Wibari ni nani?(Mithali 30:26)

Wibari ni nani?(Mithali 30:26)

SWALI: Wibari ni nani? Na kwanini wanatajwa kama moja wa viumbe wanne wenye akili nyingi?(Mithali 30:26)


JIBU: Wibari ni wanyama wadogo wanaokaribia kufanana na sungura, kwa jina lingine wanajulikana kama pimbi, au kwanga, au perere, tazama kwenye picha.

Wanyama hawa utawaona wakitajwa kwenye vifungu hivi katika biblia;

Walawi 11:4 “Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 5 Na wibari, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu”.

Zaburi 104:18 “Milima mirefu ndiko waliko mbuzi wa mwitu, Na magenge ni kimbilio la wibari”.

Mithali 30:24 “Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana.

25 Chungu ni watu wasio na nguvu; Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari.

26 Wibari ni watu dhaifu; Lakini hujifanyia nyumba katika miamba”.

Lakini ni kwanini wametajwa kama moja ya viumbe vinne vyenye akili nyingi duniani?

Ni kwasababu ya tabia yao, wanyama hawa ni waoga, hawali nyama, wala hawapo machachari sana ukilinganisha na wanyama wengine, hawawezi kukimbia sana, kwa ufupi ni viumbe dhaifu ambavyo ni rahisi kukamatwa na maadui zao, lakini katika udhaifu wao, wanajua ni wapi pa kujihifadhi nafsi zao, na si hapo pengine zaidi ya kwenye miamba.

Wibari wanatengeneza nyumba zao kwenye mapango ya miamba, mirefu, na migumu, kiasi kwamba adui zao ni ngumu kuwaona au kuwakamata, tofauti na wanyama wengine kama ngiri au sungura n.k ambao wao wanachimba mashimo ambayo hata adui zao wanaweza kuwafuatilia na kuyafukua na kuwakamata, au mvua ikija ikajaza mashimbo yao wakafa, au upepo mkubwa ukivuma unaweza kufukia mashimo yao kwa udongo utakaoporomoka au kuingia, hivyo hiyo inawafanya maisha yao kuwa hatarini sana japokuwa ni machachari au wana uwezo mkubwa wa kukimbia.

Lakini wibari kweli sio kama wanyama wengine, ni wadhaifu sana lakini wanafahamu ni wapi wanaweza kuwa salama.

Je na sisi, tutashindwa akili na wibari?

Usalama wetu upo wapi? Je tumeyajenga maisha yetu wetu wapi? Je, ni mashimoni au kwenye vichuguu, au kwenye miti au kwenye mwamba?. Tujue tu kuwa mwamba ni mmoja tu, naye ni YESU KRISTO peke yake. Ukiwa nje ya Kristo, fahamu kuwa maisha yako yapo katika hatari zote, haijalishi utajiona wewe ni mjanja kiasi gani, haijalishi utajiona ni hodari kiasi gani, haijalishi ni tajiri  kiasi gani, shetani atakumaliza tu..Huna safari ndefu..

Sikiliza maneno ya Yesu..

Mathayo 7:24 “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.

26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;

27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa”.

Kweli itakuwa ni ajabu sana tukishindwa akili na mnyama pimbi.

Shalom.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=mJ0AkfAcM4I[/embedyt]

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Mavu ni nini katika biblia?(Kutoka 23:28, Kumb 7:20)

IKO NJIA IONEKANAYO KUWA SAWA MACHONI PA MTU.

Nini maana ya “katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni”.

NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
1 year ago

Nimejifunza kitu kikubwa, nyumba juu mwamba ni salama (maisha ndani ya Kristo ni salama) Mungu awabariki sana

JOSIAH LLOYD MURUVE
JOSIAH LLOYD MURUVE
1 year ago

Mungu awabariki

Angel Emanuell
Angel Emanuell
1 year ago

Amen Amen mbarikiwe sn Mungu azidi kuwatumia