwezi kuuona kwa mtu yeyote aliyeko duniani, wala hakuna mfano wa kulinganishwa nao kwa uzuri na mvuto waliokuwa nao kwasababu Mungu aliwaumba wakamilifu sana pasipo mapungufu yeyote. Lakini baada ya wao kumkosea Mungu na kuasi ule ndipo utukufu waliokuwa nao ukaanza kuondoka kidogo kidogo na mauti kuingia ndani yao.Siku baada ya siku wakaanza kubadilika mionekano yao ikaanza kuwa kama yetu sisi tunavyoonekana sasa hivi.

Hivyo miili yao ikaanza kubadilika ghafla kutokana na kwamba Utukufu wa Mungu umewaondokea, ardhi ikalaaniwa kama tunavyosoma, jua likaanza kuwa kali, mimea ikaanza kukauka baadhi ya maeneo, na kusababisha majagwa kutokea duniani, jasho likaanza kuwatoka kutokana na jua kuwa kali, ngozi zikazidi kubadilika, makovu yakaanza kutokea..Watu wakaanza kuzaliana kwa kasi na baada ya gharika dunia ilipozidi kuharibika zaidi na kupoteza taswira iliyokuwa nayo kwanza, tunakuja kuona watu wakaanza kuweka tena ustaarabu mpya duniani wakaanza kujenga ule mnara wa Babeli ili wamfikie Mungu..Lakini Mungu alipoona matendo yao ndipo akawatawanya waende katika pembe zote za dunia..

Mwanzo 11:1 Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.

2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.

3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.

4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.

5 Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.

6 Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.

7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.

8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.

9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote.

Sasa kuanzia hapo jamii ya watu walikwenda zile sehemu zenye majangwa, wakakaa huko, wengine walikimbilia nchi za baridi, wakaa kaa huko, wengine sehemu za barafu, wengine visiwani, wengine misituni n.k…Hivyo walipoendelea kukaa kwa muda mrefu kutokana na mazingira waliyopo, wakaanza kuendana na yale mazingira, ndipo watu wakaonekana tofuati zao kulingana na mahali walipotokea.. Kwa mfano watu waliokuja pande za Afrika, mazingira ya huku tunafahamu ni ya joto, hivyo ni dhahiri kuwa ngozi ikipigwa na jua kwa muda mrefu inakuwa nyeusi, na pia nywele zinapungua..

kwahiyo hatushangai kuona watu wa Afrika ni weusi, kadhalika na watu waliopo nchi za baridi miili yao kwa kawaida itahitaji joto, hivyo nywele zitalazimika kukua na kuwa ndefu huko ndipo tunapowaona watu jamii ya wazungu, ukitazama nchi kama ya India, wahindi waliopo pande za kaskazini za baridi kama DELHI n.k utaona ngozi yao ni nyeupe, kadhalika waliopo pande za kusini(mf. Sri Lanka) ambako kuna joto kali utaone ngozi yao umefifia kidogo(inakuwa nyeusi) n.k.

Na kumbuka hii sio tu kwa wanadamu..bali hata kwa wanyama..Kama ukichunguza wanyama kama kondoo,ng’ombe au mbuzi mwitu, au farasi,mbwa,tembo n.k wanaotoka nchi za baridi utawaona wana manyoya mengi zaidi, kuliko wale wanaotokea nchi za joto.

Hivyo kwa ufupi mazingira ndiyo yaliyowabadilisha watu, na si kingine.

Shalom.

 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada Nyinginezo:

JE! ADAMU ALIWASALIANA NA MUNGU KWA LUGHA IPI PALE BUSTANINI?

JE! NGOZI NYEUSI ILILAANIWA ?

MNARA WA BABELI

DAMU YA ZAKARI BIN BARAKIA.

 KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA.

HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Alexander
Alexander
10 months ago

Sasa kama mazingira ni sababu ya watu kuwa weupe na weusi na aina nyingine je! Mbona ulaya watu weusi wanaendelea kuzaliana?????