Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?.

Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?.

Swali: Tunasoma katika Warumi 11:4, Mungu anasema kuwa “nimejisazia” lakini katika Wafalme tunasoma Mungu anasema “nitajisazia” kana kwamba ni kitendo kinachokuja mbeleni.. Je hapo mwandishi gani yupo sahihi?

Tusome:

Warumi 11:4 “Lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje? “NIMEJISAZIA WATU ELFU SABA” wasiopiga goti mbele ya Baali”.

1Wafalme 19:18 “Pamoja na hayo NITAJISAZIA katika Israeli watu elfu saba, kila goti lisilomwinamia Baali, na kila kinywa kisichombusu”.

Jibu: Ni muhimu kufahamu kuwa siku zote biblia haijichanganyi.. isipokuwa fahamu zetu ndizo zinazojichanganya..

Ili kuelewa vizuri labda tuanze kusoma juu kidogo katika mstari huo 1Wafalme 19 ila tuanzie juu kidogo..

1Wafalme 19:14 “Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana, Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu waiondoe.

15 Bwana akamwambia, Enenda, urudi njia ya jangwa la Dameski; ukifika, mtie mafuta Hazaeli awe mfalme wa Shamu.

16 Na Yehu mwana wa Nimshi mtie mafuta awe mfalme wa Israeli; na Elisha mwana wa Shafati wa Abel-Mehola mtie mafuta awe nabii mahali pako.

17 NA ITAKUWA ATAKAYEOKOKA NA UPANGA WA HAZAELI, YEHU ATAMWUA; NA ATAKAYEOKOKA NA UPANGA WA YEHU, ELISHA ATAMWUA.

18 Pamoja na hayo NITAJISAZIA katika Israeli watu elfu saba, kila goti lisilomwinamia “baali”, na kila kinywa kisichombusu”.

Katika Habari hiyo tunaona kuwa kumbe Mungu alikuwa amekusudia kuwaangamiza watu wote wanaobudu na kumsujudia baali. Lakini utaona wakati anataka kupitisha hukumu hiyo, akasema ATAJISAZIA yaani (atawabakisha) watu elfu 7 ambao hawamsujudii baali TANGU SASA.. yaani wakati wengine wote watakufa kwa upanga wa Hazaeli, Yehu au Elisha, Ambao utakuja baadaye.. hili kundi la watu elfu 7 lililopo sasa, litakuwa salama kwasababu halimsujudii Baali..

Kwahiyo Mwandishi wa Kitabu cha Warumi hajichanganyi na wa kitabu cha Wafalme, wote wapo sahihi

Ili tuelewe Zaidi labda tutafakari mfano huu.

“Umetenga magunia 10 ya makapi, na magunia 7 ya ngano.. na ukamwambia mtu mmoja kuwa “wiki ijayo utayachoma magunia yote ya makapi, na utabakiwa na magunia 7 ya ngano”. Na wakati wakati huo huo ukampa taarifa hiyo hiyo mtu mwingine kwa kusema “umejibakishia magunia 7 ya ngano ambayo hutayachoma moto wakati utakapoteketeza makapi”. Je! Kwa kauli hizo mbili utakuwa umejichanganya?.. jibu ni la!.. utakuwa umeelezea jambo lile lile ila kwa namna nyingine.. Ndicho Mwandishi wa kitabu cha Wafalme na Warumi walichoandika, kauli zao hazijakinzana bali zote zimelenga kitu kimoja na maana ile ile moja.

Lakini nini tunachoweza kujifunza hapo katika Habari hiyo?.. Tunachoweza kujifunza ni kuwa Mungu analitimiza neno lake na wala hasemi uongo.. aliwaondoa wote wanaoabudu baali na kuwasaza watu elfu 7 kama alivyosema..wasiopigia goti baali.

Na zama hizi za mwisho, unabii unasema Kristo atarudi kwaajili ya hukumu ya ulimwengu kwa wote wanaotenda maovu. Na neno lake kama alivyosema litatimia. Hivyo ni wajibu wetu sisi kusimama katika Imani kama tumeshampokea Yesu, na kama bado ni wakati wa kumpokea na kuiamini injili yake.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

Baali alikuwa nani?

Je kauli ya Bwana Yesu inajichanganya? Katika Yohana 8:14 na Yohana 5:31?

Mahali pa juu palikuwa ni wapi kama tunavyosoma katika biblia?

Ni kiumbe gani kinachosujudiwa hapo katika Warumi 1:25?

Ahera ni wapi? Kama tunavyosoma katika biblia.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Getrude Charles
Getrude Charles
1 year ago

Amina barikiwa Sana Mtumishi wa Bwana Wetu Yesu Kristo.