Wapendwa nini maana ya hili andiko “Ushuhuda wa YESU ndio ROHO YA UNABII” (ufunuo 19:10)?

Wapendwa nini maana ya hili andiko “Ushuhuda wa YESU ndio ROHO YA UNABII” (ufunuo 19:10)?

JIBU: Biblia inaposema ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii…inamaanisha kuwa mtu yeyote ambaye anajiona kuwa anayo roho ya kinabii ndani yake au anayejiita nabii, kama maisha yake au mahubiri yake hayalengi katika kumshuhudia YESU KRISTO BWANA WETU..basi huyo ni nabii wa uongo ushuhuda wake ni wa uongo!..hata kama atakuwa anaona maono kiasi gani, au anatabiri na kutenda miujiza kiasi gani huyo bado sio nabii wa kweli, ni nabii wa uongo..

Biblia inasema katika..

1 Yohana 5:9-11“9 Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana USHUHUDA WA MUNGU NDIO HUU, KWAMBA AMEMSHUHUDIA MWANAWE.

10 Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu ANAO HUO USHUHUDA NDANI YAKE Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.

11 Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.” 

Hivyo ili tumtambue kama huyu ni nabii kutoka kwa Mungu au la! …hatupaswi kukimbilia kuangalia miujiza anayofanya, au maono anayoona, tutampima kwa ushuhuda anaouhubiri (Neno la Kristo) je! anaturudisha kwa YESU? Anamuhubiri Yesu yule wa Kalvari? Yesu yule aliyesema mtu akinifuata ajikane nafsi yake ajitwike msalaba wake anifuate, Yesu yule aliyesema “itamfaidia nini mtu kupata ulimwengu mzima na kupata hasara ya nafsi yake” kama atamhubiri Yesu huyu basi hata asipofanya muujiza hata mmoja, au kutabiri huyo ni nabii wa kweli kwasababu anao ushuhuda wa Yesu Kristo ambayo ndio Roho ya unabii. Unamkumbuka Yohana mbatizaji, yeye hakuwahi kufanya muujiza hata mmoja, wala ishara yoyote..lakini ushuhuda wake ulikuwa ni nini?..ulikuwa ni kuwapeleka watu kwa YESU, na si kingine..lakini Bwana alimwambiaje?…yeye ni zaidi ya NABII..na hakuna aliyetokea kama yeye hata Musa hakuwa mfano wake. 

Lakini kitu gani kilichopo sasahivi…watu wanajiita manabii wanatabiri lakini hawana ushuhuda wa Yesu Kristo ndani yao, mungu wao ni tumbo, wanahubiri tu mafanikio ya ulimwengu huu na kukwepa mafundisho ya kumpeleka mtu mbinguni na toba, kama biblia inavyosema katika

Wafilipi 3:18-21 “18 Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, KUWA NI ADUI ZA MSALABA WA KRISTO;

19 mwisho wao ni uharibifu, MUNGU WAO NI TUMBO, utukufu wao u katika fedheha yao, WANIAO MAMBO YA DUNIANI.

20 KWA MAANA SISI, WENYEJI WETU UKO MBINGUNI; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;

21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.” 

Kwahiyo roho yoyote isiyoturudisha kwa YESU KRISTO na maneno yake, hiyo ni roho ya Yule mwovu, ikivaa kinyago cha roho ya kinabii, hivyo ili ile Roho ya kinabii iwe juu yako inakupasa kumshuhudia YESU KRISTO katika maisha yako na katika huduma yako.

 Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinaendana:

NI KWASABABU YA YESU KRISTO.

MJUE SANA YESU KRISTO.

VIGEZO VYA KUWA KARIBU NA YESU KRISTO KATIKA ULIMWENGU UJAO.

CHAKULA CHA ROHONI.

SWALI LA KUJIULIZA!


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments