Ni kwanini tunambariki Mungu? Je! Mungu huwa anabarikiwa?

Ni kwanini tunambariki Mungu? Je! Mungu huwa anabarikiwa?

SWALI: Tafadhali naomba ufafanuzi wa jambo hili, kibiblia tunaambiwa kwamba mkubwa atambariki mdogo. Sasa kuna baadhi ya wakristo waliookoka wanapokuwa katika maombi, wamezoea kusema “Nakubariki Mungu wa mbingu kwa wema wako.”. Je ni sahihi kumwambia Mungu wetu hivyo?


JIBU: Neno kubariki linamaana Zaidi ya ile ya kumuombea mtu mafanikio, ambayo tumeizoea,  kwamba mkubwa anambariki mdogo, lengo  likiwa ni ili aje kupokea mema kutoka kwa Mungu baadaye.

Bali Neno kubariki kibiblia linamaanisha pia ya kutukuza, au kuheshimisha jambo,kitu au jina. kwamba limestahili kupokea sifa zote njema..

Hivyo mkristo anaposema nalibariki jina la Bwana. Hana maana kuwa analiombea mafanikio kana kwamba linategemea baraka kutoka kwake ili lifanikiwe pasipo hizo haliwezi kufanikiwa, hapana.

Bali linamaana  ya juu Zaidi, yaani “analipa heshima zake zote kwamba limestahili heri”

Katika biblia utaona Ayubu alilibariki jina la Mungu wakati ule alipokuwa anapitia matatizo, alisema maneno hayo…

Ayubu 1:21 “akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; JINA LA BWANA NA LIBARIKIWE”.

Unaona? vilevile malaika mbinguni, usiku na mchana wanalibariki jina lake.

Ufunuo 5:11 “Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,

12 wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu NA BARAKA”.

13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, BARAKA NA HESHIMA na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.

Soma pia.. Ufunuo 7:12.

Hivyo, na sisi tunapolibariki jina la Bwana, ni kwamba tunaonyesha kuwa tunathamini haki  yote na uzima, na amani, na furaha,  na upendo, unaotoka katika jina hilo. Ni lugha nzuri Zaidi tuliyonayo  ya kumtukuza Bwana , na hakuna shida yoyote kusema hivyo.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

Mafundisho

UFUNUO: Mlango wa 7 & 11

Nini maana ya “Siku moja nyuani mwa Bwana ni bora kuliko siku elfu”?

Maswali na Majibu

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments