TUKIO LA MUSA NA ELIYA KUMTOKEA BWANA, LIMEBEBA UJUMBE GANI?

TUKIO LA MUSA NA ELIYA KUMTOKEA BWANA, LIMEBEBA UJUMBE GANI?

Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze maneno ya Uzima wa Mungu wetu..

Yapo maswali kadhaa ambayo tunaweza kujiuliza, juu ya tukio la Bwana Yesu kutokewa na Musa na Eliya siku ile alipopanda mlimani kuomba pamoja na wale wanafunzi wake watatu (Petro, Yohana na Yakobo)..

Na maswali yenyewe ni haya..

 1) Iweje Bwana Yesu atokewe na Musa ambaye tayari alishakufa miaka mingi?, na Zaidi ya yote maandiko yanasema alizikwa, tena na Mungu mwenyewe?..

2) Kwanini Musa na Eliya wamtokee?.. kulikuwa na umuhimu gani wa wao kumtokea Bwana?

Sasa ili tupate majibu ya maswali hayo vizuri, Labda tusome habari yenyewe kwa ufupi kisha tuendelee

Luka 9:28 “Baada ya maneno hayo yapata siku nane, aliwatwaa Petro na Yohana na Yakobo, akapanda mlimani ili kuomba.

29 Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimeta-meta.

30 Na tazama, watu wawili walikuwa wakizungumza naye, nao ni MUSA NA ELIYA;

31 walioonekana katika utukufu, WAKANENA HABARI ZA KUFARIKI KWAKE ATAKAKOTIMIZA YERUSALEMU”

Kiini cha majibu ya maswali yetu tutakipata katika huu mstari wa 31.. “walioonekana katika utukufu, WAKANENA HABARI ZA KUFARIKI KWAKE ATAKAKOTIMIZA YERUSALEMU”

Kumbe Sababu ya Musa na Eliya kumtokea Bwana, ilikuwa ni kuzungumza kuhusu Kufa kwake Bwana Yesu, ambako atakutimiza Yerusalemu.

Sasa swali linakuja?, je ni kwamba Bwana Yesu alikuwa hajui kwamba atakwenda kufa mpaka atokewe na watu hao wawili, wamweleze kuhusu kufa kwake?.. Jibu ni la!.. alikuwa anajua, lakini zipo siri nyingine zihusuzo kufa kwake na kufufuka kwake na kupaa kwake, ambazo hizo Baba alimfunulia siku hiyo kupitia manabii hao wawili.

Kumbuka kabla ya Kristo kufa, roho za watakatifu zilikuwa chini, na shetani alikuwa na uwezo wa kuzileta juu, kama wewe ni msomaji wa biblia utakumbuka lile tukio la Samweli kuletwa juu ya yule mwanamke mwenye pepo la utambuzi, na baada ya kuletwa juu, Samweli aliweza kutoa unabii wa mambo yajayo, ijapokuwa alikuwa ameshakufa na kuzikwa, kwani tunasoma, alimtolewa Unabii Mfalme Sauli kuhusu KUFA KWAKWE, AMBAKO KUTAKWENDA KUTIMIA KIPINDI SI KIREFU KUTOKA PALE. Unaweza kusoma Habari hiyo kwa urefu katika kitabu cha 1Samweli 28:1-19.

Sasa Biblia haijaeleza Musa alikuwa anamweleza nini Bwana Yesu, lakini tunajua kabisa ni kuhusu Habari za kufunguliwa kwao wafu, na kwamba Bwana Yesu atakwenda kusulibiwa na kushuka sehemu ya wafu wao (akina Musa na wengine walipo na kuwaweka huru, na kwamba siku ya tatu atafufuka).

Kwahiyo kumbe kabla ya Bwana Yesu kufa, Wafu waliendelea kuishi, na pia iliwezekana kuwaleta baadhi yao juu na kutoa unabii, kwa njia yoyote ile!..

Kwasababu hiyo basi tumeshapata jibu ni kwanini MUSA, aliletwa juu na Mungu, ili kutoa unabii (Habari za kufa kwake Bwana Yesu, ijapokuwa Musa alikuwa ameshakufa kitambo na kuzikwa)…Ni kama tu vile, Nabii Samweli alivyoletwa juu na yule mwanamke mwenye pepo la utambuzi. (Kumbuka jambo hilo liliwezekana tu kipindi kabla ya Bwana Yesu kufa, lakini baada ya Bwana Yesu kufa na kufufuka, hakuna mchawi yeyote anayeweza kumleta juu mtu aliyekufa, kwasababu Kristo alizichukua funguo za Mauti na kuzimu).

Hapo tumepata jibu kuhusu Musa, sasa vipi kuhusu ELIYA?

Tunajua kabisa Eliya hakufa, bali alipaa..Maana yake Eliya anayajua yaliyo ya Mbinguni.. kama Nabii, Bwana alimtoa huko na kuja kumpasha Habari Bwana Yesu, kuhusu kupaa kwake, na enzi na mamlaka zinazomngojea Mbinguni (labda na siku hiyo alimpa na tarehe ya kupaa kwake, hatujui).

Kwasababu ijapokuwa Eliya alikuwa amepaa mbinguni, lakini bado alikuwa ni Nabii. Kwahiyo ujio wa Eliya ulikuwa ni wa muhimu sana kwa Bwana, kupata taarifa kuhusu kupaa kwake.

Kwahiyo kwaufupi ni kwamba Mungu aliwatumia manabii hawa wawili kama Manabii wa Ushahidi. Na Ushahidi huo ni wa KUFA kupitia Musa, na Kupaa kupitia ELIYA. Kwasababu Kristo naye atakufa kama Musa aliye nabii mkuu, na vile vile atapaa mbinguni kama ELIYA.

Kwahiyo baada ya tukio lile, Bwana Yesu alipokea Ufunuo mkuu kuhusu Mauti yake na kufufuka kwake, na kupaa kwake.. Zaidi sana na kurudi kwake kutakavyokuwa..ndio maana tunaona pia Uso wake uling’aa kama jua, kuashiria siku ya kurudi kwake kutakavyokuwa.

Na wakati ulipofika kweli Bwana Yesu, alikufa, akafufuka, na akapaa mbinguni.. imesalia hatua moja tu!.. nayo ni KURUDI KWAKE KUTUCHUKUA!..

Je! Umejiandaaje?.. Kama Nabii hizo mbili za kufa na kufufuka kwake na kupaa kwake zilitimia.. Basi hata kurudi kwake kutatimia. Na tupo katika majira ya kurudi kwake, dalili zote zimeshaonekana, muda wowote mambo yanakwisha, Kristo anakuja kuwachukua watakatifu wake, na kitakachokuwa kimesalia kwa wale watakaobaki ni majuto na dhiki kuu.

Je umejiandaaje? Je umemwamini Yesu na kutubu dhambi zako? Je umebatizwa katika ubatizo sahihi?…kama bado unangoja nini?.. Ukiikataa leo injili siku hiyo hutakuwa na la kujitetea. Mpokee Yesu leo, na ukabatizwe na kujazwa Roho Mtakatifu.

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312


Mada Nyinginezo:

Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?

Je Eliya aliandika waraka baada ya kupaa mbinguni?

Mtu wa kwanza kufa alikuwa nani?

Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki;

Ngome ni nini?  Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Prisca komba
Prisca komba
2 years ago

Mwal ninaswali mi huwa naota ndoto za watu waliokufa hii inamaanish nini