Vitimvi ni nini kibiblia?

Vitimvi ni nini kibiblia?

Vitimvi ni mipango inayopangwa kwa siri na  kikundi cha watu ili kufanya uasi juu ya mtu au watu.

Katika biblia Mitume wa Bwana Yesu walifanyiwa vitimvi vingi sana vya kuwaangamiza, mfano wa hao utaona ni Mtume Paulo..

Matendo 20:2 “Naye akiisha kupita pande zile na kuwafariji kwa maneno mengi, akafika Uyunani.

3 Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, na Wayahudi KUMFANYIA VITIMVI, alipotaka kwenda Shamu kwa njia ya bahari; basi akaazimu kurejea kwa njia ya Makedonia”.

Na pia utaona kuna wakati Paulo alipokuwa amefungwa kule Yerusalemu, baadhi ya wayahudi kama 40 hivi walijifunga kiapo kwamba hawatakula wala kunywa hata watakapomwua Paulo (Matendo 23:12). Sasa mipango hiyo ndiyo inayoitwa vitimvi!

Matendo 23:27 “Mtu huyu alikamatwa na Wayahudi, wakawa karibu kumwua, ndipo nikaenda pamoja na kikosi cha askari nikamwokoa, nilipopata habari ya kuwa yeye ni Mrumi.

28 Nami nikitaka kulijua lile neno walilomshitakia, nikamtelemsha nikamweka mbele ya baraza;

29 nikaona kwamba ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sheria yao, wala hakushitakiwa neno lo lote la kustahili kuuawa wala kufungwa.

30 Hata nilipopewa habari kwamba PATAKUWA NA VITIMVI JUU YA MTU HUYU, mara nikampeleka kwako, nikawaagiza na wale waliomshitaki, wanene habari zake mbele yako. Wasalamu”.

Na kama wakristo wa kanisa la kwanza walipitia Vitimvi, kutokana na Imani yao, kadhalika na wakristo wa kweli wa siku hizi za mwisho ni lazima wapitie vitimvi kama wa kanisa la kwanza, kwasababu Roho ni yule yule, Bwana na yule yule hajabadilika.

Ni lazima upitie maudhi kwaajili ya Imani yako, ni lazima upitie kuhuzunishwa, ni lazima upangiwe visa, ni lazima wakati mwingine utenge au uchukiwe au hata kupigwa na kufungwa!. Hizo ndizo chapa za Yesu ambazo tunazopaswa kuzichukua..

Wagalatia 6:17 “Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu”.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Dini ni nini, na Imani ya kweli ni ipi?

YEYE ALIYEUWASHA HUO MOTO LAZIMA ATALIPA.

MWISHO WA MAVUNO, NI MWISHO WA DUNIA.

Kuhusuru ni nini kibiblia? (Luka 19:43)

Neno “Uchungu wa mauti” lina maana gani kibiblia?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments