MTO YORDANI UKO NCHI GANI KWA SASA?

MTO YORDANI UKO NCHI GANI KWA SASA?

Mto Yordani uko nchi gani kwa sasa duniani?


Mto Yordani upo katika eneo la Mashariki ya kati, ni mto ambao unasimama kama mpaka wa mataifa mbalimbali, Ikiwemo Lebanoni, Syria, Israeli, na Yordani.

Ni kama vile ziwa Tanganyika lilivyo simama kama mpaka wa nchi 4, Congo, Burundi, Tanzania, na Zambia ndivyo ilivyo hata na kwa mto Yordani,

Nchi ya Yordani, unayoisikia leo hii pale mashariki ya kati, imechukua jina lake kutoka katika mto huu.

Mto huu chanzo chake ni kwenye chemchemi kadhaa zinazotiririka kutoka katika mlima Hermoni ulio mpakani mwa Lebanoni na Syria.Kisha kutoka hapo unateremsha maji yake mpaka Israeli kwenye bahari ya Galilaya/Tiberia/Genesareti. Na kutoka hapo unaibukia upande wa pili na kuendelea na safari yake moja kwa moja mpaka bahari ya Chumvi.

Tazama picha chini.

Chanzo cha mto Yordani Mashariki ya kati

Mto huu, umekuwa kitovu katika historia ya Israeli kuanzia agano la kale mpaka agano jipya. Yoshua aliusimamisha mto huu na wana wa Israeli wakavuka kuelekea Yeriko.

Vilevile mto huu huu katika agano jipya ndio makutano mengi yalikuwa yanavuka kumwendea Yesu ili waponywe.(Mathayo 19:1-2),  Na ni mto ambao Yesu mwenyewe  alibatiziwa.

Kuonyesha kuwa ili nawe upate wokovu na ushindi dhidi ya maadui zako,na ili uponywe nafsi yako, ni lazima Uvuke Yordani yako ya Rohoni..Ili ukakutane na Yesu ng’ambo ya pili huna budi kuvuka Yordani, Na Unavukaje Yordani? Ni kwa kubatizwa, kama Yesu alivyobatizwa kwenye mto ule.

Hivyo na wewe sharti ukishamwamini Yesu moja kwa moja ukabatizwe, mahali popote penye maji tele kama ishara ya kuwa umeokoka kweli kweli. Na kuwa unakwenda kuwashinda maadui zako.

Marko 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.

Wengi wanapuuzia maagizo haya ya msingi, wanadhani kuamini tu inatosha, Ndugu kubatizwa ni tendo lenye maana kubwa sana kwako rohoni, aliyetupa maagizo hayo hakuwa amekosa cha kutuagiza bali alijua umuhimu wake.

Swali Nji wewe umebatizwa ipasavyo? Kama sivyo basi kafanye hivyo.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda masomo yetu yawe yanakufikia njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Israeli ipo bara gani?

Wafilisti ni watu gani.

 

MJUMBE WA AGANO.

Zile mbao mbili za mawe Musa alizoambiwa achonge zilikuwaje?

Mlima sinai upo nchi gani? Na Je unaijua Sinai yako ya rohoni?

CHUKIZO LA UHARIBIFU

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
JANKEN mwansasu MJWANGA
JANKEN mwansasu MJWANGA
3 years ago

Shalom shalom! Mungu akubariki kwa masomo mazuri nafarijika pamoja na kuelimika.