Maji ya Zamzam yapo kibiblia?

Maji ya Zamzam yapo kibiblia?

Naomba kujua kama Maji ya Zamzam yapo kibiblia na kama tunaweza kuyanunua na kutumia.

Jina kuu la Mwokozi wetu Yesu libarikiwe.

Maji ya Zamzam ni maji yanayoaminika kutoka katika kisima kimoja kilichopo Saudi Arabia kujulikanacho kwa jina hilo Zamzam.

Baadhi ya waarabu wanaamini kisima hicho ndicho kile kisima ambacho Hajiri aliyekuwa kijakazi wa Sara, mke wa Ibrahimua alioneshwa na yule malaika katika Mwanzo 21.

Mwanzo 21:17 “Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko.

18 Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.

19 Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.

20 Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.

21 Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.

Lakini je! Kuna ukweli katika hayo?

Jibu ni la! Hakuna ukweli katika hayo, Kisima Hajiri alichooneshwa na Malaika hakikuwepo katika nchi ya Saudia, bali katika jagwa la Parani, ambalo lipo maeneo karibia na jangwa la Sinai, mbali kabisa na Saudia.

Kadhalika biblia haijarekodi popote kuwa kisima hicho kilikuwa kinaitwa Zamzam, wala haijarekodi kuwa baada ya hapo maji yake yalikuwa ni matakatifu. Kilikuwa ni kisima tu kama kisima kingine ambacho Mungu alikitumia kumwokoa Ishmaeli pamoja na mamaye, hakikuwa cha kimiujiza, wala hakikubeba nguvu zozote za kiungu baada ya hapo.

Imekuwa ni kawaida watu kufanya ziara sehemu ambazo kulionekana uweza wa kiMungu.

Kwamfano utaona leo hii watu wanakwenda mlima Sinai, na kwenda kuadhimisha au kufanya ibada, mahali pale Musa alipoona kijiti kikiteketea, vile vile utaona wengine leo hii wanakwenda kuchukua maji ya mto Yordani, mahali ambapo Bwana Yesu alibatiziwa na Yohana Mbatizaji, wengine watachukua udogo kutoka Yerusalemu .nk. wakiamini kuwa vitu hivyo vina uungu wa kipekee na wakitofauti.

Pasipo kujua kuwa wamedanganyika, yule Adui shetani kawapofusha macho yao, wakifikiri wanamwabudu Mungu kupitia vitu hivyo kama wanamwabudu yeye.

Bwana Yesu alisema maneno haya.

Yohana 4:21 “Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.

22 Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.

23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.

24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

Umeona?. Nyakati hizi Mungu haabudiwi tena katika milima, wala katika udongo wala katika maji..bali anaabudiwa katika Roho na Kweli..

Hivyo mtu anayetumia kitu chochote kwa imani kuwa kinamsogeza kwa Mungu zaidi, au kinampatia uponyaji..basi mtu huyo kadanganyika na uongo wa adui.

Kama unapitia ugonjwa au tatizo, tumepewa jina la Yesu, ambalo hilo tukitamka mara moja tu kwa Imani, kazi zote za shetani zinavunjika.

Je! Umemwamini na kumpokea Yesu, wewe unayesoma ujumbe huu?. Kama bado unasubiri nini?..mpokee leo na akuoshe dhambi zako nawe utapata uzima wa milele.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

Kisima cha joka na lango la jaa ni nini?(Nehemia 2:13)

“Shinikizo” ni nini kibiblia, Na maana yake rohoni ni ipi?

BIRIKA LA SILOAMU.

Je! Ni sahihi mtu kubatizwa kwenye maji ya KISIMANI?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments