Si kila tunayemuhubiria, ni lazima tuone matokeo ya papo kwa papo ya badiliko.. Ni kweli tunatamani iwe hivyo kwa watu wote , na wakati mwingine ukiwa kama muhubiri unaweza kuvunjika moyo, pale ambapo unazunguka kila mahali, mwezi mzima, au mwaka mzima, kuhubiri, halafu hufanikiwi kupata tunda lolote la kudumu, au hata ukiyapata basi ni machache sana, ukilinganisha na nguvu ulizowekeza hapo.
Lakini ukiwa katika hali kama hiyo, jambo ambalo unapaswa usilitoe katika akili yako ni kuwa, mwisho wa mavuno sio siku hiyo unayohubiri, mwisho wa mavuno sio leo uliyopo mkononi mwako. Mwisho wa mavuno utakuwa ni siku ile ya mwisho, Mungu atakapotuma malaika zake, kuyatenganisha magugu na ngano. Na ngano kuziweka ghalani, sio sasa.
Mathayo 13:39b … mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika…. 49 Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki,
Mathayo 13:39b … mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika….
49 Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki,
Kwahiyo ndugu, huyo mtu unayemshuhudia/ unaowashuhudia, ikiwa hawaonyeshi badiliko leo, bado wewe endelea kuhubiri, kwasababu wakati wa kuhitimisha kila kitu bado. Pengine leo unapanda mbegu, mwingine kesho atatia maji, au wewe unatia maji leo, mwingine atapalilia, au wewe utapalilia mwingine atamalizia kuvuna,.kabla ya mwisho wa mavuno kufika.
Kwahiyo, usivunjwe moyo sana, mwisho wa dunia bado, japo upo karibu sana, hivyo wewe endelea kuingaza nuru ya Kristo katika hichi kipindi kifupi tulichobakiwa nacho, hata kama matunda hutayaona sasa. Mwachie Mungu amalize kazi zake. Kwasababu Biblia inasema..
Mhubiri 11: 4 Mwenye kuuangalia upepo hatapanda; Naye ayatazamaye mawingu hatavuna.
Songa mbele. Tangaza habari za Kristo.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya mhubiri 9:11? si wenye mbio washindao katika michezo?
AHADI YA ROHO ILIYOSALIA SASA KWA KIPINDI CHETU.
Ahera ni wapi? Kama tunavyosoma katika biblia.
UPO UMUHIMU MKUBWA WA KUMTOLEA BWANA!
Rudi nyumbani
Print this post
Ahsante mtumishi wa BABA YETU,YESU KRISTO! Mungu azidi kutupa uweza wa kuwa watoto wake kwa kuzidi kumpokea mafundisho yake(NENO LAKE)