Mbona Mungu anaruhusu watu wapate shida, ilhali ana uwezo wa kutuepusha?

Mbona Mungu anaruhusu watu wapate shida, ilhali ana uwezo wa kutuepusha?

JIBU: Kwanza tunapaswa kufahamu kuwa si mapenzi ya Mungu sisi tupitie shida yeyote ile.Lakini zipo shida na dhiki ambazo Mungu huwa anaziruhusu ziwapate wale wateule wake kwa kutimiza kusudi Fulani, aidha kwa kuwafundisha, au kwa kuonyesha utukufu wake, au kwa kuwaonya, lakini mwisho wa siku shida hizi huwa zinaishia na mwisho mwema, na ndio maana mtume Paulo alisema mahali fulani katika 

2Wakorintho 12:9 “ Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.

Kadhalika zipo shida ambazo zinatokana wanadamu wenyewe, au tunaweza kusema zinasababishwa na wanadamu wenyewe na hizo hazipo ndani ya uwezo wa Mungu kuzizua bali kwa mwanadamu mwenyewe unajua ni kwasababu gani? Jaribu kuwazia mfano huu. Kama vile sisi wanadamu wenyewe kwa wenyewe hatupendi kuchaguliwa baadhi ya mambo kwamfano kijana anapofikia hatua ya kuoa au kuolewa, mzazi mwenye busara hatoweza kwenda kumlazimisha mtoto wake aoe mke amtakaye yeye hata kama msichana huyo atakuwa ni mzuri kiasi gani, au atakuwa na maadili kiasi gani, suala la maamuzi ni la mtu binafsi. Hivyo kitu pekee atakachoweza kufanya kama mzazi mwenye busara ni kumshauri tu, na kumpa mapendekezo mema lakini si kumlazimisha, hata kama anajua huyo mke mtoto wake aliyekwenda kumchagua atakuja kumletea madhara makubwa kiasi gani mbeleni, bado hana uwezo wa kumlazimisha asimwoe. 

Na ndivyo ilivyo kwa Mungu wetu, mara zote anaona madhara yanayokuja mbele yetu, na ni kweli anatamani kuyazuia, lakini jambo analoweza kulifanya yeye kama Mungu wetu, ni kututahadharisha, au kutuonyesha jinsi mwisho wake utakavyokuwa, ili tusipotee au tusidondoke kwenye madhara. Sasa suala la kuamua kuendea au kutokuiendea njia hiyo ni la mtu binafsi. Ikiwa mtu atakubali mashauri ya Mungu basi, Mungu atamwepushia mabaya yale lakini ikiwa hatakubali basi Mungu atamwacha aangamie, hata kama Mungu atakuwa na uwezo mkubwa kiasi gani wa kumwepusha, bado hatoweza kufanya hicho kitu.

Kwasababu Mungu katuumbia sisi ndani yetu uwezo wa kuchagua.Ikiwa mtu ni mzinzi, na huku Mungu alishamwonya kuwa wazinzi hawataurithi ufalme wa mbinguni, na mtu huyo bado anaendelea katika njia zake mbovu, Hapo Mungu hawezi kumzuia japo anajua kabisa njia yake mwisho wa siku ataishia kifo, halafu aende kwenye ziwa la moto. Alimwonya shetani, hata kabla hajawa shetani, lakini hakumlazimisha asihasi, japo alijua kuwa ataasi na mwisho wa siku kuishia motoni,Mungu alimwonya lakini hakutaka kusimama katika kweli kama malaika wengine watakatifu walivyokuwa. Na ndivyo ilivyo hata kwetu,Mungu katuwekea maamuzi yetu binafsi. Kukubali au kukataa. Hakuna kulazimishwa.

Ubarikiwe


 

Mada zinazoendana:

JE! MUNGU ANASABABISHA AJALI, KWAMFANO AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE KUZAMA?

ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.

MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

MVUTO WA TATU!


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments