Kwa jina lake Ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.

Kwa jina lake Ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.

SWALI: Mstari huu unamaanisha nini?

Waefeso 3:14 “Kwa hiyo nampigia Baba magoti,

15 ambaye kwa jina lake UBABA WOTE WA MBINGUNI NA WA DUNIANI UNAITWA”,


JIBU: Mungu ni Baba wa kila kitu, Baba wa kilivyo mbinguni, na vilevile  Baba wa vilivyo duniani. Na kama tunavyojua jukumu la Baba ni kuhakikisha anaihudumia familia yake vizuri, anaitunza, anailisha, anaivisha, anaiburudisha, vivyo hivyo Mungu wetu ni Baba wa viumbe vyake vyote, vilivyo juu mbinguni (yaani malaika zake wote), na vilivyo chini duniani (Wanadamu wote). Anavihudumia na kuvitosheleza vyote kulingana na mahitaji yao. Kwasababu yeye ndiye aliyeumba kila kitu, Na ndiye mpaji wa wote.

Wakolosai 1:16 “Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake”.

Na ndio maana mtume Paulo anasema Anampigia magoti yeye, kwasababu uweza wake wa ubaba haupo tu, hapa duniani, bali pia upo kule mbinguni. Na utaendelea kuwa hivyo milele na milele. Hivyo Baba kama huyo ndiye anayestahili kupigiwa magoti.

Wafilipi 2:9 “Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;

10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;

Na sisi pia tuliookoka tunapaswa tukumbuke kuwa tunaye BABA MKUU juu mbinguni. Na kwamba anaowezo wa kututimizia mahitaji yetu yote ya mwilini na rohoni. Lakini ni sharti kwanza tujue kuenenda katika kanuni zake, ili afanyike kwetu Baba kweli kweli. Na kanuni yenyewe ni ile ile, ya kuutafuta kwanza ufalme wake na haki yake, ndipo hayo mengine atatuzidishia kirahisi.

Bwana Yesu alisema..

Mathayo 6:26 “Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? 27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?

28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti

29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.

30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?

31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?

32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.

33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa”.

Ubarikiwe.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!

Mbari ni nini kibiblia?

Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki;

JE NI KWELI SAMAKI NGUVA YUPO?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
2 years ago

AMEN barikiwa sana kaka nimejifunza kitu MUNGU wa mbinguni Akubariki sana🙏