by Admin | 19 February 2024 08:46 pm02
Ifutayo ni mistari kadhaa ya biblia ihusuyo shukrani/ kushukuru.
Zaburi 9:1 “Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu”.
Zaburi 18:49 “Basi, Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako”
2Samweli 22:50 “Basi, Bwana, nitakushukuru kati ya mataifa, Nami nitaliimbia jina lako”.
Zaburi 30:12 “Ili utukufu wangu ukusifu, Wala usinyamaze. Ee Bwana, Mungu wangu, Nitakushukuru milele”
Zaburi 35:18 “Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa; Nitakusifu kati ya watu wengi”
Zaburi 52: 9 “Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako”
Zaburi 118: 21 “Nitakushukuru kwa maana umenijibu, Nawe umekuwa wokovu wangu”.
Zaburi 71:22 “Nami nitakushukuru kwa kinanda, Na kweli yako, Ee Mungu wangu. Nitakuimbia Wewe kwa kinubi, Ee Mtakatifu wa Israeli”.
Zaburi 119: 7 “Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo, Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako”
Zaburi 106:1 “Haleluya. Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele”.
Zaburi 28:7 “Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru”.
2Wakorintho 2:14 “Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu”.
Wakolosai 4:2 “Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani”.
Zaburi 100:4 “Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake”
Zaburi 107:7 “Akawaongoza kwa njia ya kunyoka, Wapate kwenda mpaka mji wa kukaa
8 Na wamshukuru Bwana, kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu”.
1Wakorintho 15:57 “Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo”.
Zaburi 95: 2 “Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi”.
Wakolosai 3:15 “Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani”.
Ufunuo 11:17 “wakisema, Tunakushukuru wewe, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa sababu umeutwaa uweza wako ulio mkuu, na kumiliki”
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU WATOTO.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU UPENDO.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/02/19/mistari-ya-biblia-kuhusu-shukrani/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.