Mto Frati upo nchi gani, na Umuhimu wake katika biblia ni upi, kwanini utajwe sana?
Mto Frati ni moja ya mito mikubwa na mirefu iliyopo Mashariki ya kati, Mto mwingine ukiwa ni Hidekeli (Tigris), mto huu unaanzia Uturuki na kutoka hapo unakatiza katika nchi ya Syria na Iraq na kwenda kumwaga maji yake katika Ghuba ya uajemi.
Tazama picha.
Mto Frati na Mto Hidekeli (Tigris) ni moja ya mito minne ambayo inatajawa kwenye biblia ilikuwa inatoa maji katika bustani ya Edeni.
Mwanzo 2:10 “Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji, na kutokea hapo ukagawanyika kuwa vichwa vinne. 11 Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu; 12 na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham. 13 Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi. 14 Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati”.
Mwanzo 2:10 “Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji, na kutokea hapo ukagawanyika kuwa vichwa vinne.
11 Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu;
12 na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham. 13 Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi.
14 Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati”.
Lakini kingine cha kushangaza juu ya mto Frati ni kuwa umetajwa pia kitabu cha Ufunuo, Kama tu vile Babeli ilivyotajwa tangu kwenye kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo. Kuonyesha kuwa kama vile ilivyo Babeli ya mwilini, hivyo hivyo pia ipo Babeli ya rohoni (Ufunuo 17 & 18). Halikadhalika na kwa mto Frati, sio tu ule unaouna pale Mashariki ya kati, hapana bali pia rohoni upo, na siku moja utakauka, na ukishakauka basi dunia itaingia katika vita kuu ya Tatu ya dunia
Ufunuo 9:14 ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue nao malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati. 15 Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu. 16 Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi; nilisikia hesabu yao. 17 Hiyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti. 18 Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao. 19 Kwa maana nguvu za hao farasi ni katika vinywa vyao, na katika mikia yao; maana mikia yao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, nao wanadhuru kwa hivyo”.
Ufunuo 9:14 ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue nao malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati.
15 Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu.
16 Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi; nilisikia hesabu yao.
17 Hiyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti.
18 Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao.
19 Kwa maana nguvu za hao farasi ni katika vinywa vyao, na katika mikia yao; maana mikia yao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, nao wanadhuru kwa hivyo”.
Unaona?. Watu wengi hawajui kuwa kipindi hicho kimekaribia sana,. Lakini kabla hilo halijatokea, kutatungulia kwanza Tukio la UNYAKUO, (kufahamu vizuri unyakuo utakuwaje kuwaje, tazama, masomo yaliyoorodheshwa chini).
Dalili zote zinaonyesha kizazi chetu kitaweza kushuhudia mambo hayo yote. Swali la kujiuliza Je! na wewe umejiwake tayari kwa tukio la kurudi kwa pili kwa Yesu Kristo? Je! Maisha yako yanauhakisi wokovu? Kama sivyo basi jitathimini sasa kwasababu ni kipindi kifupi cha neema tulichobakiwa nacho, Dunia hii inapumbaza kweli na wengi hawalijui hilo, Yesu atakuja kama mwivi usiku.
Hivyo kama upo tayari kumpa Yesu leo maisha yako, hilo jambo la muhimu sana, basi fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba.>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia masomo ya Neno la Mungu kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Tazama chini vichwa vingine vya masomo.
Mada Nyinginezo:
MTO YORDANI UKO NCHI GANI KWA SASA?
UFUNUO: Mlango wa 9.
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
MAONO YA NABII AMOSI.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
Rudi Nyumbani:
Print this post