Ni kiumbe gani kinachosujudiwa hapo katika Warumi 1:25?

Ni kiumbe gani kinachosujudiwa hapo katika Warumi 1:25?

Tusome,

Warumi 1:25 “Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina”.

Kiumbe ni kitu chochote chenye uhai kilichoumbwa na Mungu. Katika dunia viumbe hai ni Wanadamu, Wanyama na mimea.

Kwahiyo maandiko hapo yaliposema kuwa “wameibadili kweli ya Mungu kuwa uongo na kukisujudia kiumbe inamaanisha ni kiumbe chochote kile, na si kimoja maalum!..kinaweza kuwa mtu au mti, au mnyama Fulani. Maeneo ya Korea kaskazini watu wanaabudu MTU kama Mungu, maeneo ya India watu wanaabudu Nyoka na Ng’ombe, Maeneo ya Marekani ya kusini na watu wanaabudu Chui na maeneo ya Afrika watu wanaabudu Miti n.k. Hawa wote wanaabudu viumbe vilivyoumbwa na Mungu, jambo ambalo ni machukizo makubwa mbele za Bwana.

Na mbaya zaidi wengi wanaofanya hivyo maandiko yanasema wanafanya hivyo kwa kujua kabisa! Kwamba vitu hivyo si Mungu, na dhamiri zao zikiwashuhudia, lakini hawataki kubadilika.

Warumi 1:20 “Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru;

21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.

22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;

23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo.

24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.

25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina”.

Je na wewe unaabudu watu? Kumfanya mtu tegemeo lako asilimia mia hakuna tofauti na kumwabudu!, kumwogopa mtu na kumfanya kinga yako kiasi kwamba hata anaweza kukuamulia siku ya kuabudu na ukatii huko hakuna tofauti na kumwabudu (Unakiabudu kiumbe), kumtumikia mtu mpaka unakosa muda wa kwenda kumfanyia Mungu wako ibada angalau hata mara moja kwa wiki, huyo mtu ni mungu wako.

Yeremia 17:5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.

6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.

7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.

 8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda”.

Je Bwana ni tegemeo lako au viumbe?

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3

INJILI YA MANENO LAINI ITAKUGHARIMU.

 Je kualikwa kwenye sherehe za watu ambao si wakristo ni dhambi?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments