SALA YA TOBA

SALA YA TOBA

Sala ya Toba ni nini?..Je ni lazima kuongozwa sala ya Toba pale mtu unapoamini?

Jibu: Sala ya Toba ni sala, ambapo mtu mmoja aliyeamini anamwongoza mwingine ambaye ndio anaingia katika Imani..Mtu anayeingia katika Imani anakuwa anafuatiliza maneno yale kwa Imani na kumkiri Yesu kwa kinywa chake, kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yake na alikufa kwa ajili ya dhambi zake.

Sasa hakuna maagizo yoyote katika biblia yanayosema mtu baada ya kumwamini Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake..basi anahitaji kuongozwa sala ya toba. Hakuna andiko kama hilo,  Lakini lipo andiko moja tu linalosema..

Wagalatia 6:2 “Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo”

Maana yake ni kwamba..aliye dhaifu wa Imani hana budi kushikwa mkono na kusaidiwa kusimama na hatimaye kutembea mwenyewe…Kama vile mtoto mchanga anayejitahidi kusimama ili atembee…Mzazi huna budi kumshika mkono na kumnyanyua na kumsaidia atembee..

Vivyo hivyo katika safari ya Imani. Mtu anayetoka katika dhambi moja kwa moja na kumpokea Kristo ni sawa na kitoto kichanga kilichozaliwa…wengi wa hawa hata kusali tu hawajui, zaidi ya yote hata wakiomba wanahisi Mungu hawasikii…wanakuwa hawajamjua Mungu, wala hawaujui uweza wa Mungu vizuri. Hivyo unapowashika mkono na kuwasaidia kusali pamoja nao kwa mara ya kwanza…Imani zao ni rahisi kukua na kunyanyuka na kusonga mbele.

Lakini ukiwaachia kwamba waombe wenyewe katika siku za kwanza kwanza…ni rahisi shetani kuwaletea mawazo kwamba bado hawajaokoka wala kumpokea Yesu..Hivyo wataendelea siku chache na baada ya hapo ni rahisi  kurudi nyuma. Wapo wachache ambao wanaweza kujishika wenyewe hata kusimama na kukua kiroho bila hata kuongozwa sala hiyo.. lakini wengi wa wanaomwamini Bwana Yesu katika hatua za awali wanahitaji msaada mkubwa sana..Kwasababu ni watoto wadogo kabisa kiroho waliozaliwa.

Lakini baada ya kipindi fulani, wakishakuwa basi hawana haja ya kushikwa tena mkono bali wanapaswa wakawasaidie wengine walio dhaifu kama wao walivyokuwa.

Hivyo sala ya Toba inatokana na upendo wa mkristo kwa mtoto mpya aliyezaliwa kiimani, na sio dhambi kuwaongoza watu wala kuongozwa. Hivyo upendo hauna masharti..Bwana wetu Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kusali..si zaidi sisi kuwafundisha na kuwaongoza sala wale walio wachanga kiroho katika hatua za awali?

Bwana atubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

JE SALA YA ROZARI TAKATIFU NI YA KIMAANDIKO?

NINI KINAFUATA SIKU ILE ILE YA KUOKOKA!

Je! Hamna nyumba za kulia na KUNYWEA?.Mstari huu unahalalisha unywaji wa pombe?

JINSI NEEMA YA MUNGU ILIVYOKUWA KUBWA KWA MKE WA LUTU.

BUSTANI YA NEEMA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments