Wengi tunafahamu habari za Yusufu, tunajua alikuwa ni mmoja wa watoto wa Yakobo aliyependwa sana na baba yake, Lakini baada ya kuota zile ndoto tu, ndugu zake walianza kumwonea wivu, na mwisho wa siku wakaamua kumuuza kama mtumwa kwa watu wa mataifa (Wamisri).
Na kama tunavyoisoma habari alipokuwa kule Misri Mungu alikuwa pamoja naye akamfanikisha katika mambo yote, akawa wa pili baada ya Farao mfalme wa Misri, kiasi cha kwamba hakuna mtu yoyote aliyeweza kufika kwa Farao bila kupitia kwanza kwake, Mali na vitu vyote vya Misri Farao alivikabidhisha kwa Yusufu,[Kumbuka Misri ndiyo iliyokuwa ngome yenye nguvu kuliko zote duniani kwa wakati ule], tunaweza kusema mfano leo hii taifa la Marekani lilivyo.