Kuhusuru ni nini kibiblia? (Luka 19:43)

Kuhusuru ni nini kibiblia? (Luka 19:43)

Kuhusuru ni kuzinga kitu, pande zote  kisiwe na upenyo wa kutoroka au kupita.

 Mbinu hii yalitumia majeshi ya zamani katika vita..kabla ya kwenda kupigana na adui zao waliwazingira kwanza kuhakikisha hakuna upenyo wowote wa wao kutoka..na hiyo inaweza kuchukua hata miezi kadhaa.. Mpaka pale chakula kitakapoisha ndani..Sasa kwa hali kama hiyo maudui, wao wenyewe tu  watalazimika aidha kuiomba amani..au watoke wapigane..na kwa kawaida huwezi pigana na adui yako ukiwa na njaa.. Utapigwa tu.

Neno hili utalisoma sehemu nyingi sana katika biblia..kwamfano hivi ni baadhi ya vifungu ambavyo utakutana na Neno hilo..

2 Wafalme 6:24-25

[24]Ikawa baada ya hayo, Ben-hadadi mfalme wa Shamu akakusanya majeshi yake yote, akakwea akauhusuru Samaria.

[25]Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama, wakauhusuru, hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya fedha.

1 Samweli 23:8

[8]Basi Sauli akawaita watu wote waende vitani, ili waishukie Keila, na kumhusuru Daudi na watu wake.

1 Wafalme 8:37

[37]Ikiwa nchi imeingia njaa, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewahusuru katika nchi ya miji yao; au ukiwapo msiba wo wote, au uele wo wote;

Luka 19:43

[43]Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote;

Soma pia Kumbukumbu 20:12, 19, 2Wafalme 24:11, Isaya 29:4

Ni picha gani tunaipata katika Roho?

Ndivyo anavyofanya shetani sasa katika roho..akitaka kuwaangusha watu hususani wale ambao anajua ni ngumu kuwaangusha..atakimbilia kuhusuru sehemu mbalimbali ambazo anajua wanazitegemea kuendeshea maisha yao, halafu baada ya hapo akishafanikiwa anamlazimisha ufanye dhambi fulani..

Labda anakunyima kazi..halafu anakuambia ukitaka hii kazi zini na mimi..ukiona hivyo usidhubutu..bali mpinge, kabisa kabisa..

Alipomwona Bwana Yesu anayo njaa kule jangwani..ndipo akamletea mkate..Lakini Bwana hakukubali ushawishi wake..akamwambia mtu hataishi kwa mkate, bali kwa kila Neno linalotoka katika kinywa cha Bwana.

Na wewe mwambie shetani hutaishi kwa hilo tu analoliwazia..bali kwa kila Neno linalotoka katika kinywa cha Bwana. Mungu atakupasulia mlango kwingine..

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Maji ya Zamzam yapo kibiblia?

Mintarafu ni nini?

Wanefili walikuwa ni watu gani?

HISIA YA MUNGU ILIYO MBAYA KULIKO ZOTE.

KUWA RAFIKI WA DUNIA NI KUWA ADUI WA MUNGU.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments