KUWA RAFIKI WA DUNIA NI KUWA ADUI WA MUNGU.

KUWA RAFIKI WA DUNIA NI KUWA ADUI WA MUNGU.

Yakobo 4:4  “Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu”.

Shalom.

Kitendo tu cha kuipenda dunia, na mambo yake, tayari umefanyika kuwa adui wa Mungu. Mtu akipenda anasa, akipenda uzinzi, akipenda fashion, akipenda starehe za ulimwengu huu, kama miziki, ushabiki wa mipira, ulevi, ukahaba, wizi, utapeli, tamaa za fedha, tamaa mbaya ya vitu vya kiulimwengu vinavyopita kama magari, nyumba, kiasi kwamba unaweza kufanya chochote ili uvipate n.k Mtu huyo tayari kashafanyika kuwa Adui wa Mungu.

1Yohana 2:15  “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

16  Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na KIBURI CHA UZIMA, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.

17  Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”

Kiburi cha Uzima, kinachozungumziwa hapo ni ile hali ya mtu kujiona hawezi kuambiwa lolote kutokana na aidha Elimu aliyonayo au mali alizonazo. Mtu yeyote ambaye anaidharau injili na Mungu, kutokana na kitu Fulani cha kidunia alichokipata, ambacho kinaheshimika katika dunia, mtu huyo ana kiburi cha uzima. Na mtu yeyote mwenye kiburi cha uzima tayari ni adui wa Mungu.

Biblia inatuambia dunia inapita, na tamaa zake zote.. Na tena Bwana Yesu alituambia katika Marko..

Marko 8:36  “Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?

37  Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?”

Hebu jiulize umepata kila kitu leo hii, halafu unakufa unakwenda motoni?, Umejifurahisha na kila starehe halafu unakufa ghafla, na kule Bwana anakuweka katika kundi la maadui zake?. Ni heri tukakosa kila kitu leo, lakini kule tukapate kila kitu..

Jihadhari na kiburi cha Uzima, BelshazaMfalme wa Babeli alikuwa nacho, hata ikafikia hatua ya kumdharau Mungu wa mbingu na nchi, kwa kwenda kuvitumia vyombo vitakatifu kushiriki anasa zake pamoja na wake zake, lakini siku ile kilitokea kiganja kikamwandikia MENE, MENE, TEKELI na PERESI. Na ufalme wake wote haukumsaidia, kwasababu usiku ule ule alioona kile kiganja alikufa.

Yule Tajiri aliyekuwa na Lazaro katika Luka 16, Alikuwa na kiburi cha Uzima, kiasi kwamba aliweza kumlisha mtumishi wa Mungu kwa makombo yaliyoanguka katika meza yake, lakini alipokufa alitamani aburudishe ulimi wake kwa tone moja la maji, alipokuwa katika yale mateso kuzimu. Na kiburi chake chote alichokuwa nacho duniani, hakikumsaidia kitu.

Malkia Yezebeli alikuwa na kiburi cha uzima, mpaka kufikia kuua manabii wa Mungu, na zaidi ya yote alikuwa mchawi, na ndiye mwanamke pekee katika Israeli,  aliyekuwa anajipaka uwanja na kujipaka rangi uso. Kwa kiburi chake chote hicho, lakini fahari yake iliondoka katika siku moja, Mbwa walipomla nyama yake.

Hayo yote yaliwatokea hao na kuandikwa ili sisi tusirudie makosa yaliyofanyika na tumwogope Mungu, kama Neno la Mungu linavyosema…

1Wakorintho  10:11  “Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani”.

Swali: Je! Wewe ni Rafiki wa Mungu?.. au Adui wa Mungu?… Kama bado unaupenda ulevi, uasherati, fashion, anasa, wizi, matusi, ni mshabiki wa mipira na mambo mengine yote ya uliwemwengu huu, ni Adui wa Mungu bila hata kutamka kwa kinywa chako.  Kama hujampokea Kristo leo hii ni siku yako, hapo ulipo tubu! Kwa kumaanisha kuacha dhambi zako, na pia tafuta ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa Jina la Yesu, kulingana na Matendo 2:38, na Roho Mtakatifu atakufanya rafiki wake wa kweli na wa kudumu.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengi


Mada Nyinginezo:

MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

MATARAJIO YA KILA MWANADAMU DUNIANI NI YAPI?

LAKINI NINYI, NDUGU, MSIKATE TAMAA KATIKA KUTENDA MEMA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Thadeo
Thadeo
2 years ago

JAMAN DAH MUNGU ATUSAIDIE