Sinagogi la Mahuru ni lipi? na lilimaanisha nini(Matendo 6:9)

Sinagogi la Mahuru ni lipi? na lilimaanisha nini(Matendo 6:9)

Neno hilo italisoma katika ile habari ya Stefano alipokuwa anatumiwa na Mungu kufanya ishara na maajabu yasiyokuwa ya kawaida katika kanisa lake.

Lakini baadhi ya wayahudi wa masinagogi mbali mbali walipoliona hilo wakamchukua kuja kujadiliana naye, na baada ya kuona kuwa wameshindwa waliingiwa wivu na kufanya mambo ambayo huwezi kudhani dhehebu la dini linaweza kufanya. Sasa moja ya sinagogi hilo lilikuwa ndio hilo lililoitwa Sinagogi la Mahuru; kulikuwa na mengine pia tusome.

Matendo 6:8 Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu.

9 Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;

10 lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye.

11 Hata wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu.

12 Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza.

13 Wakasimamisha mashahidi wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati;

Sasa ni kwanini liitwe kwa jina hilo?

Biblia haijaeleza chochote kuhusu chimbuko la sinagogi hilo mpaka wakajiita hivyo, lakini inaaminiwa na baadhi ya wanazuoni kuwa kulikuwa na kundi la wayahudi ambao walikuwa ni watumwa wa dola ya Ki-Rumi, Na baadaye wakafanywa kuwa huru, na ndipo hapo wakawa na sinagogi lao, wakaliita Sinagogi la mahuru. Yaani sinagogi la watu waliofanywa kuwa huru.

Hivyo hata kama chimbuko la jina hilo lingekuwa ni tofauti na hiyo, lakini bado jina lake ni nzuri, “Mahuru”.  Lakini shida inakuja ni pale ambapo mioyo yao haiakisi jina hilo.  Ni wazi kuwa watu hawa hawakuwekwa huru moyoni, kwasababu kama wangewekwa huru wasingekuwa na wivu, na wasingemzushia Stefano habari za uongo. Hiyo ni kuonyesha kuwa walikuwa ni watu walio mbali na wokovu kuliko hata watu wasiomjua Mungu kabisa.

Tunajifunza nini?

Hatushangai hata sasa kuona yapo makanisa mengi, na mikusanyiko mingi, yenye majina mazuri ya rohoni,  yenye misalaba mingi, yenye kila aina ya mapambo mazuri ya rohoni. Lakini  ndani yake wanazipinga nguvu za Roho Mtakatifu kama walivyompinga Stefano.

Biblia ilishatabiri  katika kitabu cha 1Timotheo 3 kuwa katika nyakati za mwisho watatokea watu wengi wa namna hiyo

2Timotheo 3:1 “Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.

2 Maana watu watakuwa……….

5 wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao”.

Unaona watakuwa wenye mfano wa utauwa lakini wanazikana Mungu za Mungu.

Huu si wakati wa kujivunia dhehebu au dini ndugu, ni wakati wa kujivunia Kristo ndani yako. Unaweza ukawa na dhehebu zuri kweli, kubwa kweli, lakini Mungu amelikataa, wewe litakufaidia nini? Tunapaswa tuutafute utakatifu kwa bidii kwasababu hatuwezi kumwona Mungu tusipokuwa nao(Waebr 12:14).

Tunapaswa tujichunge tusifanane na hawa wa sinagogi la mahuru ambao wana jina zuri lakini ni wapinga-Kristo ndani yao.

Bwana atusaidie.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)

Nini Maana ya Hosana?

Mataifa ni nini katika Biblia?

UFUNUO: Mlango wa 18

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
2 years ago

AMEN