KWANINI MTINI KATIKATI YA MIZABIBU?

KWANINI MTINI KATIKATI YA MIZABIBU?

Kuna baadhi ya watu Mungu anawapanda katika kanisa, kwa namna ya kitofauti na kipekee sana..

Na pengine wenyewe hawalijui hilo..hivyo wanaishi maisha ya kimaficho ficho tu..au ya juu juu tu, kwa kisingizio kuwa wao si kama wengine.. wakidhani kuwa Kristo, amewaweka hapo bure, kwasababu hiyo..

Ulishawahi kuitafakari vizuri hii habari..

Luka 13:6-9
[6]Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate.
[7]Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu?
[8]Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi;
[9]nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate.

Fikiria hilo ni shamba la Mizabibu..pengine ekari elfu moja, limeandaliwa mahususi kwa ajili ya kutoa zabibu za kibishara..lakini mwenye shamba tunaona bado katikati ya shamba hilo kubwa alipanda mti mwingine wa matunda ujulikanao kama “mtini”..

Kumbuka lengo lake halikuwa apate matunda ya biashara kutoka katika mti huo..bali pengine ya kula tu, na ndio maana mtini wenyewe ulikuwa ni mmoja tu. Lakini bado hakutaka ukae bila matunda..akaupa muda ili uzae..

Kuna watu Mungu kawapanda katika kanisa lake, ambao wanaweza kuonekana ni tofauti sana na watakatifu wengine pengine kilugha, labda hawajui kiswahili vizuri, au kimazingira, labda wapo mbali, au kinafasi, ni viongozi wakubwa n.k.na hivyo hawawezi moja kwa moja kutumika kama hawa wengine..kwa vikwazo hivyo.

Lakini wengi wa hawa huwa wanaishi maisha ya kujificha, wakidhani pengine sio sehemu ya kanisa la Kristo.

Nataka nikuambie, vyovyote vile ujionavyo..Kristo anatazamia matunda kutoka kwako. Anataka aone ukristo wako ukiangaza kwa wengine..anataka kuona unafanya kitu kwa ajili ya ufalme wa mbinguni..anataka kuona shamba lake alilokuweka wewe ndani yake pamoja na hao wengine hulikalii bure…na wewe pia kwa nafasi yako uhakikishe unazaa matunda..

Hizi ni siku za mwisho ndugu yangu..Kristo anasema Naja upesi, na ujira wangu, upo mkononi mwangu kumlipa kila mtu..sawasawa na kazi yake ilivyo..

Ufunuo wa Yohana 22:12
[12]Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

Utalipwa nini siku ile..ikiwa miaka nenda rudi, wewe ni msikiaji tu wa injili, miaka nenda rudi upo tu mafichoni, hutaki ijulikane..jiulize Ni nini umemfanyia Bwana basi..mpaka akupe ufalme siku ile?

Bwana atutie nguvu, tutambue kuwa sote tupo shambani mwake..na sio jukumu la askofu fulani au shemasi. Na kwamba Bwana atamvumilia mtakatifu yoyote katika shamba lake asiyemzalia matunda.

Tafadhali shea na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments