SWALI: Je! kuna mchango wowote sisi tunaweza kuuweka ili tupate wokovu wetu? Na kama sio kwanini basi maandiko yanasema, ufalme wa mbinguni unapatikana kwa nguvu nao wenye nguvu ndio wanaouteka (Mathayo 11:12)?
JIBU: Kuhusu mchango wetu katika Neema ya wokovu, maandiko yapo wazi ni kuwa HAUPO.
Waefeso 2:8 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu”.
Waefeso 2:8 “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu”.
Lakini swali linakuja kama ni hivyo basi kwanini, maandiko yanasema..
Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka”.
Jibu ni kuwa adui yetu yupo naye ni shetani, huyo ndiye anayeifanya njia ya wokovu ionekane ni ya jitahada kidogo. Hivyo inahitaji nguvu ya ziada kuiona na vilevile kuiendea kwasababu ni nyembamba sana na imesonga.
Mathayo 7:13 “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. 14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache”.
Mathayo 7:13 “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache”.
Kwamfano leo hii, shetani anaweza kukuzuia usimfanyie Kristo ibada, kisa tu wazazi wako wamekataa, au kazi yako imekusonga, au mazingira si rafiki hakuna mtu atakayekuelewa, unadhani ukiiruhusu hiyo hali, ataurithi uzima wa milele?. Haiwezekani, inahitaji kulazimisha mambo, kutumia nguvu, kukubali kuchukiwa, au wakati mwingine kupoteza hata kile ulichonacho, ili mradi tu usiopoteze wokovu wako.
Hapo ndipo neno ufalme wa mbinguni unapatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu ndio wanauteka.
Kwamfano, Kristo alituambia tukeshe tuombe, lengo la kusema vile lilikuwa ni kusudi tusiingie majaribuni(Mathayo 26:41), kwasababu adui yetu shetani anaishi kutuwinda. Sasa kama wewe husali, ili kuulinda wokovu wako uliopewa bure na Kristo bila kuusumbukia, unaona uvivu, ufahamu kuwa shetani atakesha kwa ajili yako, na siku ya siku ikifika atakuletea majaribu mazito, kama alivyowaletea wakina Petro usiku ule mpaka kufikia hatua ya kumkana Bwana na wengine kumtoroka uchi, unadhani walipenda? Hapana hiyo yote ni kutokana na kupuuzia kwao maagizo ambayo Yesu aliwapa muda mchache kabla kwamba wakeshe waombe, wao wakalala.
Vivyo hivyo, na wewe usipokuwa mwombaji, usipojitesa kufunga wakati mwingine, hata kutumika kwa ajili ya Kristo, ni ngumu sana kuutunza wokovu wako kama sio kuupoteza kabisa.
Hivyo, hatumwamini Yesu na kubakia hivyo hivyo tu, hapana hiyo ni hatua moja, hatua ya pili ni lazima tushindane na tupambane, tupigane vita, na tuumie ili kuulinda wokovu wetu kwasababu adui yetu shetani yupo kuuwinda wokovu wetu usiku na mchana.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Neema ni nini?
Kwanini Yakobo alimshinda Mungu, Je! Mungu huwa anashindwa na wanadamu?
NJIA YA KUPATA WOKOVU.
YEYE ALIYEUWASHA HUO MOTO LAZIMA ATALIPA.
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
Rudi nyumbani
Print this post