Nini maana ya kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua (Mithali 13:12)?.

Nini maana ya kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua (Mithali 13:12)?.

Jibu: Tusome,

Maandiko yanasema..

Mithali 13:12 “Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima”.

Ni kawaida siku zote kuugua pale unapokuwa katika hali ya kusubiria jambo kwa muda mrefu.

Mtu anayemngojea mwenzake aliyekawia kwa dakika 10, yule anayemngoja ataona kakawia kama lisaa hivi, ingawa ni dakika 10 tu zimepia.

Hiyo ni kwasababu, ya kile kinachotarajiwa kimekawia, moyo wa mtu huwa unaugua.
Lakini maandiko yanazidi kusema kuwa mtu anapopata haja yake ni Mti wa Uzima.
Sasa swali hapo ni kwanini mtu anapopata haja yake anafanishwa na mti wa Uzima.

Siku zote miti unafananishwa na watu.

Marko 8:24 “Akatazama juu, akasema, Naona watu kama miti, inakwenda”.

Pia Bwana sehemu nyingine alisema “mti hutambulika kwa matunda yake”..maana yake watu wanafananishwa na miti.

Luka 6:44 “kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu.

45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake”.

Maana yake ni kwamba, kama mtu ndani yake ni mwema, ni mtakatifu, ana uzima..Basi mtu huyo ni MTI WA UZIMA.

Matunda atakayoyatoa yatawapa wengine uzima.

Sasa ni kwa namna gani, mtu anayepata haja yake anafananishwa na mti wa uzima?.

Ni kwasababu ya ile furaha atakayoipata, itawafaidia wengi, ni kwasababu ya ile neema atakayoiachia baada ya pale.

Siku zote watazame watu waliofanikiwa kupata jambo fulani,waliokuwa wanalitafuta utaona wanakuwa wakarimu ghafla, utaona wanatoa maneno mazuri mdomoni mwao.

Mithali 15:4 “Ulimi safi ni mti wa uzima;
Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo”.

Lakini kinyume chake, mtu ambaye hajapata anachokitafuta anakuwa mkali. Huwezi kutegemea kupata chochote chema kutoka kwake, hiyo ni kwasababu bado hajakipata anachokitafuta.

Hivyo hizo ni hekima tu ambazo Sulemani aliziona na kuzitoa kwa watu.

Na sisi tunapompokea Yesu maishani, Roho Mtakatifu anatupa haja ya mioyo yetu, anakata kiu yote, hivyo tunajikuta nasi pia tunakuwa wazuri ghafla, tunatoa matunda ya Uzima, hivyo tunakuwa Mti wa Uzima kwa wengine.

Ndivyo maandiko yanavyosema..

Mithali 3:13 “Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.

14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.

15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.

16 Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.

17 Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani.

18 Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye”.

Je na wewe ni Mti wa Uzima?, Kwa wengine?. Au ni mti wa Mauti?.

Ni HAJA moja tu maishani itakayokufanya uwe Mti wa uzima duniani. Na hiyo ni kumwamini Yesu na kupokea Roho Mtakatifu.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?

Nini maana ya ‘Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu’ ?

JINSI YA KUEPUKA KUUMIZWA MOYO KUSIKOKUWA NA SABABU.

HATARI YA KUTOKUITAFAKARI BIBLIA VIZURI?

MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments