Maneno haya aliambiwa Nikodemo, mwalimu wa torati, Farisayo aliyemfuata Bwana Yesu kwa siri usiku na kumweleza mambo ambayo mafarisayo mwenzake wanayajua juu yake..alikiri na kusema kuwa sisi mafarisayo tunajua kabisa wewe umetoka kwa Mungu.(Lakini walikuwa wanampinga).. Lakini kabla hajafika mbali Bwana Yesu alimkatiza na kuanza kumweleza habari za kuzaliwa mara ya pili..
Yohana 3:1 “Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. 2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, TWAJUA ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye. 3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu”.
Yohana 3:1 “Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.
2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, TWAJUA ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.
3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu”.
Lakini ukiendelea utaona Nekodemo anaanza kushangaa juu ya habari hizo mpya, inawezekanijae mtu kuzaliwa mara ya pili.. Wakati anastaajabia hayo..Kumbe Bwana naye akawa anamshangaa, huyu ni mwalimu wa torati, mtu aliyebobea katika masuala ya Imani halafu halijui jambo hili wala hata hajawahi kulisikia?..akamwambia..
Yohana 3:10 Yesu akajibu, akamwambia, Je! Wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu?
Hata sasa baadhi yetu sisi wahubiri, Bwana anatushangaa sana.. Tunafundisha Neno la Mungu, tunahubiri, tunajiita wachungaji, tunajiita manabii, tunajiita mitume, tunajiita waalimu..Lakini habari za watu kuzaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho hatuzijui?, na hata kama tunazijua basi hatuzifundishi wala kushughulika nazo..
Bwana alimwambia Nikodemo kigezo cha kuingia mbinguni, ni sharti mtu azaliwe mara ya pili.. Hivyo na sisi kama hatutawaambia watu juu toba, na umuhimu wa kubatizwa kwa maji na kwa Roho Mtakatifu kamwe watu hao hawatakaa wauone(wauelewe), na wauingie ufalme wa mbinguni kwa namna yoyote ile, haijalishi watafunga kiasi gani, watafanyiwa maombezi mengi kiasi gani..watatoa sadaka nyingi kiasi gani, wataponywa kiasi gani..Kama hawajazaliwa mara ya pili basi wajue kuwa hakuna wokovu wowote ndani yao.
Tunazaliwa kwa maji na kwa Roho, hayo mambo mawili lazima yaende pamoja, pale mtu unapotubu kwa kumaanisha kabisa kuziacha dhambi zako, kwa vitendo, anapokusudia kuacha uasherati, rushwa, wizi, utukunaji n.k na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamwishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO.
Basi hapo anakuwa amepokea ondoleo la dhambi zake sawasawa na Matendo 2:38, Na anapokuwa amesamehewa dhambi zake, kinachofuata kwake si kingine Zaidi ya Roho Mtakatifu kuja juu yake wakati huo huo. Hivyo akitii maagizo hayo yote kwa kumaanisha kabisa kuanza Maisha mapya ndani ya Kristo na kwamba kuanzia huo wakati na kuendelea atamwishia Kristo kwa gharama zozote zile, na kukubali kwenda kubatizwa haraka iwezekanavyo, basi wakati huo huo Roho wa Mungu anaingia ndani yake, Na Hivyo anakuwa ameshazaliwa mara ya pili.
Jina lake linakuwa limeandikwa katika kitabu cha uzima mbinguni. Lakini endapo ukisema mimi nimeokoka, halafu unaukwepa ubatizo ni wazi kuwa bado hujamaanisha kuokoka, na kwa namna hiyo Roho Mtakatifu hawezi kuja juu yako, na ndio maana dhambi kuishinda inakuwa na nguvu juu yako.. kwasababu bado haujazaliwa mara ya pili. Hivyo tendo la ubatizo sio tendo la kulazimishwa au la kushurutishwa, au la kubembelezwa au kusukumwa sukumwa..Ni wewe mwenyewe uliyeona umuhimu wa kwenda mbinguni unautafuta kwa bidii zako binafsi, hata ikikugharimu kusafiri kwenda kutafuta ubatizo mahali mbali na ulipo unafanya hivyo kwasababu ni kwa faida yako mwenyewe.. Na ukifanya hivyo ndivyo utakavyomvutia Roho Mtakatifu kuja kufanya makao yake ndani yako kwa haraka sana, kwasababu anaona ni jinsi gani una kiu ya kuutaka uzima wa milele..Lakini kama utakuwa unavutwa vutwa, ni uthibitisho kubwa bado hujadhamiria kuwa upande wa Kristo, na bado hujaelewa umuhimu wa hicho kitu.
Ubatizo sio dini mpya, agizo la ubatizo halijatolewa na mwanadamu yeyote..Bali limetolewa na Bwana Yesu mwenyewe. Alisema..
Marko 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.
Unaona wokovu wako haukamilishwi na kuamini tu peke yake..bali pia na kubatizwa. Hivyo wewe mwenye kiu ya kuzaliwa mara ya pili, baada ya kutubu kwako, tafuta binafsi kwa bidii ubatizo. Na ubatizo sio dini mpya wala dhehebu jipya..na maagizo ya Bwana Yesu mwenyewe… Na ubatizo sahihi wa kimaandiko ni ule wa kuzamwishwa katika maji mengi sawasawa na (Yohana 3:23), na uwe kwa JINA LA YESU KRISTO sawasawa na (Matendo 2:38, 8:16, 10:48, na 19:5). Ikiwa ulibatizwa nje ya hapo au utotoni ni vema ukabatizwe tena.
Bwana akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA.
UMUHIMU WA KUZALIWA MARA YA PILI.
UZAO WA NYOKA.
KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?
KIWANGO CHA TATU CHA IMANI.
USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.
NINI TUNAJIFUNZA KWA MWANA MPOTEVU NA NDUGUYE?
Rudi Nyumbani:
Print this post