Mfano ule Yesu alioutoa wa Kabaila aliyesafiri katika nchi ya mbali, una maana gani (Luka 19:12-27) ?!!

Mfano ule Yesu alioutoa wa Kabaila aliyesafiri katika nchi ya mbali, una maana gani (Luka 19:12-27) ?!!

JIBU: Tusome.. 

Luka 19:12 “Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.

13 Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hata nitakapokuja.

14 Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.

15 Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake.

16 Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi.

17 Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.

18 Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida.

19 Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.

20 Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso.

21 Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.

22 Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;23 basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake?

24 Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi.

25 Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi.

26 Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang’anywa hata alicho nacho.

27 Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa mwachinje mbele yangu”.

Shalom!

Mfano huo Bwana aliutoa alikuwa anajizungumzia yeye na kanisa lake. 

Huyo Mtu Kabaila aliyesafiri kwenda nchi ya mbali ni BWANA wetu YESU mwenyewe, (KABAILA maana yake ni MTU ALIYEZALIWA KATIKA FAMILIA YA JUU ZAIDI KATIKA JAMII inaweza kuwa familia ya kifalme au kichifu,nk) kama tunavyojua, Bwana Yesu asili yake ni Mbinguni ametoka katika familia ya kimbinguni, na ndio maana hapa anajifananisha na huyu Kabaila, tunaona na baada ya kumaliza tu kazi yake alipaa kwenda mbingu za mbingu..sasa hiyo ndiyo nchi ya mbali inayozungumiwa pale kwenye huo mfano, Na amekwenda kule kwa makusudi kabisa ili kutuandalia sisi makao ili arudi tena kuja kutuchukua. Na kama mfano unavyosema “akawaita watumwa wake kumi akawapa mafungu 10 ya fedha” maana yake ni kwamba Bwana wakati anaondoka duniani siku ile alituachia sisi Roho wake Mtakatifu..kisha akatugawia majukumu kama agizo kuu, akatuambia tukahubiri injili kwa kila kiumbe ili kuleta faida katika ufalme wa mbinguni, aaminiye na kubatizwa ataokoka, kwahiyo Roho Mtakatifu aliachiliwa juu ya kila mwamini kila mmoja kwa kiwango chake cha neema alichopewa, hilo ndio fungu la fedha kwenye huo mfano (Matendo 2:38)..

Ukichunguza pia utaona hawakuambiwa wakafanye biashara moja, hapana kila mmoja alikuwa na uhuru wa kufanya biashara yake, hii ikiwa na maana kila mmoja anayo karama yake Mungu kampa. Na kwa kupitia hiyo utaulizwa uliitumiaje katika mambo yahusuyo ufalme wa mbinguni. 

Uwe ni mwinjilisti uwe ni mwalimu uwe ni mchungaji n.k. Na kama huo mfano unavyosema kwamba kuna siku moja yule kabaila alirudi, na kuanza kuwauliza wale watu aliowapa yake mafungu kila mmoja ameleta faida kiasi gani katika biashara, Ndivyo itakavyokuwa kwetu kila mmoja ataenda kutoa hesabu mbele ya Bwana wetu YESU siku ile. kaitumiaje neema aliyopewa duniani Ndipo atakapowakusanya watumishi wake wote, na kuanza kumlipa mmoja baada ya mwingine kulingana na jinsi alivyotumika katika huduma, katika nafasi yake ya kuhubiri injili..waliotumika kwa uaminifu watalipwa thawabu kubwa zaidi, lakini waliozembea au waliokuwa wanafanya kazi ya Mungu kwa ulegevu na uvivu, au kinyume cha Neno Bwana anasema atawanyang’anya na thawabu yao na kupewa watu wengine. 

Kwahiyo hiyo ndio maana ya mfano huo, unatufundisha kuwa makini sana na Neema Mungu aliyotupa ya Roho wake Mtakatifu, na karama alizotupa, kwamba siku moja tutakwenda kuulizwa, kama umepewa karama ya kuhubiri, au kufundisha halafu haufundishi inavyopaswa au kulingana na Neno, au unakuwa mvivu na kuendelea na mambo yako mengine na kuidharau kazi ya Mungu…Basi siku za mwisho utakwenda kuulizwa..Kama ulipewa karama ya kuhubiri kwa njia ya uimbaji na uimbaji wako hauna tofauti na waimbaji wa miziki ya kidunia, kila mtu akutazamapo anaona kitu tofauti na unachoimba, utakwenda kuulizwa siku ile. Ndio maana Bwana anasema..

Ufunuo 22:12 “Tazama, naja UPESI, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”.

Ubarikiwe.

Mada Nyinginezo:

JIFANYIE RAFIKI KWA MALI YA UDHALIMU.

BWANA ALIMAANISHA NINI KWENYE MSTARI HUU MARKO 2:21″ HAKUNA MTU ASHONAYE KIRAKA CHA NGUO MPYA KATIKA VAZI KUKUU;?

NI KWASABABU YA YESU KRISTO.

ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.

NINI MAANA YA HILI ANDIKO “USHUHUDA WA YESU NDIO ROHO YA UNABII” (UFUNUO 19:10)?

MTEGEMEE MUNGU, NA SI MWANADAMU.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments