Zile mbao mbili za mawe Musa alizoambiwa achonge zilikuwaje?

Zile mbao mbili za mawe Musa alizoambiwa achonge zilikuwaje?

SWALI: Zile Mbao za mawe Musa alizoambiwa achonge kwa ajili ya zile amri 10 zilikuwaje?..je ni mbao za miti zilichonganyikana na mawe au zilikuwa ni kitu gani?


JIBU: Neno mbao asili yake sio miti…bali ni kipande cha kitu chochote ambacho kipo bapa, ambacho kinaweza kufaa kwa matumizi mbali mbali kama uandishi au ujenzi. Umoja wa neno mbao ni UBAO. Hivyo ubao unaweza kuwa wa miti, chuma, mawe, glasi au chochote kile.

Hivyo Mbao mbili Musa alizoambiwa achonge hazikuwa za miti, bali za mawe. Na ndizo hizo Mungu alizozitumia kuandikia amri zake. Sasa Kwanini Mungu alitumia mawe na si miti? Ni kwasababu maandishi yaliyoandikwa kwenye mawe yanadumu kwa muda mrefu zaidi ya yale yanayoandikwa kwenye miti…kwasababu miti inaoza na kuharibika na kuliwa na mchwa lakini mawe yanadumu miaka mingi..Hivyo Mungu kuonyesha kwamba Amri zake ni za daima na milele na kwamba hazifutiki ndio maana alitumia mawe.

Lakini Pamoja na hayo mawe yanaweza kuharibika pia na maandishi yale yakapotea miaka inapozidi kuwa mingi…Hivyo Mungu aliruhusu pia amri zile zikae kwenye mawe kwa muda tu, kwasababu mbeleni alikuwa na mpango mwingine maalumu sana wa mahali pa kuziandikia ambapo zitadumu milele.

Hivyo wakati ulipofika, akaleta mpango mwingine wa kuandika amri zake si katika miti wala mawe ambayo yapo leo na kesho kupotea…Ndipo akaleta agano jipya kupitia mwana wake mpendwa ambapo ataziandika amri zake na sheria zake mioyoni mwa watu wake..Humo ndimo mahali pekee ambapo ahaziwezi kufutika kamwe kama maandiko yanavyosema..

Yeremia 31:31“Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.

32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana. 33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia SHERIA YANGU NDANI YAO, NA KATIKA MIOYO YAO NITAIANDIKA; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

34 Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena”

Hivyo ili tuzishike amri za Mungu hatuna budi ziandikwe ndani ya mioyo yetu….Na zinaandikwa tu pale tunamwamini Yesu Kristo na kupokea Roho Mtakatifu. Kumbuka Yesu ndiye mjumbe wa Agano jipya (Malaki 3:1) Hivyo yoyote aliyemwamini, na kupokea Roho wake Mtakatifu amri na sheria za Mungu zinaandikwa katika mbao za moyo wake…anakuwa anazitimiza sheria zile bila kujilazimisha wala kulazimishwa, wala hazimfanyi kuwa mtumwa, kiasi kwamba anapata tabu kuzishika sheria za Mungu…yeye mwenyewe tu anajikuta anazipenda sheria za Mungu na kuzitenda.

Bwana atubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Sanduku la Agano lilikuwa linawakilisha nini katika Agano jipya?

HUDUMA YA (ELIFAZI, SOFARI, NA BILDADI).

Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?

MUUNGANIKO WA MADHEHEBU NI MPANGO WA MPINGA-KRISTO.

IFANYE KAZI YA MUNGU PASIPO HOFU!

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments