Mavu ni nini katika biblia?(Kutoka 23:28, Kumb 7:20)

Mavu ni nini katika biblia?(Kutoka 23:28, Kumb 7:20)

 Mavu ni nini?


 Mavu ni wadudu jamii ya nyuki, kwa jina maarufu ni NYIGU. Maumbile yao ni makubwa zaidi ya nyuki wa kawaida, Na mauvimu yao ni kama tu yale ya nyuki..

Wametajwa mara kadha wa kadha katika biblia, na hivi ni baadhi ya vifungu vinavyowaelezea;

Kutoka 23:27 “Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao.

28 NAMI NITAPELEKA MAVU MBELE YAKO, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako.

29 Sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmoja; nchi isiwe ukiwa, na wanyama wa bara wakaongezeka kukusumbua”.

Kumbukumbu 7:19 “uyakumbuke hayo majaribu makuu yaliyoyaona macho yako, na hizo ishara, na maajabu, na mkono wa nguvu, na mkono ulionyoka, aliokutolea nje Bwana, Mungu wako; ndivyo atakavyowafanya Bwana, Mungu wako, mataifa yote unaowaogopa.

20 Tena Bwana, Mungu wako, ATAMPELEKA MAVU KATI YAO, hata hao watakaosalia, hao wajifichao, waangamie mbele zako.

21 Usiingiwe na kicho kwa sababu yao; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu katikati yako, Mungu mkuu, mwenye utisho”.

 

Yoshua 24:11 “Nanyi mliuvuka Yordani, mkafika Yeriko; nao watu wa Yeriko wakapigana nanyi, Mwamori, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhiti, na Mgirgashi, na Mhivi, na Myebusi; nami nikawatia mikononi mwenu.

12 NIKATUMA MAVU MBELE YENU, waliowafukuza mbele yenu hao wafalme wawili wa Waamori, si kwa upanga wako, wala kwa upinde wako”.


 Katika mistari hiyo tunaona Mungu alivyowatumia wadudu hawa mavu kama silaha ya kuwafukuza maadui wa Israeli. Kufunua kuwa wapo mavu wa rohoni, ambao Mungu huwa anawatuma kuwafukuza maadui wa watakatifu duniani sasa.

Na mavu wenyewe ni malaika wa Bwana, na maadui wa watakatifu ni majeshi ya mapepo.. Mtakatifu yeyote rohoni huwa analindwa na kundi la malaika wa Bwana, hivyo shetani na mapepoo yake hawezi kumgusa kwa namna yoyote.

Lakini ikiwa mtu yupo nje ya Kristo, ibilisi ni lazima awe na mamlaka juu ya mwili wako. Na mapepo pia ni lazima yatajiamulia kufanya chochote yapendacho ndani yako, kwasababu hawapo mavu wa kukulinda wewe.

Kama hujaokoka na unahitaji kuokoka leo, basi fungua hapa kwa ajili ya sala ya Toba, >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Kumbuka Ni kwa Yesu tu unaweza kuwa salama pengine pote unapotea.

Bwana akubariki.

Tazama na tafsiri ya maneno mengine ya biblia chini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Neno beramu lina maana gani katika biblia?

Mkatale ni nini katika biblia? (Matendo 16:24)

MUNGU HANA MBARAKA MMOJA TU!..MWAMINI.

DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments